Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

wazo poa sana!
 
Hakuna kitu kinaitwa pesa za ziada,na hakuna pesa isiyokuwa na matumizi,vali ni maamuzi ya kuacha hiki na kufanya kile.
 
Kwa taarifa yako hamna watu wame invest Properties kwenye PRIMARY AREAS kama wahindi, ila wako very strategic. We angalia toka Askari monument, Samora Avenue mpaka unafika Clock Tower ni majengo mangapi ya wahindi ndio utapata jibu
Prime areas not Primary...
Pia the guy is right wahindi wengi wanakaa kwenye rental properties hizo unazoongelea wewe ni za investment na ni wachache wamefanya hvyo,
 
Hongereni wote kwa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (Doctor of Philosophy, PhD) pale Mlimani City.
 
Vipi kama hiyo nyumba ikawa ni guest?
 
Ngwanakilala,
Kama mwenye hiyo hela kaamua hivyo sioni ubaya. Nyumba itarufisha hiyo hela hata atakapokuja ishi mjukuu. Kam hauna pa kuwekeza jenga nyumba.
 
Nimepata wazo zuri sana hili litanisaidia mbeleni huko Mungu akijaalia
 
Jenga nyumba kwa ziada ya pesa unayopata. Usijenge nyumba kwa mkopo au pesa ya biashara.

Kwa mfano unatoa 20milioni kujenga msingi na kusimama kwa Mwaka mmoja,huku biashara yako 20 milioni kwa muda huo unapata 6-8milioni.

Sema basi tu sababu ya kasumba ya kiafrika ila ujenzi wa nyumba nao unachangia umaskini.
 
Binafsi kwa maono yangu,ukijenga nyumba ya m.100 na mungu akakusaidia mambo yako yakawa yanaendelea kwenda nyumba kakopee haha m.70 au 100 maisha yaendelee kwa sababu faida ya nyumba ni kukopea tu kopa pesa endelea kupigana huko
 
Ulijenga maeneo gani kaka
 
Just imagine alienunua kariakoo nna kujenga nyumba akiuza saivi ana make mkwanja gani

Kwetu tulinunua kiwanja laki 4 hapo dar wilaya ya ubungu 1994 tulianza kujenge mdogomdogo haki ikawa nyumba kubwa enzi hizo hili eneo lilikuwa nyumba moja moja Ila leo zimekuwa nyingi Hadi biashara zinatembea kweli just imagine tukiuza hiyo nyumba leo tuna kiasi gani

Cost za ujenge wa nyumba na thamani ya kiwanja muda ule hata 15 milioni sidhani Kama inafika Ila leo tunaweza una hio nyumba sio chini ya 50m maana sio ya kisasa sana



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara ni kipaji na si wote wanaweza kufanya biashara na kufanikiwa kwa kiwango kile anachokitamani.Kuwekeza fedha kwenye biashara kuna kupoteza au kufanikiwa.Kwa wale ambao hatuna uzoefu au kipaji kwenye biashara huwa tunakimbilia kwenye ujenzi tukiamini kule hela haipotei hata kama hakutakuwa na faida.
Pia inategemea na chanzo cha fedha au mtaji;kwa mfano ukiangalia wanaojenga viwanda,hotel n.k kwa asilimia kubwa wanatumia mikopo..na wanaamini hata wakishindwa kurejesha mikopo hiyo lile jengo litatumika kama 'bond'.Kwa hiyo inategemea na kipaji cha mtu husika katika biashara.
 
1994-2020 = 15m-50m?
 
Ukitaka kufaidi biashara ya guest nenda ikwiriri tengeeza guest za kawaida za 10000
Nimekuwa nasafiri sana kwenda ikwiriri sijawahi pata guest bila kuweka oda. Ikifika satatu waweza kuzurura mji mzima mwisho ukalala stendi
Ikwiriri ndo wapi?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…