paul sylvester
JF-Expert Member
- Mar 18, 2020
- 3,503
- 3,499
Anzisha hiyo hoja wewe, tutakuja kukujibu, hii ni hoja inayojibu zile propaganda za mgombea Fulani hivi anayekataa Hansard za Bunge Kwa maksudi zilizoidhinisha manunuzi ya ndege.Umeona wapi shirika linafanya biashara lakini ukaguzi hakuna.
Mkuu, ukimsikiliza mgombea anasema hakuna mbunge hata mmoja anayejua hata fedha zilizotengwa kununua hizo ndege. Hiyo ndiyo ilikuwa hoja yake kwenye clip hiyo kama umeisikiliza. Halafu baadaye anaonekana Mheshimiwa Halima Mdee akiijadili hoja hiyo akiwa Bungeni. Msinishambulie mimi kwakuwa mimi sio niliyesema hivyo na bahati nzuri nimeweka video yake. Mimi sigombei hata udiwani.
Mkuu hii ni hoja yako ambayo ni nzuri kabisa. Lakini haikuwa hoja ya siku ya mgombea wetu. Ungeisikiliza kwanza hiyo video clip.Hii ndiyo hoja....
Hoja siyo kupitishwa ama kutopitishwa kwa fedha za ujenzi wa CHATO INTERNATIONAL AIRPORT...
Kuna watu wamejaliwa kusema uongo, huyu mgombea anasema uongo bila hata kupepesa macho yaani akiwa rais tutadanganywa hadi tukome.
Polepole anasema tena kwa kimombo kuwa amepoteza kumbukumbu.Mkuu, hoja ya Mgombea ni kwamba bunge halikuhusishwa kabisa, na ndivyo anavyotueleza wapiga kura wake.
Kawadanganye wanachadema wenzako uliona wapi mchakato wa manunuzi unapelekwa bungeni? Bunge huwa linapitisha bajeti tu siyo manunuzi. Wakati mwingine mkubali tu kuwa mgombea wenu anachemka sana asifikiri watz ni wajinga kiasi hicho.Kilichopelekwa bungeni ni bajeti ya manunuzi ambapo kama kawaida ya wabunge wa CCM ni ndiyoooo. Kilichotakiwa kupelekwa ni hoja ya kuzinunua na ijadiliwe shirika litaendeshwa vipi. Hata hayo ya reli ni bajeti tu zinapelekwa bungeni ila siyo hoja! Watu walitaka hoja ijadiliwe. Huwezi kujenga reli ya trilioni 6 aa kitanzania halafu uamue peke yako...
Devices alizowekewa na mabeberu ya Kibelgiji inampa shida!Polepole anasema tena kwa kimombo kuwa amepoteza kumbukumbu.
Maswali hayo ya bunge kutohusishwa yaliulizwa wakati was uhai wa bunge, iweje majibu yasipatikane wakati huohuo yaje yatolewe sasa?Mkuu, hoja ya Mgombea ni kwamba bunge halikuhusishwa kabisa, na ndivyo anavyotueleza wapiga kura wake.
Mkuu, hoja ya Mgombea ni kwamba bunge halikuhusishwa kabisa, na ndivyo anavyotueleza wapiga kura wake.
Wabelgigi washenzi sana walimtesa Patrick Lumumba wakamgoa meno bila ganzi,harafu wakamtosa kwenye tindikali ya Sulphuric Acid akayeyuka kabisa.Devices alizowekewa na mabeberu ya Kibelgiji inampa shida!
Bora corona kuliko ccm.Wabelgigi washenzi sana walimtesa Patrick Lumumba wakamgoa meno bila ganzi,harafu wakamtosa kwenye tindikali ya Sulphuric Acid akayeyuka kabisa.
Juzi binti yake ameomba serikali ya Belgium irudishe jino lake.Ukisikia wazungu washenzi ni hao.
Kwanza mnaongelea bunge gani? Hili bunge la Ndugai?Mbunge litakuwa limehusishwa endapo tu report ya ukaguzi itarudishwa bungeni.
Je report ya manununuzi ya ndege za ATCL imewahi kufanywa na CAG na kupelekwa bungeni??
Mkuu, hoja imeletwa sasa na mgombea akiwa kwenye kampeni za kuwania urais. Wakati bunge likiendelea hakukuwa na kampeni wala mgombea urais. Nadhani tukae sawa kwanza hapo.Maswali hayo ya bunge kutohusishwa yaliulizwa wakati was uhai wa bunge, iweje majibu yasipatikane wakati huohuo yaje yatolewe sasa?
Serikali ya awamu ya tano imejikita zaidi katika uongo na ulaghai ila bahati mbaya ni wa kishamba zaidi ambao kila mwenye akili hawezi kudanganyika.
bunge hewa kabisa hiliKwanza mnaongelea bunge gani? Hili bunge la Ndugai?
Pole inaonekana ni mara yako ya kwanza kupanda ndege. Kwanza kuhusu huduma ya chakula imesimamishwa kutokana na Corona pia naomba nikujulishe kuwa ndege ikiweza kupakia 1/3 ya uwezo wake tayari hakuna loss hapo.Mimi nitoe ushauri wangu ambao hauegemei upande wowote. Juzi nimepanda Bombadier kutoka Dar mpaka Mwanza. Ujazo wa ndege hii ni abiria 72 lakini tuliopanda ndege ile ni kama abiria 30 tu ambayo kwa biashara ni hasara kubwa na hii inatokana na wananchi wengi hali zao za kiuchumi siyo nzuri...