Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Goba viwanja bei gani? Ukitoka barabara kuu ya lami huko ndani kuna barabara nzuri?
Miaka km miwili imepita nliambiwa nkaangalie eneo dogo tu milioni 20,lafaa kwa makazi lakini...sikujua ht ni sq mita ngapi..ss sijui saivi sh ngapi..

Goba sehemu nyingi mabonde kupanda na kushuka kwa hio inabidi kudesign ujenzi.,wengi washapawezea

Barabara za ndani kwa nilizopita ni mabonde labda kama wameshazilima..lami ndani bado

Kwa ujumla ni pazuri pameshachangamka mnooo,panakua mjini kwa kasi.,hata kupangisha nyumba panafaa zaidi ya sana
 
Hizi ndio mada nazoweza soma na kuchangia at least, nitarudi kueleza mawazo yangu baadae, nitapishana na mzungunzaji mkuu!
 
Ni kweli. It is a long term investment wala sio biashara ya mzunguko
Mkuu kwanini mnasema mjengaji haoni faida wakati anachukuwa kodi mara nytumba inapomalizika.? Tatizo wewe unadhani mpaka fedha ulizowekeza zirudi zote ndiyo faida ianaanza kuonekana!. Real Estate ni biashara nzuri sana na ukishajenga wewe unakuwa huna tena stress za leo biashara imekuwa mbaya au kesho nitafanya nini. Hiyo hiyo kodi unayochukuwa kila mwezi ndipo ilipo faida. Cha kuzingatia ni kufuata kanuni za kujenga nyumba ya biashara. Kama ni ya kupangisha ina kanuni zake.
 
Too much pilipili
Mimi najifunzaga kwa Wahindi bora upange mtaji peleka kwa biashara

Wahindi wengi wamepanga nyumba siyo kwamba hawana pesa za kujenga, LA hasha, pesa wanazo isipokuwa wanaogopa kujenga wakihofia wasije wakanyang'anywa tena nyumba zao kama walivyofanyiwa wakati wa Mwalimu Nyerere enzi za Azimio LA Arusha.. Wengi wanahifadhi pesa zao, hata kama mambo yakija kugeuka baadaye waweze kukimbilia zao nchini India. Kama ujuavyo, watawala wa Afrika hawatabiriki.
 
Ukijenga nyumba ya 150m Magomeni Kagera utapata bei gani? Trust me kuna nyumba za zaidi ya 150m hapo Magomeni Kagera kama unaelekea kwa Mtogole. Watu wa real estate wanasema LOCATION,LOCATION,LOCATION.

Bwana mkubwa yule ana uelewa mdogo
 
Good Analysis, lakini real estate inachangamoto na ni kama kamari fulani kwa mtu ambaye huna mtaji mkubwa.

Rear estate kwa matajiri ni biashara nzuri na ni nzuri for the long term ya vizazi na vizazi lakini kwa mwezangu na mimi ambaye unahitaji kuwa na daily income ya kusustain maisha ya kila siku naiona kama ghost business.

Mawazo yangu mimi ni kama yako wewe Boss
 
Umepata hiyo pesa, yote Ukaizike!? Huo ni wendawazimu wa hali ya kutosha. Kama unawashwa na kujenga, toa hats mil 30 ukajenge nyumba iishe kabisa uhamie hiyo nyingine iweke kwenye mzunguko wa biashara ya kuaminika na uifanye wewe mwenyewe.

Nilishasema sitokaa niyaogope maisha nikimbilie kuizika pesa(kujenga) niache kuiweka kwenye biashara kwa kuogopa kupanga.

Chukulia mfano, umeenda kujenga Mbande au Kisewe huko Mbagala, shughuli zako ziko Tegeta na huko ndiko ulikokuwa umepanga mwanzoni.

Uko sahihi kabisa

Hata mimi naamini kujenga ni uoga wa maisha nani mawazo yakizamani. Business models are changing we also must change
 
Mina cute, Huoni wewe pia itahitaji miaka 10 kubreak even
Bado ndani ya hiyo miaka 10 kuna marekebisho mengi na pia nyumba nzuri na mpya zitajengwa hivyo itakubidi upunguze bei
 
Kuna nyumba fulani ipo ilala ilianza kuuzwa 1.2bil hadi leo ipo 600m haijauzwa imepita lami hadi kwenye hio nyumba, pia kuna kasri moja lipo karibu na chuo cha DSJ yani ni opposite na DSJ linauzwa 1.2bil hadi leo halijajengwa hio nyumba ukitoka nje tu lami ukitembea dakika 5-7 umefika kituoni lakini bado hakuna wanunuzi
Mifano yako haifanyi biashara ya nyumba iwe mbaya kwa kila mtu. Hata huko kwenye biashara nyingine kuna mifano kibao ya watu waliofeli.
 
