Ngwanakilala
JF-Expert Member
- Jun 25, 2011
- 774
- 1,464
- Thread starter
-
- #21
20.8333333333 miaka mpaka hela yako irudi na hapo kila kitu kiwe kizuri bila maintanance tc (which is next to impossible) Labda kama ulivyosema kuwa fadha ambazo huna kazi nazo...
Sisi watu weusi nyumba ndio fahari yetu na vijukuu vyetu
Mimi huwa naamini kuwa real estate ni biashara kichaa
inategemea hiyo nyumba umeijengaje.. na umeijenga wapi...
kwa milioni 20 tu watu wanajenga nyumba na wanapangisha laki 5 .. hapo mchawi location tu..
Kuna mmoja yeye ni dereva kwenye ubarozi wa nchi ya kibeberu flani. Amechukua mkopo milio 30,Genius
Asante sana. Umetoa somo mubashara sana Chief.
Wengi sana wakichukua mikopo hufanya makosa kama ulivyoainisha hapo juu nakuishia kulia na kuhangaika. Sometimes mkopo hubadilika kua laana. Asilimia kubwa sana ya watu hawana elimu uliyotoa hapa - wengi sana
Ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00. Itakupa rental yield ya 4.8%, siyo nzuri saana, lakini haijambo.
Rental yield ya kuanzia 7% kwenda juu ni nzuri zaidi. Nyumba ni long-term investment. Wanaweza kuja kufaidi matunda watoto wako/wajukuu/vitukuu. Kila kitu ni timing. Hali ya real estate Tanzania kwa sasa ni tete sana.
rental yield unaipata kwa formula gani??
mfano nikijenga nyumba kwa milion 20 nikapangisha kwa laki 4 kwa mwez.. rental yield ni ngapi?