Je! ni kweli dunia inazunguka jua?

Je! ni kweli dunia inazunguka jua?

limetumbuka,

Mfano nipo juu ya gari then nikaruka juu basi gari litaniacha na mimi nitadondoka chini, iweje ndege imeruka ipo juu uniambie ipo duniani bado?

halafu na satelite (man made sio sayari) si zipo juu ya dunia why hatuzigongi?

satelite.jpg

Mtu akiwa juu ya gari then akaruka ni dhahiri kwamba gari litamuacha,ila je ushafikiria mtu ambaye yuko ndani ya bus ambalo liko wazi juu (let say mtoto) then akaruka kwa kutumia nguvu kidogo,je bus litamuacha au ataangakia ndan ya hilohilo bus??.

Basi hata kwa dunia ipo hivyo,ili kitu chochote ili kitoke nje ya dunia lazima kiwe projected kwa velocity kubwa (called escape velocity=11.2km/s ).

Pia mkuu ndege na helicopter haziwezi kuachwa na dunia kwasababu zinakuwa bado zipo ndani ya mipaka ya dunia,zinakuwa bado zipo chini ya gravitation force ya dunia inayozifanya ziendelee kuwepo

tumesoma kwenye jografia kua dunia inazunguka jua hivyo tunapata majira ya mwaka kama kiangazi na masika je ni kweli? galileo alikuwa sahihi?

Fikra ya kawaida
chukulia umepanda ndege au hellcopter halafu unaenda marekani then ile hellcopter ikasimama juu angani kwa muda mrefu lets say mwezi mmoja, je dunia itakuacha? kama haikuachi hio dunia inazungukaje kwenye orbit? na zile satelite ambazo zipo angani kama dunia inazunguka kwenye orbit mbona hatuzigongi? tunaambiwa dunia inazunguka kwa speed kubwa sana ina maana satelite zinamatch speed ya dunia?


Theory ya taycho brahe
Jamaa huyu mdanish (denmark) alitoa theory yake ambayo inamashiko tu

-sayari nyengine kama mercury na venus zinazunguka jua
-then jua na mwezi vinazunguka dunia

Tychonian_system.svg


Kama theory ya juu ipo sahihi inamaana hata dunia haizunguki bali jua ndio linatuzunguka.

Mnaonaje hii ipoje? kuna mtu ana point za kuprove kuwa galileo yupo sahihi?

Mkuu nimekusoma maswali yako na pia nimekuelewa vzr.Inaonekana ulisoma physics ila nahisi hukubahatika kuendelea nayo hasa ktk higher levels.Ila una haki ya kuuliza ili walau upate majibu
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nitoe Rough knowledge kama Astronomer na mdau mkubwa space engineering sasa tuanzia hapo kwa ukiwa juu ya ndege dunia inakuacha ,Ndege zote kasoro rocket zipo ndani ya dunia hivo hata upae nayo aje dunia haiwezi kukuacha mana upo ndani ni kweli dunia inazunguka ktk njia yake ya duara orbital kwanini hatugundui kama inazunguka kwa vile tumo ndani yake na ipo ktk constant speed yani mabadiliko ya speed na kujilinganisha na stationary object uwapo ktk chombo kinacho safiri ndo utagundua upo kwenye mwendo , Satellite zote zipo nje ya dunia na sio kuwa zote zina match speed na dunia no hizo zinazofanana speed na dunia ni Geostationary sat zipo umbali wa 36000Km na zinatembea hazipo stationary sasa nitoe darasa na maswali juu umewah jiuliza kwanini tuna elekeza dishi zetu labda azam upande fulani fixed ile hali satellite ipo ktk mwendo? yani angular velocity
 
1. Dunia sio duara bali ni bapa isipokuwa ni bapa yenye milima na mabonde.

2. Dunia hsizunguki jua. Tumia akili ya kawaida, chukua mpira au chubgwa kisha igundike zile toothpick kueneza pande zote alafu zungusha. Utaona kuna point fulani ukifika toothpick zinadondoka.

Kama dunia duara why sisi hatudondoki? Nilikubali dunia duara ili nifaulu mitihani lakini moyoni nasema NO.
Reasoning nyingine ni za ajabu kweli kweli. Ngoja nipite kwanza
 
Duuh? Mwalimu gani huyo aliyekusomesha? Bila ya kukupa uzaifu wa theory hiyo? Ukiambiwa na wewe ujiambie mkuu, Jua ndio lenye kuzunguka natumai unaliona kutokea mashariki kuendea magharibi >>>kukusaidia tafuta Heliocentric theory(sun center theory) theory inamapungufu sana >>>>Geothentric theory(Earth center theory) theory ipo sahihi
 
CHIEF-MKWAWA hii ndio shida ya elimu yetu. Waliosoma wanashindwa kufafanua jambo katika lugha nyepesi ya mtu wa kawaida kuelewa.
 
CHIEF MKWAWA hii ndio shida ya elimu yetu. Waliosoma wanashindwa kufafanua jambo katika lugha nyepesi ya mtu wa kawaida kuelewa.
Uko sahihi tangu Jana nilikuwa naipitia hii thread. Watu wanashindwa kufafanua wanachofahamu kutoka darasani wanaanza kukashifu mtoa post.
 
