Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Mwaka juzi nilijenga nyumba ya kisasa ya room 4.kwa ajili ya kupangisha, Lakini nilipo maliza kuweka paa, pamoja na madirisha ya chuma na milango miwili ya mbele na nyuma.wazo la kufuga kuku wa nyama likawa limeingia kichwani..Nikaacha kumalizia nyumba Naendelea na ufugaji..Kupangisha nyumba biashara kichaa.Mimi hapana

Hii ndio point yangu kuweka hela nyingi kwenye nyumba yenye return ndogo tena inayokuja kidogo kidogo ni ukichaa
 
Mtazamo wangu

Biashara ya nyumba ni biashara bora kwa watu wenye mitaji mikubwa, kwa wazee/watu wazima. Matajiri wote unaowafahamu duniani wanafanya hii biashara

Mfano wa kujenga nyumba kwa milioni 150 si halisi, kuna mtu amewekeza karibu milioni 60 kwenye moja kati ya nyumba zake na kila mwezi anaingiza milioni 1+ (hapo sio mjini kivile)

Nyumba always ina appreciate unless kuwe na special circumstance (mfano majanga, nchi kubadili sera/sheria n.k). Kuanguka kwa biashara za kawaida/zisizo real estates hakuhitaji special circumstances

Usihangaike na Real Estate kama huna mtaji wa kutosha, kwani hii biashara inaingiza faida kidogo kidogo na taratibu lakini kwa uhakika
 
Aga Khan na utajiri wooote ametapanya (diversify) utajiri wake afya (hospital), Benki, media (TV&Magazeti). Ss tunawaza kujenga vijumba (maana nyingi hazi-qualify hata kuitwa nyumba au apartments).

Point yako niya msingi sana

Sisi ni Eagle tuliototolewa na kuku sasa tunadhani sisi ni kuku. Tunachakura chakura chini na kula minyoo. Tusichojua ni kwamba sisi ni Eangle na tunaweza kupaa juu sana na kula finer things. Aga Khan yeye amejua hilo wakati sisi hatujui na ndio tofauti yetu
 
Mc cane,
Great points has point ya kwanza na ya mwisho

Biashara ya nyumba ni biashara bora kwa watu wenye mitaji mikubwa, kwa wazee/watu wazima. Usihangaike na Real Estate kama huna mtaji wa kutosha, kwani hii biashara inaingiza faida kidogo kidogo na taratibu lakini kwa uhakika
 
Mkuu hakuna investment mbaya duniani ,ila inatokana na wewe na situation yako ,ukichukua mil150,000 ukawaunachukua bidhaa china unauza Tanzania ndani ya mwaka una 400+ ,ila kama wewe ni meneja benki kama mchumi sitakushauri maana inahitaji ufuatiliaji wa hatari.

kuna mzee alikuwa muajiliwa insurance nic ,anasema alijisoma uchumi wake akawa anakopa na kununua maeneo nje ya mji by then ekari mbagala kiburugwa mil 1 ,ilipofika enzi ya kikwete akastaafu, akavuta kama mil 300 yote akaitumia kupima viwanja vyake kuvuta umeme na mabomba ya awali ya maji.

Mzee alipiga sio chini ya bil 8 ,sasa tafuta wafanyabiashara wa umri wake na hao unaosema walifungua maduka mpaka leo wapo wapo tu mzee ana ghrofa mbili kalikoo na maapartment kama yote mbezi beach na saizi analima strawberry na mapassion anapeleka mbele
 
Nahisi kuna mambo kadhaa yanaachwa kwenye huu mjadala.

1: Nyumba ya kuishi Vs Nyumba ya Kupangisha.

Nyumba ya kuishi : Hapa watu tumetofautiana malengo kwenye maisha.., ukielewa hili wala hutopata tabu., mimi nimekua na ndoto zangu kua nyumba ntakayoishi lazma iwe na swimming pool lazma iwe na uwanja mkubwa garden parking ya maana n.k,

hivyo nimekua mkubwa nimejenga hivi lakini nje ya mji kidogo...kwangu mimi ..nimetimiza ndoto..na kila nikilala nikiamka...naona fahari., sasa ukiniambia nikakae sinza mfano..kwenye kijumba kama kiota cha ndege kisa tu nakaa mjini ...siwezi kukuelewa..sana sana ntakuona una shida na umaskini.

huu ni upande mmoja wa kuangalia hili suala..., watu wanajenga kwa sababu mbalimbali...wengine wana ndoto za kuishi maisha flani hivi..wengine wana familia kubwa hawawezi kupangisha chumba na sebule . n.k

Nyumba ya kupangisha: Pia kwenye hili ....inabidi tuwaze zaidi.., Wapo wanaoona hii ndo biashara salama ..hawataki stress za biashara...., ukijenga nyumba kwa mil 100, ukiwa unapokea kodi laki 5 kila mwezi...ukiwa unaila hii pesa..., tatizo liko wapi.,? kuna tofauti gani kama ungekua na hii 100mil na wewe uwe una withdraw kidogo kidogo kwenye account?

