Je, ni halali kwa kisimbusi cha Azam kuiondoa TBC kwenye free local channels?

Je, ni halali kwa kisimbusi cha Azam kuiondoa TBC kwenye free local channels?

Hivi uliangalia channel namba ngapi?
Sikumbuki mkuu, huwa sina tabia ya kukariri namba za channel, hata itv sijui ipo channel namba ngapi. Ila ni special kwa kombe la dunia.
 
Haina shida, hata hivyo mda wa kukaa home sio sana, mostly weekends au zile mechi za usiku.
Sio kila mechi ya usiku au mchana utaiona ,wana consider big matches zile, kama hizi za Qatar, Iran k utaziona.Ila zile za magiant hutoziona,haijalishi inanyeshwa mchana au usiku sababu kifurushi chako ni kidogo.
 
TBC ni waongo sana kudai kuwa wameshinda tenda kutangaza kombe la dunia.

Ikumbukwe national media zote wanapewa free to air hili kombe sasa Rioba anadangaya watu hapa kutaka kupiga hela, TAKUKURU ingilieni kati, TBC wanapata huduma kupitia kodi zetu sasa iweje wauze kuangalia kombe la dunia.
Huo ni mchezo wa azam tv baada ya kuona tbc inaonesha michuano na ukumbuke tbc ni free channel so haina azam hawatakuwa na maslahi yoyote, walichofanya ni kuifunga ili mlipie kwa za ile 23,000 yao ndo muone! Huo ni wizi wa Azam tv
 
Nitajie Channel iliyopata host kutoka Multichoice?

Fifa wana offer television za taifa kuonyesha mechi bure na ndio maana DSTV hajampiga pini TBC.

Ila channel za taifa zinazo onyesha WC ,ukitoa TBC zote Azam kaziblock sababu ni hao DSTV.
Mbona ukilipia unaziona!!!??
 
Mbona mimi nina kifurushi cha 23,000 na nimeangalia leo kupitia Channel yao maalumu kwa World cup? Ana ni leo tu?
Hutoweza kuona mechi zote.Ni kuanzia package ya Compact ndiyo utaona mechi zote 64
 
Labda walisikia malalamiko ya wengi waliomba kwenye ufunguzi waangalie kupitia kifurushi hicho lakini pia sikilizia na leo kama wataonesha basi wamebadili gia angani lakini tangazo lao ni hiloView attachment 2422727
Upo sahihi kabisa,hawajabadili ni kuanzia Compact ndiyo utaona mechi zote.Chini ya hapo utaona tu baadhi ya mechi
 
Sio kila mechi ya usiku au mchana utaiona ,wana consider big matches zile, kama hizi za Qatar, Iran k utaziona.Ila zile za magiant hutoziona,haijalishi inanyeshwa mchana au usiku sababu kifurushi chako ni kidogo.
Haina shida, TV yenyewe sio sana kwa kweli. Kuna wakati naweka bundle kwa sababu ya cartoon za watoto tu.
 
kwahiyo Azam lengo lao watulazimishe kuangalia ligi ya nyumbani! bas sawa.
 
TBC ni waongo sana kudai kuwa wameshinda tenda kutangaza kombe la dunia.

Ikumbukwe national media zote wanapewa free to air hili kombe sasa Rioba anadangaya watu hapa kutaka kupiga hela, TAKUKURU ingilieni kati, TBC wanapata huduma kupitia kodi zetu sasa iweje wauze kuangalia kombe la dunia.
Anadhani anongea na watanzania wa meals 1998, msamehe bure...
 
... kumbe sababu ndio hiyo? Azam wako sahihi! Watanzania tumezidi kupenda vya bure; kulipia 23,000 hatutaki tunataka tujiegemeze kwenye kisingizio cha local channels ni free!

Watu waambiwe ukweli; wajifunze kulipia huduma hakuna vya bure.
Watanzania twapenda vya bure bure

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Usijikite kwenye Azam TBC iko kwenye visimbuzi vingine pia. Kwenye nyuzi 72 mashariki TBC ni free kama ITV kwa king'amuzi cha HD, msiwe mateka wa Azam🤸🏋️⛹️🤾
 
Upo kazini mchana hakuna umeme, unarudi home jioni unakatika.
 
Back
Top Bottom