Ukiwa ndani ya bus linaloenda, halafu ukaruka juu unadhani utatua wapi? You will land at same spot you launched from as long as the bus is moving with un accelerated velocity, its Newton's first law of motion or inertia

mkuu phys uligonga ngapi? hii sentesi inaonyesha unajua phys hata kama utakua ulipata d
 
mkuu phys uligonga ngapi? hii sentesi inaonyesha unajua phys hata kama utakua ulipata d

Wore tumefundishwa hivyo shule na ndivyo tunavyoamini kwamba mtu akiwa ndani ya gari au kitu chenye mwendo, ataendelea kua katika hali ya mwendo hadi pale nguvu nyingine itakapoathiri hivyo kitu kubadili hali ya huo mwendo.

Sasa Chief-Mkwawa anachouliza hapa, hata kama nipo kwenye pickup nikaruka kuelekea huu umbali wa km 5, ni kweli kwa kipindi Fulani utaendelea kua katika hali ya mwendo, lakini kwa huo umbali hiyo nguvu itaisha na ukija kurudi chini pickup itakua imeshasogea mbali sana huwezi kudondokea kwenye pickup tena.
 
Uko sahihi tangu Jana nilikuwa naipitia hii thread. Watu wanashindwa kufafanua wanachofahamu kutoka darasani wanaanza kukashifu mtoa post.

Mimi nnachofaha, hizi zote ni theory tu, hii ya duniani kulizunguka kua ndio imeonekana kuwa na ukweli kidogo lakini sio kwamba iko sahihi, ndio maana Leo hii anaweza kutokea mwanasayansi mwingine akaipinga kwa hoja na akaja na theory mpya kabisa na vigezo vya kwa nini anafikiria huko sahihi, hapo itapimwa na tutaambiwa theory mpya inavyosema. Hii ni sawa na Sayari, Mwanzo ni tuliambiwa ziko Tisa, lakini wanagundua zingine na tafiti zinaendelea.

Sababu ni kwamba, hivi vitu vipo tayari haiku ten gene sea na MTU, kama vile anaetengeneza ndege au gari anaeweza kukwambia ametumia kanuni gani ili chombo chake kifanye Kazi. Hivyo basi kujaribu kufikiri na kuwa na mawazo mbadala sio kosa wala kutokuelewa jambo.

Shukrani sana mkuu
 
Danny Job,

Sure it make sense kwenye nguvu ya uvutano, je kwa nasa, china na urusi ambao wanatuma vyombo kwenye anga za juu wakirudi hawaikuti dunia pale walipoiacha? inakuwa imesogea kwengine?

na zile picha za toka anga ya juu mbona sjawahi kuona hata moja ikionesha dunia yetu ikizunguka kwa speed?

Kuhusu speed ya dunia.ulichokosea ni kufikilia uwezo ulionao wewe ukaulinganisha na dunia. Chukulia tumeweka mashindano ya mbio za mita moja kati yako wewe na sisimizi kumbuka mita moja sijakosea. Hivi wewe si milliseconds kadhaa umemaliza mashindano je sisimizi atachukua mda gani..concept hapa ni kwamba dunia kwa ukubwa wake inaweza kucover kilometer nyingi kwa mda mchache kuliko unavyofikilia. Hivyo hiyo speed usidhani utaiona dunia ikiwa inakwenda kwa kasi sana! Ni ipo mwendo wa kinyonga brother brother
 
Kuhusu speed ya dunia.ulichokosea ni kufikilia uwezo ulionao wewe ukaulinganisha na dunia. Chukulia tumeweka mashindano ya mbio za mita moja kati yako wewe na sisimizi kumbuka mita moja sijakosea. Hivi wewe si milliseconds kadhaa umemaliza mashindano je sisimizi atachukua mda gani..concept hapa ni kwamba dunia kwa ukubwa wake inaweza kucover kilometer nyingi kwa mda mchache kuliko unavyofikilia. Hivyo hiyo speed usidhani utaiona dunia ikiwa inakwenda kwa kasi sana! Ni ipo mwendo wa kinyonga brother brother
Huwezi kunotice au kugundua upo kwenye motion kama upo ndani ya icho kitu kinachozunguka na pia kama kiko ktk constant speed
 
Heliocentric vs Geocentric in 21st Century 🙂
Geocentric hio nadharia ni religion based na watawala enzi hizo kina Martin Luther walitaka mashuleni ifundishwe ivo yani earth iko centre. Tunamshukuru nicolas Copernicus kwa nadharia yake ya Heliocentric yani sun center
 
yap nakubali nitatua pale pale ila basi litaniacha litakuwa mbele si sawa?

dunia inajizungusha kwenye orbit kwa kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa, ina maana kama nimepanda hellcopter nikasimama juu angani kwa sekunde 10 basi dunia ingeniacha kilomita 300, je kwanini hainiachi?

na hawa nasa wanapotuma vifaa nje ya dunia vikirudi haviji sehemu ile ile vilipotokea? maana dunia inakuwa imeshamove pale ipo eneo jengine. au ni changa la macho tu tunapigwa

Ni kweli mkuu huwa dunia hua imeshamove but kitu kimoja mnachokosea kuzani kuwa dunia ni inamove kwa speed ya ajabu sana ukweli ni kuwa ipo polepole sana..hivyo kama chombo kipo nje ya gravity ya dunia .kinapaswa kiwe na kwenye mwendo ili kiwe sambamba na dunia!
 