Pili: kwa wale wenye watoto., kuna njia gani safe zaidi ya kumpa kianzio mwanao zaidi ya real estate? ..mimi ninae jenga..unajuaje kama nimewajengea wanangu...baada ya hio miaka 20, wao watakua vijana na ndo wataanza ku enjoy? cha kuelewa hapa ...sio kila investment mtu anayofanya ni kwa ajili yake....

Swali la kizushi : Nyie mnaoona fahari kua mnapanga tu...hao wenye nyumba wenu wangekua na mawazo kama yenu ..mngekua mnaishi wapi?

Hitimisho: Tusijazane upepo wala kutiana ujinga... mwisho wa siku Nyumba/Kiwanja (kwa ajili ya biashara) ndo best way ya kuhifadhi pesa .., ila kwa anaetaka biashara yenye kurudisha faida haraka haraka..hio sio investment sahihi kwake.
 
Mina cute,
Linganisha nyumba ya kupanga na lodge ili tuone ipi inalipa zaidi? Au lodge watu wanaziogopa kutokana na imani za kidini?
 
bonna,
Na kwakuongezea, jamani biashara sio rahisi kiasi hicho mnachofikiri!! Ni rahisi kusema "hii milioni 100 bora niifanyie biashara halafu faida ntakayopata ndio nitumie kujenga".. Nani kakuambia utapata faida? Kwanza kwenye biashara milioni 100 ni pesa ndogo sana ambayo ukicheza wala hutajua ilipoenda! Wapo watu wengi wameingiza pesa kwenye biashara na mwisho wakatoka mikono mitupu.

Uzuri wa kujenga ni kua angalau utaiona hiyo nyumba na angalau utakua na uhakika wa hizo laki 5 kwa mwezi kwa maisha yako yote na pia unaweza kuitumia kama dhamana kukopea,na ukifariki bado watoto wanakua na kitu cha kugombania
 
TheChoji, Biashara Mil 100 ndogoo????[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji33][emoji33][emoji33] Au unataka kuanzishaa viwandaa mkuuu.. Hio mil 100 naweza anzisha hata biashara zenye faida nzuri 3.
 
bonna,
Ushauri wako ni mzuri kwani umegusa engo zote fair and balanced.

Pia tuko wote katika hili hapa - na mimi ndoto zangu ni kama zako

mimi nimekua na ndoto zangu kua nyumba ntakayoishi lazma iwe na swimming pool..lazma iwe na uwanja mkubwa..garden..parking ya maana n.k
 
Makini sana

Huyo mzee ni investor na wala sio mfanya biashara. Amepiga hela za masafa marefu
Ndo maana namshauri dada akae na manguli wa biashara asiegemee wazo moja kinachokufaa wewe siwezi mshauri mwingine ,mkinga anakuja mjini anafungua kiduka, hapangi nyumba anaishi humo humo na mkewe na mtoto mdogo badae anajenga ndo anahama hataki show off za kupanga ,nyumba yenyewe anajenga.

Chumba kimoja anahamia, kwa miaka kumi analima ekali 20 kila ukiona anajifanya anaenda krismas na familia siku anapasua miti unashangaa ananunua ghorofa kaliakoo kwa ujinga eti ohh ni wachawi kaduka haka ndo anunue ghorofa hebu ulizia bei ya ekari ishirini zenye miaka muni zinauzwaje.
 
'Leo nikiuza ni pesa ndefu sema fixed assets kwa sasa kuuzika kwa bei nzuri ni mtihani'.

Umejichanganya kwny hio sentensi.

Sasa utamuuzia nani akupe hio pesa ndefu?
Sijajichanganya mkuu. Pesa niliyonunulia nyumba haikuwa kubwa sana kwa kuwa hakukuwa na dalali kabisa. Ni mtu tulifanya biashara akafuraji ndipo akaniambia anauza nyumba. Hivyo kama nilinunua bei nzuri na leo hii ni 20 times the original price je kwani nikipata now say 15 times the iriginal price siyo pesa ndefu?
 
The only,
Hujaeleza vizuri hizo Bilioni 8 alizipataje na akazitumia kufika hapo alipo. Umecomment kifupi hebu andika maelezo marefu ya kueleweka mkuu.
 
Hujaeleza vizuri hizo Bilioni 8 alizipataje na akazitumia kufika hapo alipo. Umecomment kifupi hebu andika maelezo marefu ya kueleweka mkuu.
mkuu huyu ni mtu hai anakampuni inaitwa Taj...... watoto wa mjini washamjua ,kwa awamu hii kumwaga madetail usije mletea matatizo mzee wa watu ,elewa 1990-1999 ardhi dar hususani mbagala,kigamboni tegeta etc ilikuwa bwerere ,kuna jamaangu aliwahi nunua nyumba ya vyumba 3 2008 upande wa pili wa mlimani city kwa mil 22 ,leo hata akitaka 200 + anakamata ,ishu sio kununua nyumba unanunua strategically
 
Back
Top Bottom