Je, ni kwanini Japan tunayoambiwa ina uchumi mkubwa na maendeleo inagandamiza abiria kwenye treni kama viazi ulaya?

Ndio, nchi tajiri halafu wanaishi katika ufukara wa kutisha., hata wabongo tu wenyewe, wale wa Mbagala kabisa waliozoea kuingia madirishani, hawawezi kuvumilia ufukara wa kutosha unoonekana hapo, tena tunaambiwa ni kawaida hiyo kwao...

Siyo tu kawaida. Ni mfumo wanauataka kutokana na ratiba za shughuli zao.

Kuna watu hata hapa Dar Wana magari na Bado wanataka watumie usafiri wa umma Kwa sababu zao binafsi.

Pia wapo wenye uwezo wa kujenga nyumba zao lakini wameendelea kupanga maeneo yaliyokaribu na shughuli zao.
 
Mimi nimeona tu nchi tajiri inashindilia rumbesa watu wake kwenye treni kama maharage ya Soya, nikashangaa kiwango hiki kikubwa cha ufukara kwa matajiri. Ni hicho tu.., nimeshangaa tu.., ufukara hauna limits kumbe..
Anhaa kumbe unashangaa train endelea kushangaa
 
Mfumo wa kuishi katika Ufukara wa kutisha, kwamba ndicho wanachotaka?

Kuna watu wanataka kuishi katika ufukara ili hali wana hali nzuri kiuchumi na wanaweza kuondokana na ufukara?


👆🏽Ukimwangalia huyo mwamba hapo, anapenda na ni uamuzi wake wa hiari kuishi katika ufukara na mateso makali namna hiyo, ilihali uchumi wake unamruhusu kujinasua katika hali hiyo ya Ufukara? Billgates anaweza kupanda katika treni ya namna hiyo kwa kupenda, if no, why?
 

Kwahiyo wewe unaona huyo hawezi kumiliki gari?
Ufukara unsupima Kwa kipimo Gani? Unaongelea mtu mmoja mmoja kwamba ltaifa fukara au watu fukara taifa Tajiri?
 
Endelea kushangaa kuna kitu utajifunza na kuachana na upumbavu
Mi nadhani tujikite kwenye hoja tu.., mambo ya upumbavu bila kuuonyesha kwa hoja ni kijoja. Kwamba kuna tajiri anaependa kuishi katika ufukara? Hoja ndio hiyo.., tujadili hoja tu
 
Kwahiyo wewe unaona huyo hawezi kumiliki gari?
Ufukara unsupima Kwa kipimo Gani? Unaongelea mtu mmoja mmoja kwamba ltaifa fukara au watu fukara taifa Tajiri?
Hiyo mimi sijui, mimi nazungumzia maisha ya kifukara katika usafiri wa treni kwa nchi tajiri yenye uwezo kiuchumi.
 
Huko far East wote wako hivyo. Hawanaga muda wa kupoteza
Duniani kote hakuna mwenye muda wa kupoteza, ila tunazungumzia tu Ufukara kwenye usafiri wa treni kwa nchi tajiri. Kwamba watu hawezi kuwahi kazini katika mazingira yasiyo ya ufukara wa kutisha? Au Norway na Sweden wao wana muda wa kupoteza? Au na wao huwa wanaminywa kama chachandu?
 
Kama haujui inakuaje unajua kwamba hayo ni maisha ya kifukara?

Nimejua kupitia video clips mbali za waJapan wakiminywa kama panya ndani ya tren. Au kuminywa kama mahindi ni utajiri?
 
Lakini wewe si ndio ulisema haujui?

Kwahiyo tukiwa level seat kwenye daladala au mwendokasi nchi yetu inakua Tajiri yenye uchumi wa juu?
Hayo mengine sijui. Ila Umeniuliza nimejuaje kuhusu ufukara? Nimekujibu ni kwa kupitia video clip za waJapan wakiminywa.

Hakuna aliyesema level seat ni kipimo cha utajiri. Bali hoja ni nchi tajiri kuwa na aina ya usafiri wenye ufukara wa kutisha.
 
Ufukara upi hapo hali unaona hilo treni la kisasa
 
Hayo mengine sijui. Ila Umeniuliza nimejuaje kuhusu ufukara? Nimekujibu ni kwa kupitia video clip za waJapan wakiminywa.

Hakuna aliyesema level seat ni kipimo cha utajiri. Bali hoja ni nchi tajiri kuwa na aina ya usafiri wenye ufukara wa kutisha.

According to you...
 
Nimewahi ishi Japan. Futa hilo neno ufukara . Ile ni inchi ya kipekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…