Nahisi kuna mambo kadhaa yanaachwa kwenye huu mjadala.
1: Nyumba ya kuishi Vs Nyumba ya Kupangisha.
Nyumba ya kuishi : Hapa watu tumetofautiana malengo kwenye maisha.., ukielewa hili wala hutopata tabu., mimi nimekua na ndoto zangu kua nyumba ntakayoishi lazma iwe na swimming pool lazma iwe na uwanja mkubwa garden parking ya maana n.k,
hivyo nimekua mkubwa nimejenga hivi lakini nje ya mji kidogo...kwangu mimi ..nimetimiza ndoto..na kila nikilala nikiamka...naona fahari., sasa ukiniambia nikakae sinza mfano..kwenye kijumba kama kiota cha ndege kisa tu nakaa mjini ...siwezi kukuelewa..sana sana ntakuona una shida na umaskini.
huu ni upande mmoja wa kuangalia hili suala..., watu wanajenga kwa sababu mbalimbali...wengine wana ndoto za kuishi maisha flani hivi..wengine wana familia kubwa hawawezi kupangisha chumba na sebule . n.k
Nyumba ya kupangisha: Pia kwenye hili ....inabidi tuwaze zaidi.., Wapo wanaoona hii ndo biashara salama ..hawataki stress za biashara...., ukijenga nyumba kwa mil 100, ukiwa unapokea kodi laki 5 kila mwezi...ukiwa unaila hii pesa..., tatizo liko wapi.,? kuna tofauti gani kama ungekua na hii 100mil na wewe uwe una withdraw kidogo kidogo kwenye account?
Pili: kwa wale wenye watoto., kuna njia gani safe zaidi ya kumpa kianzio mwanao zaidi ya real estate? ..mimi ninae jenga..unajuaje kama nimewajengea wanangu...baada ya hio miaka 20, wao watakua vijana na ndo wataanza ku enjoy? cha kuelewa hapa ...sio kila investment mtu anayofanya ni kwa ajili yake....
Swali la kizushi : Nyie mnaoona fahari kua mnapanga tu...hao wenye nyumba wenu wangekua na mawazo kama yenu ..mngekua mnaishi wapi?
Hitimisho: Tusijazane upepo wala kutiana ujinga... mwisho wa siku Nyumba/Kiwanja (kwa ajili ya biashara) ndo best way ya kuhifadhi pesa .., ila kwa anaetaka biashara yenye kurudisha faida haraka haraka..hio sio investment sahihi kwake.