Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Mimi huwa naamini kuwa real estate ni biashara kichaa
Hii biashara inawafaa watu wenye mitaji mikubwa ambao wana focus kwenye long term plan....na sio kutegemea umeinvest leo return yake upate kesho big NO.

All in all in other way round unaweza ukajenga ukapangangisha kisha ukakopa ...hiyo nyumba ukaweka kama dhamana fedha ya mkopo utakayopata ukafanya mambo mengine....ku accerelate further investment ambazo sio real estate....
 
Kujenga nyumba za kupangisha hutakiwi kuweka mambo mengiiii, kama bati za kupaulia ni za kawaida tu, madirisha huweki dirisha za aluminum ,kwenye rangi ndiyo inupiga rangi ya ukweli, marejesho yake ni ya muda mfupi tu na faida utaiona
 
Kwa mfano kwa dar es salaam, Pale maeneo ya mlimani city njia ya kwenda chuo pembeni kuna nyumba zipo pale ni za ovyo ovyo yani chumba,sebule,jiko na choo na ndani kubovubovu tu lakini kodi ni laki3
 
nyumba za kupangisha inategemea na location, hakuna asset nzuri kama nyumba, siku umezeeka huna nguvu za kufanya kazi huku watoto wako hawaeleweki mara wengine wapiga debe, boda boda ndio utaona faida yake,
 
Wahindi wengi nchini hawamiliki nyumba ila wamefikia utajiri wa kutisha. Sisi wabantu tunakimbilia kujenga Mapinga, sijui Mkuranga watoto tunawapeleka st.kayumba bado utegemee maajabu maishani
Mkuu nikupe taarifa waarabu na wahindi ndiyo wameikamata biashara ya real estate bongo. Usiangalie vijumba vya Mkurunga, nenda prime areas mikocheni, Posta, Upanga, Masaki e.t.c kuna ma apartment ya maana wameya shusha. Wao wanafanya seriously kwakua wana mitaji mikubwa. Kuna jengo lile refu ambalo linaichungulia Ikulu, mmiliki wa lile dude ana balaa kwenye real estate industry.
 
Kwa mfano kwa dar es salaam, Pale maeneo ya mlimani city njia ya kwenda chuo pembeni kuna nyumba zipo pale ni za ovyo ovyo yani chumba,sebule,jiko na choo na ndani kubovubovu tu lakini kodi ni laki3
Hoja yako nini hapa? Kwa sababu kuwa na bahati ya kupata eneo kama hilo ni bahati sana na inatokea kwa wachache mno!
 
Wahindi wengi nchini hawamiliki nyumba ila wamefikia utajiri wa kutisha. Sisi wabantu tunakimbilia kujenga Mapinga, sijui Mkuranga watoto tunawapeleka st.kayumba bado utegemee maajabu maishani
wahindi hela zao za majini, usiwaige
 
Mkuu naomba unielezee kwa Lugha Raisi, hapo! Nikitaka kuweka mpunga wangu kwa miezi mitatu faida inakua kiasi gani, hii chart hapa chini sijaielewa.View attachment 1208896

Mfano umeweka mil 2 na tukitumia mfano interest ya 4.5% then itakua

2mili×3/12×4.5%(1-0.1)=Tsh. 20,450

Huo ndio mpunga utakaopewa mzee baba.

3/12 ni miezi 3 utayoweka pesa yako,hio 12 jumla miezi iliyoko kwa mwaka.

4.5% hio ni riba ya CRDB

10% ni kodi ya serikali kwny faida utakayopata
 
Kufanya maamuzi kati ya kujenga au kuwekeza kwenye biashara ni changamoto inayowapata watu wengi hapa nchini Hapa nitatoa maoni yangu kulingana na changamoto hii na wewe utafanya maamuzi kulingana na hali yako ilivyo.

Kama upo tayari kuingia kwenye biashara na una muda wakutosha kusimamia biashara zako nakushauri uingie kwenye biashara na uachane na kujenga kwanza . Na hii nasisitiza sana hasa kwa watu ambao hawana kipato kikubwa sana cha kuweza kujenga kwa mara moja. Nashauri hivi kwa sababu kujenga kunaweza kuwa njia ya kuzika fedha na hivyo kushindwa kuzitumia mara moja kuzalisha fedha zaidi.

Kikubwa hapa ni wewe kuamua kama kweli unataka kufanya biashara na kufikia mafanikio makubwa wekeza fedha na muda wako ulionao sasa kwenye kukuza biashara yako. Ikishakua utakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuweza kujenga au hata kununua nyumba iliyokamilika.
 
Mkuu nikupe taarifa waarabu na wahindi ndiyo wameikamata biashara ya real estate bongo. Usiangalie vijumba vya Mkurunga, nenda prime areas mikocheni, Posta, Upanga, Masaki e.t.c kuna ma apartment ya maana wameya shusha. Wao wanafanya seriously kwakua wana mitaji mikubwa. Kuna jengo lile refu ambalo linaichungulia Ikulu, mmiliki wa lile dude ana balaa kwenye real estate industry.
Kuna Mtanzania mweusi wa kujenga Apartments Mikocheni (ukiacha Kimei)?
 
Mfano umeweka mil 2 na tukitumia mfano interest ya 4.5% then itakua

2mili×3/12×4.5%(1-0.1)=Tsh. 20,450

Huo ndio mpunga utakaopewa mzee baba.
Hapa nimefaulu uwezekaji japo wankijinga ila ni,epiga bao miaka ya 2012 nilinunua shamba la miti eka 30 njombe ikiwa na miaka 4 wiki jana kwakweli nimepiga bao .... by then miliona kama ghali ila kilichonifanya ninunue nilikuwa sijapangilia nn chakufanya baada kupa mpunga flaninhivi na haikutosha kufanyia nilichopanga...... leo bei ya mti iko juu sana kwa sasa around 70000 hafi 100000
 
Back
Top Bottom