Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Mkuu,

Hupendi ninavyoandika.

Nakupeleka ignore list, kuanzia hapa sitaona posts zako.

Na wewe fanya hivyo ili usione ninavyoandika.

Utakuwa umemaliza tatizo la kuona maandishi usiyopenda kuyaona.
Sasa kiranga umempeleka ignore list kwa sababu hapendi unachoandika?!!
 
Sasa kiranga umempeleka ignore list kwa sababu hapendi unachoandika?!!
Sipendi achefukwe, nimemuasa na yeye anipeleke ignore list kwa sababu hapendi ninavyoelezea mambo.

Ndiyo uungwana.

Mimi sipendi kumchefua. Na tukijibizana nitamchefua zaidi.

Au unaonaje hapo?
 
Natafuta kitu ambacho hakina kasoro hapa duniani, kitu kikamilifu kwa 100% kitu ambacho huwezi kukuta mawaa ndani yake.

Nimeangalia kama dini, zote zinamapungufu ndani yake.

Kama ni elimu zote zina mapungufu ndani yake, zimekosa majibu mengi.

Kama ni sera za vyama, sera za vuama vyote vimejaa mapungufu

Kama ni kazi za sanaa, zote zina kasoro.
Demu wangu ana ulemavu wa miguu, nampenda hivyo hivyo alivyo, ni Mungu kanipa nami ninamshukuru
 
Je, mapungufu yana upungufu katika upungufu wake? Kwa sababu mapungufu hayajakamilika?

Hivyo, je, kwa kuwa hayajakamilika katika kukamilika, yamekamilika katika upungufu wake?

Au, hayajakamilika hata kwenye upungufu, kwa kuwa yangekamilika kwenye upungufu yasingekuwapo na yasingejulikana kuwa ni mapungufu?

Ukifikiria sana utaona, kitu ambacho hakina mapungufu hakipo. Kipo, lakini, kuwapo kwake kuna maana hakipo.

Kitu hicho ni nothingness, nothingness ni kutokuwepo chochote, hata vacuum in space si nothingness, kwa sababu ina space. Nothingness yenyewe hata space haina. Haina space, haipo kwenye time. Haipo. Inafikirika tu.

Hiyo nothingness haipo. Kwa kuwa kuwapo kwake ni kutokuwapo.Ikiweza kuwapo nje ya hapo tu, inakuwa si nothingness tena.

Hiyo dhana ya nothingness, kinadharia, ndiyo haina makosa. Kwa sababu ina lowet entropy, hauwezi kupunguza entropy hapo. Huwezi kuharibu, ili uharibu, inabidi uitoe kwenye nothingness.

Hiyo nothingness ndiyo haina mapungufu.

Kitabu cha kusoma ni "Why Does The World Exist: An Existential Detective Story" cha Jim Holt.
Greatthinker
 
Natafuta kitu ambacho hakina kasoro hapa duniani, kitu kikamilifu kwa 100% kitu ambacho huwezi kukuta mawaa ndani yake.

Nimeangalia kama dini, zote zinamapungufu ndani yake.

Kama ni elimu zote zina mapungufu ndani yake, zimekosa majibu mengi.

Kama ni sera za vyama, sera za vuama vyote vimejaa mapungufu

Kama ni kazi za sanaa, zote zina kasoro.
Mbona vingi. Maji, hewa safi, upendo wa kweli, utajiri halali, elimu halali, ukweli, kifo, haki, usawa na mengine mengi wakiwamo watoto wachanga
 
Mambo haya ni magumu sana, mwanadamu asiye mkamilifu hawezi kufanya Jambo likawa halina kasoro, sababu hata yeye asili yake ni kutokuwa mkamilifu
 
Back
Top Bottom