Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Ngwanakilala,
Jibu tokana na swali lako, ndiyo, ni busara...
Tatizo biashara ya nyumba marejesho yake hayataki haraka, ila yako steady na ni ya uhakika,...hayataki haraka kabisa, ila kama waweza fanya bashara nyingine iliyo na risk na rewards mapema fanya tu
 
Kajichanganya wapi?? Mbona kaongea vizuri tu...Amesema kwa sasa haiuziki kwa hizo bei kubwa.
'Leo nikiuza ni pesa ndefu sema fixed assets kwa sasa kuuzika kwa bei nzuri ni mtihani'.

Sasa hio pesa ndefu ataipatia wapi boss?
 
Upumbavu wamekupa,wao wanamajumba CANADA,hapa walijenga wao majumba yote ya msajili baada ya kutaigishwa wakaacha,we zubaa tu,soma majengo ya msajili yana majina ya kinanani.
Hujaelewa topic mkuu.
Kujenga sio dhambi ila unachoambiwa Ni kwamba jenga kwa pesa ya ziada.
Yaani usijitese na kumaliza pesa yote kwa ajili ya kujenga.
Kwa hiyo naamini hata hao wahindi wanajenga lakini kwa pesa ya ziada,yaani hawezi kuchukua pesa iliyo kwenye mzunguko wa biashara ili ajengee.
 
Katika taaluma ya Financial Management kuna Home accounting na Business Accounting. Watu wengi sana Duniani na hasa wa Dunia ya tatu hawatofautishi kati ya vitu hivi viwili.

Pia kuna uwekezaji wa kibiashara (business) na uwekezaji usio wa kibiashara (social).Kuwa na pesa bila ya kupata uelewa wa namna ya kuzitumia ni sawa na ugonjwa ambao Daktari wake ni mwanataaluma wa Financial Management. Ukizitumia bila kupata ushauri kwa mwanataalumu sahihi uatakuwa unajitibu mwenye na uwezekano mkubwa ni ugonjwa kutokupona na mwisho wake ni mauti.

Katika uwekezaji wowote ule ni lazima uangalie uwiano wa mali za kudumu (fixed assets) na mali za kawaida katika mzunguko (current) assets).

Pia ni lazima kujua Madeni ya kawaida ya kibiashara (current liabilities) na madeni ya muda mrefu (long term loans)
Kitaaluma na kwa kila biashara kwenye Balance sheet hii kuna uwiano (ratio) unaotakiwa kwa kila eneo(item).
Huwezi kujenga nyumba ya Tshs 150m ambayo ni mali ya kudumu (fixed asset) lakini ukawa una pesa mkononi au Bank Tshs 10m.

Kimsingi kama una nyumba ya Tshs 150m inatakiwa iwe asilimia 10 tu ya mali zako zilizoko kwenye mzunguko (current assets). Utakuwa mpumbavu au mwizi kama utajenga nyumba ya Tshs 150m ukawa una pesa chini ya Tshs 150m katika mzunguko.

Watanzania na watu wengine wa Dunia ya tatu ni self made business men au traders (wafanyabiashara ngumbaru walio jitengeneza wenyewe yaani wachuuzi) . Wafanyabiashara wa namna hii huwa wanaiga biashara za wenzao (copy and paste) na kawaida hawakui na mwisho hufilisika.
Falsafa inasema.

Tengeneza Biashara, ipe jina na lile jina liwe maarufu kuliko jina lako. Hata utakapokuwa umekufa ile biashara itakuwa inaishi.
 
Manofu,
Hamna kinachobadilila kwa kiasi kikubwa maana hata hiyo milioni kwa miaka hiyo ilikuwa pesa ndefu sana kama ambayo unaiona milioni 100 labda ya sasa... Kikubwa ni kuwa unakuwa umeweka hazina
 
Nyumba ya Mil 20 upangishe kwa Laki 2.5 kw mwezi labda kama imejengwa Posta au kkoo...!!
Hiyo ni nyumba ya 2 bed rooms na jiko dogo ambalo limeungana na sebule. Hata kimara, Boko, Bunju na Mbz ndiyo bei zilizopo. Posta pale ni maduka, ulizia bei ya frem ndogo ambayo unaijenga kwa 10m tu, ndipo uje hapa utueleza ni sh ngapi!
 
Hiyo ni nyumba ya 2 bed rooms na jiko dogo ambalo limeungana na sebule. Hata kimara, Boko, Bunju na Mbz ndiyo bei zilizopo. Posta pale ni maduka, ulizia bei ya frem ndogo ambayo unaijenga kwa 10m tu, ndipo uje hapa utueleza ni sh ngapi!
Sasa Fremu ni Nyumba?
 
Kwa mfano kwa dar es salaam, Pale maeneo ya mlimani city njia ya kwenda chuo pembeni kuna nyumba zipo pale ni za ovyo ovyo yani chumba,sebule,jiko na choo na ndani kubovubovu tu lakini kodi ni laki3
Location hapo ndo mchawi
 
Posta unapajua? Pana nyumba za kuishi za kupangisha pale?
Sasa kupata Kiwanja tu pale huweziii...Hata kikiwepo ni mamillion...!! Ukesema mil 20 useme unajenga kimara hukoo labda na hapo laki 2.5 ni nyumba yenye Tiles...madirisha ya aluminium..gypsum safii...Masterbed room[emoji23][emoji23][emoji23] Bado vingine kibaooo so sio simple mzeee
 
Ndachuwa,
Sio kweli kwamba kila wakati nyumba ina "appreciate" katika namna hii, kwamba thamani ya nyumba ina double au tuseme kuongezeka thamani kwa kiasi kikubwa!

Value ya nyumba au jengo inategemea mambo mengine mno na ni pamoja nyumba yenyewe, huduma za kijamii na miundo mbinu na kadhalika. Ukijenga nyumba la milioni 150 kwenye kiwanja chako Mlandizi haliwezi ku-appreciate sawa na nyumba ya namna hiyo hiyo iliyopo Sinza, hilo ni moja!

Pili kuna suala la soko, soko pia linashinikiza thamani ya vitu kama nyumba, ardhi. Wakati wa Kikwete kulikuwa na pesa nyingi mno mtaani na ilikuwa kawaida sana kuona ardhi, nyumba zikiuzwa kwa bei ya kufa mtu na pengine ardhi na nyumba hizo hazikuwa na thamani hizo...ndio kusema bei zilikuwa "inflated", sasa kwa sasa hali ni tofauti sana!

Ushauri wangu, tujielimishe zaidi kuhusu masuala ya "real estate"...nyumba, ardhi na itatusaidia. Kwa sasa sehemu nyingine duniani mambo yanabadilika, hata mtazamo wa watu kuhusu umiliki wa nyumba umebadilika.

Watu wengi wanachagua kuwa na nyumba ndogo lakini "functional" hivyo pengine kabla ya kujiingiza kwenye mkopo wa nyumba wa milioni 150 au 300 ni nzuri kufikiria je, unahitaji nyumba kubwa namna hiyo? Haiwezekani kujenga nyumba ya kadiri kwanza halafu kujenga hiyo "dream home" taratibu?

Mikopo ni bora tu kama inatusaidia kuingiza pesa zaidi au kuongeza ubora wa maisha yetu ila kama tunakopa halafu tunaumwa kichwa na kuwa stressed kila wakati nafikiri ni wakati wa kufikiria kidogo!
 
Back
Top Bottom