Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

1.Kwenye hiyo 150m angeweza kuweka Fixed Deposit ambapo kwa sasa hivi kama ni mzuri ktk bargaining anaweza akapata 13% ingawa competitive rate iko kwenye 11% mpaka 12% ambayo inamhakikishia more than 15m kwa mwaka

2. Anaweza akaweka FD ya hiyo 150m akaendelea ku enjoy interest ambapo ile Fixed Deposit Receipt/Certificate anaweza akaitumia kama collateral na kwa taratibu za kibenki FD ya Tshs 150m anaweza kupata mkopo wa Tshs 120m. Ambazo hizo 120m anaweza kujenga apartment units 2 au 3, anakuwa na double income(interest + rent)
Mara nyingi Mortgage loans huanzia miaka 5 mpaka 15 hivyo installments zake zinakuwa ndogo ndogo sana ambazo zinaweza kukufanya ktk miaka 5 zile units 2 au 3 na ile Fixed Deposit zikajiongeza ukawa una uwezo tena wa kuongeza unit nyingine
Utakuwa unaenda hivyo mpaka miaka 10 unajikuta una 5 au 6 units
Yaani kadri Mortgage outstanding amount inapopungua ndipo unapopata nafasi ya ku renew mikopo na kuongeza apartment unit nyingine
Suala la location ni muhimu sana unaweza chagua location za Uswazi ukajenga kwa gharama nafuu na wapangaji wengi, vyumba vingi nk
Au unaweza jenga sehemu za Kishua nyumba zenye gharama, wapangaji much knower wasiotabirika, na bei zisizotabirika za kodi. Tatizo la maeneo haya ya kishua uchumi ukitikisika kidogo kama hivi sasa rent nazo zinatikisika kitu ambacho huku Uswazi hakuna kwa sababu watu wanaoshindwa kulipa kodi Ushuani ndio hao hurudi huku kwa akina Yahe. All in all kuwa na mbinu madhubuti na kujua who is the right Financier ni kitu cha muhimu sana. Sio kila bank iko friendly ktk Mortgage Financing, unaweza kuta out of 58 registered banks tulizonazo ni 3 au 5 ndizo ziko friendly katika Mortgage Financing

Kwa maoni yangu mimi biashara ya nyumba mtaji wa chini kabisa unatakiwa uwe nao ili biashara ikuwe, watoto wasikose nyama, na loan installments zilipwe vizuri basi usipungue Tshs 350m
wazo poa sana!
 
Hakuna kitu kinaitwa pesa za ziada,na hakuna pesa isiyokuwa na matumizi,vali ni maamuzi ya kuacha hiki na kufanya kile.
Hujaelewa topic mkuu.
Kujenga sio dhambi ila unachoambiwa Ni kwamba jenga kwa pesa ya ziada.
Yaani usijitese na kumaliza pesa yote kwa ajili ya kujenga.
Kwa hiyo naamini hata hao wahindi wanajenga lakini kwa pesa ya ziada,yaani hawezi kuchukua pesa iliyo kwenye mzunguko wa biashara ili ajengee.
 
Kwa taarifa yako hamna watu wame invest Properties kwenye PRIMARY AREAS kama wahindi, ila wako very strategic. We angalia toka Askari monument, Samora Avenue mpaka unafika Clock Tower ni majengo mangapi ya wahindi ndio utapata jibu
Prime areas not Primary...
Pia the guy is right wahindi wengi wanakaa kwenye rental properties hizo unazoongelea wewe ni za investment na ni wachache wamefanya hvyo,
 
Hongereni wote kwa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (Doctor of Philosophy, PhD) pale Mlimani City.
 
Mawazo yako ni sahihi sana tena makini sana. Haya mambo unaonekana unayaelewa sana hasa uliposema

Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
Vipi kama hiyo nyumba ikawa ni guest?
 
Ngwanakilala,
Kama mwenye hiyo hela kaamua hivyo sioni ubaya. Nyumba itarufisha hiyo hela hata atakapokuja ishi mjukuu. Kam hauna pa kuwekeza jenga nyumba.
 
Hii biashara inawafaa watu wenye mitaji mikubwa ambao wana focus kwenye long term plan....na sio kutegemea umeinvest leo return yake upate kesho big NO....all in all in other way round unaweza ukajenga ukapangangisha kisha ukakopa ...hiyo nyumba ukaweka kama dhamana fedha ya mkopo utakayopata ukafanya mambo mengine....ku accerelate further investment ambazo sio real estate....
Nimepata wazo zuri sana hili litanisaidia mbeleni huko Mungu akijaalia
 
Jenga nyumba kwa ziada ya pesa unayopata. Usijenge nyumba kwa mkopo au pesa ya biashara.

