Je, ni kweli bangi inaweza kukinga dhidi ya wachawi?

Je, ni kweli bangi inaweza kukinga dhidi ya wachawi?

Mimi bange sivuti ila napenda harufu ya majani yake ule mmea umebarikiwa sana ni vile tu watu wenye fitna wanausema vibaya, ukweli ni kuwa bangi huwa inachochea sana katika kukamilisha nia uliyo nayo moyoni, moyo wako ukiwa na tamaa wivu na chuki bange inaenda kuchochea ile nguvu iliyo ndan yako ndo hapo unaenda kufanya mambo ya kipuuzi siku zote bange ni mbaya kwa watu wenye nia mbaya.

Lakin bange ukivuta kwa malengo ya kupambania maisha yako inaenda kuchochea na kuleta morali katika kile kilicho ndani yako kama ni kufanya ibada hakuna kipindi cha sala kitakacho kupita kama ni mtu mwema bas hata mambo ya kinafki na uchonganishi hautayataka kuyaskia kabisa Wana wanaweza kuleta stori za uchonganishi, ila we ukawa zako cool tu hata kuchangia mada huchangii kwakua tayar ilishakuchoche katika kile kilicho ndani yako ambacho ni amani.

Marasta wengi wale wa kweli ambao hawali nyama huwa hawawezi kushuhudia hata kuku akichinjwa huwa wanaumia sana moyoni kwakua Imani yake ni amani na upendo Sasa bange inaenda kuchochea kile kilicho moyon na hata utendaji wake unakua ni sahihi zaidi kwa 90% zaid ya yule ambae hatumii mmea.

Umeeleweka vyema sana ndugu
 
Habari zenu ndugu zangu wa Jf ni imani yangu kwamba nyote mko salama na niwape pole kwa mihangaiko ya wiki nzima hakika kazi inaendelea.

Sasa ndugu zangu mojakwamoja twende kwenye mada yetu kama kichwa cha habari kinavyoeleza.

Kumekuwa na stori stori nyingi mtaani kila mtu akisema lake kuhusiana na kilevi aina ya BANGI lakini katika vyote nilivyowahi kuvisikia kuhusiana na kilevi hiko mpaka kupelekea kuandika uzi huu ni kwamba.

Siku moja nilikaa kijiweni na washkaji kadhaa sasa mmojawapo alikua akivuta BANGI kwa wakati ule ilikuwa kama mida ya saa moja moja hivi jioni sasa ghafla tukaanza sikia sauti ya paka mita kadhaa akilia sana yaani alianza kulia dakika kadhaa baada ya jamaa yule kulipua kitu cha Arusha sasa alikuwa akipiga sana kelele ikabidi tuache stori zetu tuulizane kwani vipi maana hata tulipojaribu kumfukuza ni anakimbia mita kadhaa kisha anarudi anajificha sehemu fulani ambayo ni gizani anajua ni ngumu kumuona na anaanza kulia kama kawaida.

Sasa buana yule jamaa aliekuwa akivuta akatuambia kwamba huyu ni mchawi hataki tuvute bangi inamsumbua alituambia kwamba nyumba ya jirani kuna bibi mmoja wanamshukia sana kuhusu masuala ya ushirikina inawezekana kamaindi.

Nikajaribu kumuuliza kwamba kwani BHANGI ina uhusiano gani na masuala ya uchawi jamaa akaniambia “ebhanaee hii kitu iheshimu kwasababu ina nguvu kubwa sana katika mambo mengi hii kitu ukiwa unavuta mchawi hakusogelei hata kidogo yaani anapita mbali kabisa”.

Sasa ilinibidi niangue kicheko lakini moyoni nikajisemea yaani nitafanyia uchunguzi kama ni kweli nami nianze tu kutumia hii kitu maana nimezungukwa na wanga kwasana na mimi sio mtu wa dini sana wala mganga simjui anafananaje kwahivyo siku nikigundua kuna ukweli aisee itanibidi niitumie kama kinga yangu.

