Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Bunge halikuhusishwa kwenye ununuzi wa ndege za ATCL?

Wakikujibu mi najinyea mkuu
 
Hili ndiyo lengo kuu,tusikute Kuna upigaji.Tuonyeshwe risiti ya manunuzi na mikataba.
 
Hizo zinazozungumza na halima bado hazijanunuliwa au hazijaja. Lissu anazungumzia zile za mwanzo zilizonunuliwa kinyemela na mtu na mpwa wake
 
Lissu hajasema kuwa hakuna mbunge hata mmoja anayejua fedha zilizotengwa kwa ajili yakununua ndege hizo. Alichosema ni hakuna ( si mbunge au mwananchi) anayejua bei ya ndege na hakuna aliyeona mkataba wa manunuzi. Hakusema kuwa suala la ununuzi wa ndege halijawahi kujadiliwa Bungeni. Anachohoji ni mchakato wa kununua ndege baada ya Bunge kupitisha maombi ya serikali kupitia Bunge. Halima Mdee anahoji maombi ya serikali ya kupewa kibali ili cha Bunge ili watengewe Shilingi bilioni 495 wakati mwaka uliopita walitengewa bilioni takribani 500. Ni dhahiri kuwa yeye kamambunge hajawahi kupata mrejesho wa matumizi wa pesa zilizoombwa. Mrejesho unakuwa ni Mkataba wa manunuzi unaoonyesha bei na masharti ya manunuzi. Wote wawili wanaongelea kitu kimoja. Kuna tofauti kubwa kati ya kutenga pesa na matumizi yake. Bajeti inaonyesha makisio ya matumizi wakati mikataba ya manunuzi inaonyesha kiasi kinachotakiwa kukamilisha manunuzi.

Amandla...
 
Chadema wapuuuzi tangu wa juu mpaka wa chini, Kwa nini hawakumkumbusha mgombea kuhusu Hilo, ukizingatia pengine Kwa yaliyompataga yameweza kupunguza vitu Fulani mkichwa,

Chadema jitokezeni mpangue hiyo hoja ya Polepole
 
Ya Chato nimeongeza kwa kuwa ni kaa la moto hawataki kujibu.

Ila nilichoandika mwanzo ni kuwa wanamilead kuwachanganya watu. Lisu hakusema kuswa bajeti haikuinclude Manunuzi ya ndege. Alichosema ni kuwa hakuna mtu anayejua Bei za ndege wala mikataba yake ... Which makes a lot of sense. Inawezekana tunaambiwa tumenunua Cash kumbe bado kuna deni tunadaiwa. Ila hakuna proof yeyote kwamba tumelipa kiasi gani ....!!
 
Mkuu, hoja ya Mgombea ni kwamba bunge halikuhusishwa kabisa, na ndivyo anavyotueleza wapiga kura wake.
Basi ndiyo imekula kwenu. Sisi wananchi hatujui bei ya kila ndege. Hapo kuna ufisadi. .. wananchi tunamuelewa Sana Lisu kuliko huyu John mtaka fujo.
 
Hilo ni swali lako wewe!

Mada inahusu alichoongea Lisu na kilizungumzwa na Mdee bungeni!
 
Mkuu, hoja ya Mgombea ni kwamba bunge halikuhusishwa kabisa, na ndivyo anavyotueleza wapiga kura wake.
Hapo ni taarifa tu ya jumla. Bunge linapohusishwa, ni kupitia hatua mbili muhimu sana:

1) Kwanza ni kupitia kamati ndogo ambapo nyaraka zote hupitiwa na kuhakikiwa. Je, taratibu za manunuzi zimefuatwa? N.k. baadavya hapo kamati ndogo hutoa taarifa bungeni na kuchambua kila kitu. Kisha bunge hujadili na kutoa baraka, maonyo, tahadhari, au hata kuagiza serikali ichukue hatua, au kupendekeza kuundwa kamati maalum ya bunge kufukua zaidi uozo kama upo.

2)Kupitia ofisi ya C.A.G. ambayo hufanya ukaguzi wamanunuzi na matumizi yote ya serikali, isipokuwa idara chache mahsusi, ikiwemo ofisi ya Rais, na taarifa yake huwasilishwa bungeni, ikiwa na mchanganuo kamili, na kujadiliwa. Hapo nyaraka hizo zote huwa wazi kwa umma na mtanzania yoyote anaweza kuziona na kutoa maoni yake.

Ishu ya ununuzi wa ndege haijadiliwi katika ngazi ya kamati ndogo, na wala haikaguliwi na C.A.G. kwa sababu imehamishiwa ofisi ya Rais. Kwa hiyo ukiacha taarifa fupi sana inayoongekewa hapa, Bunge halina ruhusa ya kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia serikali, katika ishuvya ununuzi wa ndege
 
Polepole anasema tena kwa kimombo kuwa amepoteza kumbukumbu.
Aliye poteza kumbukumbu ni PLPL alisema mwenyewe CCM kukukiwa na tume huru haiwezi kushinda na mwaka huu mnapigwa kwa uzembe wenu 'he can't think outside the box '
 
Kawadanganye wanachadema wenzako uliona wapi mchakato wa manunuzi unapelekwa bungeni? Bunge huwa linapitisha bajeti tu siyo manunuzi. Wakati mwingine mkubali tu kuwa mgombea wenu anachemka sana asifikiri watz ni wajinga kiasi hicho.
Bunge husimamia kila kitu kupitia kamati ndogo, Oversight Committees, ambazo kwa utaratibu wa jumuiya ya madola, ambapi sisi ni wanachama, kamati hizi husimamiwa na wabunge kutoka kambi rasmi ya upinzani, ili kuweka utawalabora.

Pia bunge hudhibiti kupia C.AG. sasa hizi njia mbili zote bunge limefungwa mikono na kuzibwa mdomo. Ununuzi wa ndege umehamishiwa ofisi ya Rais, ambayo haikaguliwi na C.A.G.

Ukipenda, hiki ni kichaka cha kuficha maovu. Usiri wa nini?
 
Mkuu, sikiliza tena hoja ya mgombea wetu kabla ya kufika mbali huko kwa CAG.
Utamwachaje C.A.G. ambaye hutumwa kufanya kazi ya Bunge? Wakati wanagombana na Prof. Assad, Ndugai alieleza hili vizuri sana. Kwamba C.A.G. ni mtumishi wa Bunge. Bunge haliwezi kwenda kufanyavhayo yote, linamtumia C.A.G.

Pia kumbuka kwamba Magufuli ana kawaida ya kunyofoa pesa toka sehemu moja kwenda ingine. Mfano Tume ya uchaguzi mwaka juzi ilitumia fedha mara sita zaidi ya zilizotengwa. Pia wizara ya ujenzi. Sasa kama hakuna mrejesho, hakuna usimamizi, tutajuaje ni pesa ngapi hasa imetumika? Na je, taratibu zote zimefuatwa?
 
Na huu ndio mwisho wake
 
Mpumbavu ni wewe!Una uhakika gani hizo fedha zilizotengwa zote zitatumika kununua ndege ili hali bei halisi iko katika mikataba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…