Huoni wewe pia itahitaji miaka 10 kubreak even
Bado ndani ya hiyo miaka 10 kuna marekebisho mengi na pia nyumba nzuri na mpya zitajengwa hivyo itakubidi upunguze bei
Hii biashara kichaa sio ya Kufanya kwa kutumia hela ya Mkopoo utakufa mawazooo...!! Una hela yako huna nayo kazii fanya hivii
 
Na hii ndio hofu yetu watanzania wengi.
Huwa hatujiamini kwenye biashara,lakini sababu inatokana na lack of business knowledge.
Ndio maana wote tumekuwa na utamaduni wa kujenga tu au kuziacha hela benki kwenye saving account.
Ila wahindi huwa hawana hobby ya kujenga majumba wapatapo pesa Wana njia zingine za investment Kama kununua bonds/shares au other liquid assets Kama golds na kuzihifadhi ndani.
Siku akifirisika anauza kwa Bei ya juu na kuibuka tena.

Ni kweli kwa hilo wahindi wanapatia sana

Nilifanya kazi benki kati ya mwaka 2013 mpaka 2015 na nilikua na process applications za products fulani ambazo zililazimu kuona salary slips na savings za watu. Nilishangaa kuona wahindi wengi wana hela benki kati ya million 50 mpaka 100 na zaidi lakini kwenye makazi wameandia STAYING WITH PARENTS
 
Faida ni ndogo sana. Una imvest million 100 unapata faida 250,000 kwa mwezi daaah faida ndogo sana. Kwa million 100 zipo biashara nyingi zinazoweza kukupatia faidazaidi ya million 1 kwa mwezi
Huyu ni muongo Fixed mara nyingi ni 10p.a na kwenye faida unatoa 11pc
Hapo kwa mwaka atapata 10mil toa 11pc hivyo atakuwa na milioni 8 na point
 
Uko sahihi kabisa

Hata mimi naamini kujenga ni uoga wa maisha nani mawazo yakizamani. Business models are changing we also must change
Woga wa maisha isiwe hadi kwenye nyumba yako ya kuishi

Model zingine Issue muda
Real estate unajenga unaacha unaendelea na kazi zingine

Business model nyingine yawezakua si capital intensive ila labor intensive

Mind you hapa unazungumzia side business ya kuongeza kipato au kutunza pesa badala ya kuweka benki tu
 
Hii biashara watakuja kufaidi Vitukuu vyakoo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ndoto za alinacha kabisaa

Ukifuata Kanuni za kujenga nyumba za biashara, Unaweza ukafaidi vizuri kabisa matunda ya biashara yako, wewe mwenyewe NA watoto wako pia baada ya wewe kutoweka duniani. Kitu cha msingi ni kuzingatia misingi NA Kanuni za ujenzi wa nyumba, pamoja na kuchagua location nzuri.
 
Wahindi wengi wamepanga nyumba siyo kwamba hawana pesa za kujenga, LA hasha, pesa wanazo isipokuwa wanaogopa kujenga wakihofia wasije wakanyang'anywa tena nyumba zao kama walivyofanyiwa wakati wa Mwalimu Nyerere enzi za Azimio LA Arusha.. Wengi wanahifadhi pesa zao, hata kama mambo yakija kugeuka baadaye waweze kukimbilia zao nchini India. Kama ujuavyo, watawala wa Afrika hawatabiriki.
Achana na hao
Nenda kwenye makampuni makubwa ya kibiashara Vodacom airtel benk n.k
Wote hawa huishia kupanga tu na sio kujenga mzee
Ujenzi ni dead project Mzee
Leo tunalaumu mifuko ya hifadhi za jamii kwakuwa mapesa yote wamepeleka kwenye maujenzi
Mojawapo ya demand for the 'stimulus package' pale USA ilikuwa ni wadau kuchukua pesa yao na kuizamisha kwenye ujenzi
Pata hela fanya biashara huwezi tia kwenye fixed account au kanunue hisa huko
Huwezi hayo yote ni bora upige tu chipsi zege na mayai na kuku sio ujenzi mkuu
Ujenzi iachiwe serikali yenyewe kupitia NHC na wenzako na magharama yao yasiyohimirika
 
Hahahaha,kumbe umegundua mkuu.
Mimi nilikuwa na rafiki zangu wahindi tunafanya nao kazi ndio walinifungua akili.
Walikuwa wananiuliza umeinvest kiasi gani Hadi Sasa na akaunti yako Ina pesa kiasi gani?
Mimi nikawa nawajibu sina kitu hela zote nimenunua kiwanja na kuanza ujenzi,Kisha wananiuliza kwa mfano ukifukuzwa kazi ghafla utafanya nini?
Basi walikuwa wananicheka sana.

Jamaa wana akili sana. Wanayatazama maisha kwa upana na urefu sana. Hawana mawazo mgando
 
Back
Top Bottom