Ndachuwa,
Sio kweli kwamba kila wakati nyumba ina "appreciate" katika namna hii, kwamba thamani ya nyumba ina double au tuseme kuongezeka thamani kwa kiasi kikubwa!
Value ya nyumba au jengo inategemea mambo mengine mno na ni pamoja nyumba yenyewe, huduma za kijamii na miundo mbinu na kadhalika. Ukijenga nyumba la milioni 150 kwenye kiwanja chako Mlandizi haliwezi ku-appreciate sawa na nyumba ya namna hiyo hiyo iliyopo Sinza, hilo ni moja!
Pili kuna suala la soko, soko pia linashinikiza thamani ya vitu kama nyumba, ardhi. Wakati wa Kikwete kulikuwa na pesa nyingi mno mtaani na ilikuwa kawaida sana kuona ardhi, nyumba zikiuzwa kwa bei ya kufa mtu na pengine ardhi na nyumba hizo hazikuwa na thamani hizo...ndio kusema bei zilikuwa "inflated", sasa kwa sasa hali ni tofauti sana!
Ushauri wangu, tujielimishe zaidi kuhusu masuala ya "real estate"...nyumba, ardhi na itatusaidia. Kwa sasa sehemu nyingine duniani mambo yanabadilika, hata mtazamo wa watu kuhusu umiliki wa nyumba umebadilika.
Watu wengi wanachagua kuwa na nyumba ndogo lakini "functional" hivyo pengine kabla ya kujiingiza kwenye mkopo wa nyumba wa milioni 150 au 300 ni nzuri kufikiria je, unahitaji nyumba kubwa namna hiyo? Haiwezekani kujenga nyumba ya kadiri kwanza halafu kujenga hiyo "dream home" taratibu?
Mikopo ni bora tu kama inatusaidia kuingiza pesa zaidi au kuongeza ubora wa maisha yetu ila kama tunakopa halafu tunaumwa kichwa na kuwa stressed kila wakati nafikiri ni wakati wa kufikiria kidogo!