Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Real Estates ni kupiga Apartments na maofisi. Sio kujenga kanyumba kamoja kisha unasubiria kodi zije. Halafu nadhani kuna namna ya management ya Real estates.

Donald Trump ni Mogul wa hizo biashara toka enzi. Labda tumuulize

Tatizo moja wapo ya biashara hii, ni Management:-
Kuanzia hatua ya kuchagua kiwanja, location, ujenzi wa nyumba au jengo lenyewe, n.k.

Management ikiwa mbaya, nyumba au jengo lililotakiwa kujengwa KWA milioni 20 KWA mfano, linaweza kujengwa KWA gharama ambayo ni Mara mbili ya hapo. Elimu ktk fani ya Management ndio tatizo kubwa zaidi KWA sisi Watu weusi, tena ni tatizo sugu liliotushinda KWA kiwango kikubwa.
 
Ni kweli kwa hilo wahindi wanapatia sana

Nilifanya kazi benki kati ya mwaka 2013 mpaka 2015 na nilikua na process applications za products fulani ambazo zililazimu kuona salary slips na savings za watu. Nilishangaa kuona wahindi wengi wana hela benki kati ya million 50 mpaka 100 na zaidi lakini kwenye makazi wameandia STAYING WITH PARENTS
Hahahaha,Sasa mbongo akipata milioni 5 tu hashikiki na baa zote zitamjua Kama ana hela na akili zinavurugika hasikii la muhadhini wala mnadisha swala.
 
Real Estates ni kupiga Apartments na maofisi. Sio kujenga kanyumba kamoja kisha unasubiria kodi zije. Halafu nadhani kuna namna ya management ya Real estates.

Donald Trump ni Mogul wa hizo biashara toka enzi. Labda tumuulize
Issue we mtanzania wa kawaida hicho kipato unatoa wapi

Labda uwe mfanya biashara
 
Hahahaha,Sasa mbongo akipata milioni 5 tu hashikiki na baa zote zitamjua Kama ana hela na akili zinavurugika hasikii la muhadhini wala mnadisha swala.
🤣🤣🤣🤣🤣 wahindi wana hela sana aisee.
 
600,000 × 12 = 7.2m kwa mwaka.
150m ÷ 7.2m = 29 years ili pesa yako irudi. Hapo hijaweka hata senti tano ya services and replacements na usumbufu wa wale wapangaji jeuri.

Tuone kama utaweka fixed acc kwa walau 8% interest kwa mwaka.

8% times 150m = 12m
Kwa miaka 29 = 348m

After 29 years tuna watu wawili hapa baba mwenye nyumba na huyu Mzee wa fixed account...Haya wachumi tusaidieni hapa nani kapata zaidi?

Mmoja ana nyumba yake na kiwanja na mwingine ana 348m + 150m =498m

Nani mjanja?? Wekeni na approx land value baada ya hiyo miaka 29.

Mjenzi ana nyumba 150m + vakue ya kiwanja after 29 years.
 
Mkuu kuna kitu haujui kwenye real estate business.., nayo ni Other Peoples Money.., pia kitu kinaitwa Property Ladder..

Moja hakuna mtu wala sio busara kujenga nyumba kwa cash au pesa yako.. (it takes long kwa return on investment)

Hivyo basi katika hii real estate.., mtu anakopa benki anajenga nyumba hata ikichukua miaka 20 kurudisha ile pesa, hajengi moja..., hio aliyoshajenga anaiombea mkopo benki anajenga nyingine na nyingine na nyingine hii miaka 20 inakuwa sio ya kupata pesa ya kula bali wapangaji ndio wanaomnunulia hizo nyumba.., after the end of 20 years anakuwa amejenga nyumba bila kutumia senti yake hata moja.. (thus other peoples money)... na property ladder unaanza na nyumba moja unakopa unajenga ya pili, tatu, nne n.k.

Cha maana ni Location, Location, Location na sio muda wa kumaliza hio investment.., Walijisemea wachina wote tungetaka kupata kivuli cha miti tunayopanda hakuna mtu angepanda mti..., 20 years in nothing if someone else is paying..

nakuacha na msemo mwingine "As Safe as a House..."

Mawazo yako ni mazuri. Very strategic and technical. Nimeyapenda
 
🤣🤣🤣 hesabu za Present value na future value lazma zihusike. ROI, ROCE na wenzake

600,000 × 12 = 7.2m kwa mwaka.
150m ÷ 7.2m = 29 years ili pesa yako irudi. Hapo hijaweka hata senti tano ya services and replacements na usumbufu wa wale wapangaji jeuri.
 
Ulaya wengi wanakufa bila nyumba! Wanapanga mpaka mwisho wa maisha yao. Kuwa na pesa ya kutosha kwenye akaunti inawatosha... Mambo ya nyumba kufa ama kupona ni yetu Waafrika.
Kama tayari kuna 72M, hata ikiuzwa 180M sioni ubaya. .
Ulaya mtu anakopa nyumba au apartment. Anakuwa analipa riba kwa miaka. Deni lake linabaki like lile. Value ikipanda, anauza na kulipa ile principal na faida juu.
Ile riba inakuwa kama kodi ya nyumba tu.
 
