Je, ni kweli Allah amewaumba binadamu na majini ili wamuabudu?

Majini ni stori za Abunuwasi
 
Mungu hakuwahi kuumba majini, bali Maiaika ambao baada ya kuwa wameasi ndiyo wakaitwa majini
Itakua bibilia ndio inasema hivo

MWENYEZIMUNGU (s.w) hakuumba majini na wanadamu isipokua wapate kumuabudu

Ni ibilisi tu (laana ya MWENYEZIMUNGU iwe juu yake) ndie katika majini ambae aliishi na malaika na baadae akaasi

Malaika ni viumbe watakatifu ambao hawamuasi ALLAH na wala hawana matamanio kama walivo majini na wanadamu

Wapo majini wema na waovu

Na wapo wanadamu wema na waovu
Mungu hakuwahi kuumba majini, bali Maiaika ambao baada ya kuwa wameasi ndiyo wakaitwa majini
 
Viumbe wote vimeumbwa na allah mwingi wa rehema, ikiwemo watu , majini , miti na kadhalika na hakika lengo kubwa wote tunalijua ni kumuabudu yeye mungu mmoja ambae hana mshirika, hakuzaa wala hakuzaliwa
Viumbe wote, Nguruwe inclusive?
 
Mimi nikotofauti na hii fikra ambayo pia hapo zamani nlijua ivo kutokana na mapokeo ya kijamii ila kwa siku hizo najuaga Mungu aliumba binadamu ili akatawale dunia na vyote viujazavyo kwa lugha ingine ni kwamba Mungu alitaka kutawala dunia kwa kukaimisha madaraka kwa mwanadamu...nimewakilisha tu
Mungu kaumba Majini kawaleta duniani, wakaasi na kufanya Uovu, Katuma Malaika wakawa piga, then kaumba binadamu moja ya kiongozi, Wa Majini kaasi (ibilisi, Satan, lucifer etc) yeye na wenzake hawa amini kiumbe dhaifu kama Binadamu anaweza kuwa preferred juu yao, Majini wengine hawakuasi, Kwa Ajili hii sisi Binadamu tumeletwa Duniani kama Test tu kapewa na free will, unamfata Shetani ama mafundisho ya mungu, dunia sio makazi yetu Kutokana na Unachofanya Duniani utapelekwa kwenye makazi yako ya milele.
 
Kwahiyo majini wameumbwa na nani mkuu? Maana muumba ni mmoja tu au ndio miungu watatu?
Majini ni viumbe walioasi wakatupwa kwenye ulimwengu Wenye dhiki na wakaanza maisha ya kudanga.
Yesu alipokuja ndio akazidi kuwanyanganya Hata kile kidogo walichokua wamebaki nacho.

Ni Sawa na Wafungwa Gerezani ,wote ni wakosaji Japo kuna Wafungwa Wenye roho nzuri Kule gerezani. Lakini hawana sifa ya uadilifu.
Majini wapo wapole Lakini haiwafanyi kuwa watakatifu. Hawajakubalika Kwa sababu walimuunga mkono Shetani.

Watu wanamfikiria Mungu kama MTU Wa Dini vile .
Mungu ni mtawala Wa Vitu vyote na anachotaka ni utii tuu. Kuabudu ni kunyenyekea mbele yake Kwa Kila kitu.
Shetani alipoasi alikosa utii na wapo viumbe waliomtii na kumfuata Shetani na wapo waliokataa kumtii Shetani na kuendelea kumtii Mwenyezi Mungu . Ikumbukwe kuwa Shetani alikua ni Kati ya viumbe Wa juu sana kule mbinguni na alikua na kundi kubwa sana chini yake.
Lakini pia palikua na viumbe waliobaki neutral bila kumtii Shetani Wala Mungu . Hao viumbe walisubiri upande utakaoshinda ndio watakaojiunga nao. Hawa walikua kama chawa Wa kisiasa. Baada ya Shetani kushindwa Kwa kichapo kikali Toka Kwa Malaika mkuu Wa Vita Mikaeli alitupwa Duniani kwenye dhiki kuu pamoja na wale wote waliomuunga mkono na wale waliokuwa neutral .

Kwa hiyo Majini wapole wapo ila hawana nafasi Tena mbele za MUNGU mana walikosa utii. Kukosa utii mbele ya Mfalme Wa wafalme ni uasi.
Hivyo majini yawe yanaswali au yanaimba yote yaliasi .
Mungu ni mtakatifu sana .
Hata binadamu baada ya kuasi na kutupwa nje ya Edeni na kuungana na Shetani , anapata tu rehema ya kuingia Peponi kupitia mwaliko Wa Masihi Yesu Kristo kubeba makosa Yao na kuwafanya wawe watu wake yaani amewakomboa Kwa gharama ya kujitoa kuja Duniani kupambana kiumbe hatari na mwenye maarifa Mengi Lusifer au Shetani . Bila ukombozi hakuna binadamu atakayeingia Peponi Kwa matendo yake zaidí ya gharama ya utii wa Kristo Yesu.
 
