Je, ni kweli Bongo maisha yamekuwa magumu kwa sasa? Nimepigwa mzinga na wahitimu watatu ndani ya siku moja. Kiwango wanachoomba ndiyo kimenishangaza!

Pamoja sana kaka. Tusisahau biashara ndogo ndogo. Zinaokoa sana kwenye nyakati ngumu
Kweli mkuu unakuta kuna muda mambo yapo tait biashara kubwa haiuzi ile ndogo ndo inauza ndiyo inayokubeba
 
Biashara ndogo sawa, ongeza na biashara isiyotegemea umeme wa TANESCO, Pia biashara isiyovutia TRA
 
Maisha ya mjini ni magumu sana, kwa sababu kuishi kwako kunategemea uwezo wako wa kununua vitu na huduma; wengi mjini hawalimi labda kutokana na mazingira, iwe pilipili, mchicha, yai n.k wananunua.

Kama unaona mbali na hutaki msongo wa mawazo, kawekeze mkoani na huko mjini pawe sehemu ya soko tu.
 
Sasa usiombe upigike huku una mwanamke unampenda upo nae kwny mahusiano funzo utalopata hapo hutakuja usahau kmmk...

Utaona demu anakukwepa waziwazi yan inaongeza machungu mara mbili

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
 
Umesahau kitu mkuu. Wakumbushe vijana wasiwasahau wazee wao, haya mengine ni laana na mikosi ya kukana asili na tamaduni zao.
Ni kama umenisema Mimi...


Nina bifu na dingi naye amekausha najiona naadhibika.
 
Kama unao uwezo saidia sio kuwasimanga humu mkuu,shida haina mwenyew
 
nikopeshe buku 5 hapo nijazie kodi mkuu, kesho jion nitakirudishia kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…