Je, ni halali kwa kisimbusi cha Azam kuiondoa TBC kwenye free local channels?

TBC kwenye Azam ilikuwa inaonesha vizuri. Ila kwenye Dstv ilikuwa inascratch yaani kama inafifishwa hivi. inaonekana kuna uhuni dstv wanafanya.
Wanataka wateja walipie kifurushi cha Compact yaani hadi siku ya ufunguzi wameshindwa kua na huruma wanawaza hela tu.... elfu 56 umeme wenyewe wa magumashi [emoji1787]
 
Mbona wapo Tbc ni Channel no 400 na siku zote wako kwenye Regional see Free
 
TBC kwenye Azam ilikuwa inaonesha vizuri. Ila kwenye Dstv ilikuwa inascratch yaani kama inafifishwa hivi. inaonekana kuna uhuni dstv wanafanya.
Yani niliweka mara moja tu nkakutana na kituko nikarudi channel ya dstv nyinginee
 
Azam TV hata wangesema wataonesha bure kombe la dunia nisingelipia... poor quality of content hafu wanajikuta miungu watu nimekuja likizo bongo na king'amuzi chao nimeking'oa uchafu nyumbani kwangu sitaki mimi..
 
Siyo kweli kwa maana Nape leo akiwa pale ofisi za TBC alisema kwamba wameiagiza TCRA wafuatilie ving'amuzi vilivyoiondoa TBC kipindi hiki

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Wanataka wateja walipie kifurushi cha Compact yaani hadi siku ya ufunguzi wameshindwa kua na huruma wanawaza hela tu.... elfu 56 umeme wenyewe wa magumashi [emoji1787]
Mbona mimi nina kifurushi cha 23,000 na nimeangalia leo kupitia Channel yao maalumu kwa World cup? Ana ni leo tu?
 
Nimechelewa kulipia dstv yangu, kesho mapema nitalipia.

Ila ilinibidi ni switch ili niweze kuangalia kupitia tbc ndio nikakutana na mtangazaji akiwa kwenye ubora wake [emoji119]
 
Mbona mimi nina kifurushi cha 23,000 na nimeangalia leo kupitia Channel yao maalumu kwa World cup? Ana ni leo tu?
Labda walisikia malalamiko ya wengi waliomba kwenye ufunguzi waangalie kupitia kifurushi hicho lakini pia sikilizia na leo kama wataonesha basi wamebadili gia angani lakini tangazo lao ni hilo
 
Kama hoja ni hiyo kwanini wamezuia tu kwa watu ambao hajalipua kingamuzi Cha AZAM, ila ambao wamelipia mechi zinaonekana
... kumbe sababu ndio hiyo? Azam wako sahihi! Watanzania tumezidi kupenda vya bure; kulipia 23,000 hatutaki tunataka tujiegemeze kwenye kisingizio cha local channels ni free!

Watu waambiwe ukweli; wajifunze kulipia huduma hakuna vya bure.
 
Nakubaliana na wewe 100% Azam hana maslahi yoyote ya kuiondoa TBC mimi nadhani labda TBC walitaka kitu lakini sioni sababu yoyote ya kibishara kusukuma Azam kufanya hivyo kwa sababu hawana haki za kurusha mashindano kwa hiyo hakuna mgongano wa maslahi.
 
TBC wanaonesha Ila Duh quality ni mbovu
Hakuna la kushangaza TBC hawajahi kuwa na quality ndio maana ni kama bure lakini ukitaka quality ni DSTV unalipa lakini unapata bidhaa katika ubora.
 
Labda walisikia malalamiko ya wengi waliomba kwenye ufunguzi waangalie kupitia kifurushi hicho lakini pia sikilizia na leo kama wataonesha basi wamebadili gia angani lakini tangazo lao ni hiloView attachment 2422727
Kumbe ni hivi, basi itakuwa hiki kifurushi kitaonyesha mechi kadhaa tu.
 
Mbona mimi nina kifurushi cha 23,000 na nimeangalia leo kupitia Channel yao maalumu kwa World cup? Ana ni leo tu?
Utaangalia ila sio mechi zote kuna nyingine hutoziona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…