Arien
JF-Expert Member
- Aug 29, 2017
- 11,245
- 11,767
wazo poa sana!1.Kwenye hiyo 150m angeweza kuweka Fixed Deposit ambapo kwa sasa hivi kama ni mzuri ktk bargaining anaweza akapata 13% ingawa competitive rate iko kwenye 11% mpaka 12% ambayo inamhakikishia more than 15m kwa mwaka
2. Anaweza akaweka FD ya hiyo 150m akaendelea ku enjoy interest ambapo ile Fixed Deposit Receipt/Certificate anaweza akaitumia kama collateral na kwa taratibu za kibenki FD ya Tshs 150m anaweza kupata mkopo wa Tshs 120m. Ambazo hizo 120m anaweza kujenga apartment units 2 au 3, anakuwa na double income(interest + rent)
Mara nyingi Mortgage loans huanzia miaka 5 mpaka 15 hivyo installments zake zinakuwa ndogo ndogo sana ambazo zinaweza kukufanya ktk miaka 5 zile units 2 au 3 na ile Fixed Deposit zikajiongeza ukawa una uwezo tena wa kuongeza unit nyingine
Utakuwa unaenda hivyo mpaka miaka 10 unajikuta una 5 au 6 units
Yaani kadri Mortgage outstanding amount inapopungua ndipo unapopata nafasi ya ku renew mikopo na kuongeza apartment unit nyingine
Suala la location ni muhimu sana unaweza chagua location za Uswazi ukajenga kwa gharama nafuu na wapangaji wengi, vyumba vingi nk
Au unaweza jenga sehemu za Kishua nyumba zenye gharama, wapangaji much knower wasiotabirika, na bei zisizotabirika za kodi. Tatizo la maeneo haya ya kishua uchumi ukitikisika kidogo kama hivi sasa rent nazo zinatikisika kitu ambacho huku Uswazi hakuna kwa sababu watu wanaoshindwa kulipa kodi Ushuani ndio hao hurudi huku kwa akina Yahe. All in all kuwa na mbinu madhubuti na kujua who is the right Financier ni kitu cha muhimu sana. Sio kila bank iko friendly ktk Mortgage Financing, unaweza kuta out of 58 registered banks tulizonazo ni 3 au 5 ndizo ziko friendly katika Mortgage Financing
Kwa maoni yangu mimi biashara ya nyumba mtaji wa chini kabisa unatakiwa uwe nao ili biashara ikuwe, watoto wasikose nyama, na loan installments zilipwe vizuri basi usipungue Tshs 350m