Wakuu naomba kuuliza, anachokisema huyu mama kwamba hata kama bikra ya mwanamke ilitolewa muda mrefu? Anasema hata kama mwanamke amezaa watoto sita bikra yake inaweza kurudi bado.
Hii ni kweli au anatupoteza huyu?
Hii ni kweli au anatupoteza huyu?
- Tunachokijua
- Bikira (hymen) ni utando mwembamba wa tishu unaopatikana kwenye mlango wa uke. Utando huu huumbika wakati mtoto akiwa tumboni mwa mama. Ukubwa, umbo na unene wake hutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine, na unaweza kubadilika kadiri muda unavyopita.
Utando wa bikira mara nyingi huhusishwa na historia ya mtu kufanya tendo la ndoa, kana kwamba ni kifuniko kigumu kinachozuia kuingia kwenye uke jambo ambalo sahihi. Wataalamu wanaeleza kuwa bikra inaweza kuondoka bila hata ya mtu kufanya mapenzi.
Utando huo wa tishu (bikra) Unaweza kutanuka au kuchanika kutokana na shughuli za kawaida za kila siku, matumizi ya vifaa vya vinavyowekwa ukeni kwa ajili ya hedhi au kufanya tendo la ndoa. Mambo mengine ni kwenda gym, kuendesha baiskeli, kujichua
Je bikra inaweza kurudishwa baada ya kutoka?
Vyanzo na wataalamu vinaeleza kuwa unapopoteza bikra yako hakuna namna utaweza kuirudisha tena.