Mungu kaumba Majini kawaleta duniani, wakaasi na kufanya Uovu, Katuma Malaika wakawa piga, then kaumba binadamu moja ya kiongozi, Wa Majini kaasi (ibilisi, Satan, lucifer etc) yeye na wenzake hawa amini kiumbe dhaifu kama Binadamu anaweza kuwa preferred juu yao, Majini wengine hawakuasi, Kwa Ajili hii sisi Binadamu tumeletwa Duniani kama Test tu kapewa na free will, unamfata Shetani ama mafundisho ya mungu, dunia sio makazi yetu Kutokana na Unachofanya Duniani utapelekwa kwenye makazi yako ya milele.
Hizi ni hadith za Qur'an tu na ndiyo maana kila Muislam analilia kufuga majini ili awe anawatuma kuiba kwa kupitia chuma ulete.
 
Hiyo Ni Quran Yako Hakuna Aya Inasema Hivo Au Hujui Kufafanua Unachosoma.Ni Aya Ya Ngap Hyo
Kwanini Mungu akuumbe halafu eti akuone unateseka kwa kuinama na kuinuka mara 5 kwa siku, ili umuabudu, kwani usipomuabudu atapungukiwa nini?
 
Kuna watu wanashangaa kusikia majini yameumbwa ili kuabudu.!!! Mtu akisikia neno jini akili yake anaipeleka katika mawazo TOFAUTI kabisa ! Kweli wazungu wamewashika watu pabaya na propaganda zao !
Wazungu wameingiaje hapa tena? Jini ni PEPO... Malaika wa Shetani... Ila ndio hivyo tena, Dini ya Alah ina ushirika nao na ni waumini wenzenu.
 
Kuna Majini Mabaya Na Mazur Kama Quran Inavosema.Kama Tulivyo Wanadamu Kuna Wabaya Na Wazur,
Hakuna Jini baya na zuri... hakuna Pepo baya na zuri, hakuna shetani mbaya na mzuri.

Mudi hapa aliwapeleka chaka vibaya sana.
 
Mbona muongo ?weka andiko linalosema majini yamelaaniwa .

Mbona hakuna ushahidi kuwa majini yalikuwa yanaishi huko uongo wako unakusaidia nini ?
Majini hayajalaaniwa... majini ni ndugu zetu waislam na tunaswali nao msikitini kumuabudu Allah.

Daaah... Mtu anatetea Jini... hii dini inafurahishaga sana sometimes.
 
Ni ajabu ikiwa utamtafsiri jini kutokana na upeo wako au mafundisho ya dini yako.

Ushaambiwa dini ni viumbe kama ilivyokuwa binadamu kuna ,wema ,waovu,washirikina ,wapagani nk na wana ulimwengu wa tofauti kabisa .

Ingekuwa ajabu kama ingekuwa tumearishwa tuwaabudu au tuwatumikie.
 
Kwanini Mungu akuumbe halafu eti akuone unateseka kwa kuinama na kuinuka mara 5 kwa siku, ili umuabudu, kwani usipomuabudu atapungukiwa nini?
Mungu hakutegemei wewe bali wewe ndio unamtegemea yeye, hatumuabudu sababu yeye anatuhitaji sisi bali tunamuabudu sababu sisi tunamhitaji yeye.
 
wanafuga majini kweli,,kasome "suratul jinn" ALLAH anawaambia waislam,hakika ninyi nyote mtaenda motoni kwani mnawaweka majini kati yangu na ninyi,,na majini yanalalamika kwa kusema kwamba,,,,tunashirikiana na wanadamu ktik kutafuta risk!!!
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

1. Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!

2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.

3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.

4. Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.

5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu.

6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.

7. Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.

8. Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.

9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!

10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu.

11. Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.

12. Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.

13. Nasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.

14. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.

15. Na ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.

16. Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi,

17. Ili tuwajaribu kwa hayo. Na anaye puuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.

18. Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.

19. Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu alipo simama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga!

20. Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote.

21. Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.

22. Sema: Hakika hapana yeyote awezae kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipo kuwa kwake Yeye tu.

23. Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.

24. Hata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.

25. Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu.

26. Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,

27. Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.

28. Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote walio nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.
 
Ipe
Mkuu jini anaweza kuwa ndugu yangu katika Imani?
Kwani kuna undugu usio na Imani?
Hivi ili umkubali ndugu si ni lazima uamini kuwa ni ndugu yako?

Nipe mfano wa ndugu usiye mwamini kuwa ni ndugu yako.
 
Kwani majini ambao hawakudhuru wala kumkufuru Mwenyezi Mungu wana ubaya gani kujenga nao urafiki?
Sasa mbona mnakataa kuwa ni marafiki zenu?
Mtume wenu kasema muitane Kaka, wewe una kauli gani ya tofauti.

Wewe ni nani kwanza wa kumpinga Mtume wa Allah

"Kujenga nao urafiki" huwa wenzetu mnakutana nao wapi mnakojenga nao urafiki?
 
Back
Top Bottom