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.

Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).

Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
Umemaliza nilichotaka kusema. Kama una malengo maalum mfano kulipia watoto ada huku ukilinda hiyo pesa ni vyema ukawekeza kwenye nyumba. Mfano hapa Tabata kuna mzee ambaye namfahamu alinunua kiwanja miaka kama 17 imepita kwa 10m ni kiwanja kikubwa kwa hapa mjini akajenga nyumba 2 za kupangisha vyumba 2 na sebule self na bado eneo likabaki kubwa. Mwaka jana eneo lililobaki kama 500sqm aliliuza kwa 22m, na kila mwezi anachukua laki 5 kutoka kwenye hizo nyumba.
Kama malengo ilikuwa ni kusomesha watoto basi wanasoma vzr, na thamani yake kwa sasa ni kubwa zaidi ya ile ya mwanzo.
Kuna jamaa yangu naye akitaka kufanya biashara hachukui hela yake. Yeye anajenga nyumba na kisha anaenda kuchukua mkopo benki halafu anendelea na biashara huku nyumba akiwa amepangisha.
Ni malengo tu.
Na umri pia, kwa sababu wanaofanya uwekezaji wa nyumba namna hiyo ni wale ambao umri umeenda na kama ni wafanyakazi wanakaribia kustaafu na hiyo inakuwa sehemu ya kuwapa hela kidogo kidogo
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hesabu za Present value na future value lazma zihusike. ROI, ROCE na wenzake
Nyumba ya Laki 6 leo baada ya miaka 5 itakuwa laki 4 kama sio 3[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Maisha yanaenda kasi sana Hizi hesabu za kwenye makaratasi achana nazo kabisaa... Watu hawajifunzi kwa Jiwe tuu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi wife ananiboa anaponiambia tujenge lijumba wakati mtaji wa kujenga nyumba naimarisha shamba langu la ng'ombe

Ng'ombe unauza maziwa unapata mahela bado ng'ombe yupo ndama yupo na mbolea juu.

Miradi inalipa sio majumba sijui ni matakataka gani na kaahidi tutaachana kama sitajenga

Mimi ndio kwanza nanunua ng'ombe mwingine na wengine watatu wanazaa next month yeye ananiletea mambo ya majumba

Bili ya lita mbili nakaa mjengo wa heshima hapa mjini

Nashuri uchumi ufundishe kuanzia std III
 
Business kwa mazingira yetu sio guarantee, lakini pia ujenzi wa nyumba kusastain maisha yako ya kila siku nayo ni changamoto kama huna mtaji mkubwa..

Baadala ya kujenga nyumba for 100 -150mil kwa maana ya biashara ni bora ukawa na shamba la minazi au miti la 20heka for 5yrs ambayo itakugharimu labda 20mil na baada ya hapo unaanza kuuza nazi miaka nenda rudi.... Ukanunua mchele au Mpunga na mahindi ukauza sehemu mbalimbali just to sustain your daily life.. Hapo utakuwa umeinvest labda 50mil na 100mil unapigilia fixed ambayo utakupa 8mil/year...

Ujenzi wa nyumba wakati mwingine ni kama uoga wa maisha maana 150mil inaweza yenyewe ikajenga nyumba ya 150mil for 5yrs na maisha mengine yakaendelea...
ONYO NA TAHADHARI : usiingie kwenye biashara na 150mil kama hukuwahi kufanya biashara, you will only be safe kwa kufanya biashara ambazo ni risk free kama daladala au ujenzi wa nyumba..

150mil inaweza kununua 3coaster zikawa daladala mjini .. Hesabu 100k mpaka 80k ukichukua 80k x 30 x 3 = 7.2month.. Assume ubovu wa gari, service, mabao, mizinguo ya dereva na konda kwenye hesabu, laza 4mil monthly kula 2mil/month weka akiba 2mil/month yearly utakuwa na 24mil ukienda 3years itakuwa 72mil uza zote kwa 25x3 = 75mil vuta nyingine tatu and the circle continue life goes on.
 
Ulaya wengi wanakufa bila nyumba! Wanaanga moaka mwisho wa maisha yao. Kuwa pesa ya kutosha kwenye akaunti inawatosha... Mambo ya nyumba kufa ama kupona ni yetu Waafrika.
Ushasema ulaya

Lakini wengi wana mortgage
Baada ya miaka say 20 inakua yako

Kama hapa kwetu tu ishakuja hio style

Issue sasa una kipato cha uhakika ili wakate for 20yrs?.

Inabidi ulinde ajira yako ama biashara
 
Unaweza kukuta jamaa ana PhD ya Kiswahili toka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI)
Hahahaha,hawa ndio wale wanajiitaga wazalendo hata watoto wao wakiomba hela ya nauli ya kwenda shule anawaambia watembee kwa miguu.
Wakiomba hela ya askirimu anawapa hotpot limejaa mihogo.
 
Back
Top Bottom