Sasa ndugu zangu najua wakongwe wapo humu naombeni kufahamu je ni kweli BHANGI inaweza kukukinga dhidi ya wachawi?

Na kama kuna anaefahamu nguvu ingine ya BHANGI si mbaya akatujuza hapa.

Nawasilisha
Ukiwa maskini unaandamwa na maruerue ya ajabu ajabu kama hayo
 
Hahaha hivi ni kweli sasa mbona nasikiaga yule raisi wa Kenya Mhe .Kenyatta anakulaga wida
Ukiwa na pesa bangi haiwezi kukudhuru. We jaribu kuvuta bangi hujatia kitu tumboni na huna kitu mfukoni Wala deal yoyote inayokaribia ku mature.
Hapo bangi itakutuma ukabake, ukaibe simu, umtukane mzazi nk
 
Ni kweli lakini sasa muda mwingine inagegemea na anaekupa hizo kudu unajua ndugu kuna vijiwe kadhaa nimewahi kufika unafika unakuta hakuna rika lako hata salamu unajistukia inabidi useme As. Aleikum kwaio hao huwa wanaongea vitu makini sana muda mwingine kwakuwa wameanza muda mrefu na wamepitia mengi
Hakuna cha vijiwe au aina ya watu kwenye vijiwe. Plain fact ni kwamba bange kama bange haiwezi kuzuia uchawi.

Ukibisha zaidi nenda kwenye hicho kijiwe uwaulize hao wandewa uchawi ni nini na uchawi unafanya vipi kazi.. Ukipata majibu ya kueleweka ya hayo maswali ndio utaelewa vizuri.

Halafu punguzaa.. Ikiwezekana acha kabisa.
 
Nadhani zaidi ya 50% ya maisha ya watanzania ni fix tupu.
Tunaishi uongo tulioambiwa tukiwa wadogo, fiction za imani na fixi za mitandaoni!
 
Kama ni kweli nitatafuta majani ya bangi nitwange ili maji yake ninyunyuzie nyumba yangu kila ninapolala.
 
Nadhani zaidi ya 50% ya maisha ya watanzania ni fix tupu.
Tunaishi uongo tulioambiwa tukiwa wadogo, fiction za imani na fixi za mitandaoni!

Mmmm [emoji848] kwaio kumbe itakuwa ni fix tu
 
Yaani iko hivyo na ukiwa unafanya kitu muda mwingine ukakosea katika hali ya ubinaadamu tu kama kuna mtu karibu yako anaefahamu kama unatumia hio kitu basi atakwambia tu “acha bange”
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji3] kabisa iko hivyo!
 
Huo ndio ukweli, Kwenye bangi sio mchawi tu,, hata majini ni hayasogei.

Dunia ndio iko hivo, nakumbuka kuna mtaalamu alikua akielezea kuna mti fulani wa kawaida tu, kuwa endapo mtu aliyechukuliwa msukule akiuchukua na kuushika basi kumbukumbu zake zinaweza kurudi na kumsaidia kutoroka huko anapo tumikishwa.
Mti wa mbaazi,
 
Sio bange pekee ipo pia mimea na madini pia hawa wapumbavu awakugusi.Nguvu ya uchawi ipo kwenye dawa so KILA dawa ijayo miiko yake Ili itende kazi,ukimeza dawa ukanywa maziwa au pombe dawa haiwezi fanya Kazi.So ukizijua Siri na codes za zao hawawezi kukusumbua.Sababu KILA kitu duniani ni hesabu na kanuni na KILA kanuni Ina ant yaani against.
So wengi wanadhurika na uchawi sababu ukosefu wa maarifa ya kutozijua codes na ethics za kichawi zinafanyaje Kazi.Zipo hata kanuni za kulala wakija usiku hawawezi kukubeba.Mwanadamu anaogopa mvua so majini nayo kuna vitu wanaogopa,hawa wapumbavu sio kwamba wao ni miamba Sana au wananguvu Sana kushinda binadamu sema tu wengi hawana maarifa na kuijua nguvu yao waliopewa na Mungu
 
Back
Top Bottom