Kwa mfano unatoa 20milioni kujenga msingi na kusimama kwa Mwaka mmoja,huku biashara yako 20 milioni kwa muda huo unapata 6-8milioni.

Sema basi tu sababu ya kasumba ya kiafrika ila ujenzi wa nyumba nao unachangia umaskini.
 
Binafsi kwa maono yangu,ukijenga nyumba ya m.100 na mungu akakusaidia mambo yako yakawa yanaendelea kwenda nyumba kakopee haha m.70 au 100 maisha yaendelee kwa sababu faida ya nyumba ni kukopea tu kopa pesa endelea kupigana huko
 
mnajidanganyaaa, Nyumba ya kupangisha inalipa sana, inategemea na eneo tu, mi nna Chumba sebule jiko, napangisha laki na nusu, na upande mwingine Ivyo Ivyo,

Yaan Nyumba moja ila ina pande mbili, kwaiyo nakusanya laki tatu kwa mwezi, na ya kawaida tu nje, ila ndani finishing nzuri,

Imenigharimu milioni 30,kujenga,
nimepaulia miti badala ya mbao za 4by 2..ila kwa upande wa 2by2 nimetumia mbao za Dawa, pia fishabodi mbao za dawa, mabati nimenunua ya gage 32 kwa Bei ya 16,000. Nimetumia bati sabini na tano tu, nyumba inalipa sana, ila usijenge kitajiri kama ni yakupangisha, na ikibidi mpaka mchanga nenda kanunue mwenyewe usimtume mtu, na misumari pia kanunue mwenyewe,

Yaan iyo million 150 mi najenga nyumba nne hapo za kodi ya laki tatu kwa mwezi,, ela Ya urithi niliifanyia jambo la maana nashukuru kwakweli
Ulijenga maeneo gani kaka
 
The higher the risk the higher the return ingawaje parameter zinatofautiana but remember Asset nyingi ambazo sio current kama nyumba na kiwanja zinagain thamani kila siku just imagine mwenzio aliyenunua kiwanja ubungo miaka 20 iliyopita nakujenga nyumba kwa Milioni 10 sasa hv akipauza Anapauza kwa kiasi gani? Je hakuna Return on investment ya maana kweli?
Just imagine alienunua kariakoo nna kujenga nyumba akiuza saivi ana make mkwanja gani

Kwetu tulinunua kiwanja laki 4 hapo dar wilaya ya ubungu 1994 tulianza kujenge mdogomdogo haki ikawa nyumba kubwa enzi hizo hili eneo lilikuwa nyumba moja moja Ila leo zimekuwa nyingi Hadi biashara zinatembea kweli just imagine tukiuza hiyo nyumba leo tuna kiasi gani

Cost za ujenge wa nyumba na thamani ya kiwanja muda ule hata 15 milioni sidhani Kama inafika Ila leo tunaweza una hio nyumba sio chini ya 50m maana sio ya kisasa sana



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara ni kipaji na si wote wanaweza kufanya biashara na kufanikiwa kwa kiwango kile anachokitamani.Kuwekeza fedha kwenye biashara kuna kupoteza au kufanikiwa.Kwa wale ambao hatuna uzoefu au kipaji kwenye biashara huwa tunakimbilia kwenye ujenzi tukiamini kule hela haipotei hata kama hakutakuwa na faida.
Pia inategemea na chanzo cha fedha au mtaji;kwa mfano ukiangalia wanaojenga viwanda,hotel n.k kwa asilimia kubwa wanatumia mikopo..na wanaamini hata wakishindwa kurejesha mikopo hiyo lile jengo litatumika kama 'bond'.Kwa hiyo inategemea na kipaji cha mtu husika katika biashara.
 
Just imagine alienunua kariakoo nna kujenga nyumba akiuza saivi ana make mkwanja gani

Kwetu tulinunua kiwanja laki 4 hapo dar wilaya ya ubungu 1994 tulianza kujenge mdogomdogo haki ikawa nyumba kubwa enzi hizo hili eneo lilikuwa nyumba moja moja Ila leo zimekuwa nyingi Hadi biashara zinatembea kweli just imagine tukiuza hiyo nyumba leo tuna kiasi gani

Cost za ujenge wa nyumba na thamani ya kiwanja muda ule hata 15 milioni sidhani Kama inafika Ila leo tunaweza una hio nyumba sio chini ya 50m maana sio ya kisasa sana



Sent using Jamii Forums mobile app
1994-2020 = 15m-50m?
 
Ukitaka kufaidi biashara ya guest nenda ikwiriri tengeeza guest za kawaida za 10000
Nimekuwa nasafiri sana kwenda ikwiriri sijawahi pata guest bila kuweka oda. Ikifika satatu waweza kuzurura mji mzima mwisho ukalala stendi
Ikwiriri ndo wapi?.
 
Back
Top Bottom