1. Dunia sio duara bali ni bapa isipokuwa ni bapa yenye milima na mabonde.

2. Dunia hsizunguki jua. Tumia akili ya kawaida, chukua mpira au chubgwa kisha igundike zile toothpick kueneza pande zote alafu zungusha. Utaona kuna point fulani ukifika toothpick zinadondoka.

Kama dunia duara why sisi hatudondoki? Nilikubali dunia duara ili nifaulu mitihani lakini moyoni nasema NO.
Hatundoki kwa vile kuna gravity ina act kutuvuta centre of the earth
 
Ukisoma kitabu cha physics cha zamani acha hivi vya nyambari nyangwine kitabu hicho katika topic ya astronomy kuna theories mbili ambazo zinazungumzia kati ya jua na sayari kipi kinazunguka mwenzake;

Sasa kuna hiyo theory ya inasema kwamba juo lipo stationary/tulivu na sayari zipo kwenye mwendo kulizungua jua kwenye orbit zake

Imetupiliwa mbali hiyo theory hakuna namna kwa space bodies including sun kuwa unmovable..space hairuhusu kitu chochote ki hold position. Hata hivyo vi space ship havisimami na ni hatari sana kujalibu kufanya hivyo kwa sababu utaacha space I decide where to put u!
 
Moja katika topic za kuvutia ni astrophysics, why hamvutiwi na vitu vinaovoonekana na vinaelezeka kwa shida
hebu jaribu hata kugoogle kidogo ujifunze unaishije ishije
 
mkuu inategemea unaruka uelekeo upi,kama unaruka juu tu bila kulekea kushoto au kuli nyuma au mbele basi utatua katika point ileile ndani ya gari, newtons first law mkuu.

unapozungumzia dunia unazungumzia mpaka magnetic field ambayo ndiyo force inayoweka kila kitu kinasie duniani pamoja na gravitational force. ili hiyo ndege iachwa ni lazima kusiwe na magnetic field na gravitation force iwe 0 hapo newtons law haita apply na ukisemacho kitatokea.

Ukweli mtupu
 
Chief-Mkwawa,

Katika nukuu hizi sijaona yoyote inayoonesha dunia haizunguki jua. Au labda kwa kuwa kuna neno foundation linatajwa ? au hii "The world is firmly established, it will not be moved."???

Swali: firmly established to where or to what?? will not be be moved from where or to where?? Haiwezi kuwa it will not be moved from its orbit???

Mkuu wewe ni Genius
 
Mie sio mtalaamu wa jiografia... ckupata bahati ya kuisoma angalau to A-Level lakini ngoja tutumie akili ya kawaida! Let's assume kwamba gari unayoizungumza ni kubwa sana, kwa mapana na marefu...

let's say ni kama kutoka Dar hadi Mwanza kwa upana na urefu... assumption is based on the fact kwamba hata dunia nayo ni kuwa sana!!

Sasa ndo upo juu ya gari, assuming haupo kwenye ncha kabisa ya gari husika huku nikijaribu kuamini kwamba hata humu duniani tunamoishi si kwamba tupo nchani! Sasa ukiwa juu ya hilo gari (kubwa), unaamua kuruka! Je, gari hiyo kubwa itakuwa na kasi gani kiasi kwamba, hadi unadondoka inakuwa tayari imeshakuacha?

Maana yangu ni kwamba, kama utakuwa umesimama, let's umbali wa 1km kutoka kwenye ncha moja ya gari, basi gari liwe limeenda kwa umbali wa zaidi ya 1km kabla hujaondoka ndipo utaweza kudondokea nje ya eneo la gari!!!

Tukichukua mfano huo kisha tukaupeleka kwenye principles za wana-jiografia, ni kwamba hata utakaporuka na ndege, kutokana na ukubwa wa dunia bado utakuwa around and within the earth circumference hata kama utakuwa above it... which means, utakapoamua ama kwa voluntary or involuntarily ku-descend bado utafikia duniani coz' bado ulikuwa around the dunia circumference!

Is like lile gari letu lenye urefu kutoka Dar hadi Mwanza... assume umeruka ukiwa Dodoma wakati sehemu ya gari bado ipo Dar es salaam (almost 500 km) na sehemu nyingine ipo Mwanza lakini gari hiyo inaelekea Kampala!

Sasa wewe ukisharuka, ina maana hata kama utaweza ku-float hewani kwa saa 3, bado ile sehemu ya gari iliyokuwa Dar itakuwa haijakupita... sana sana badala ya kuwa Dar es salaam, itakuwa mbele kidogo ya Morogoro na ili ikupite basi uendelee kuelea kwa saa nyingi zaidi ili hadi kile kipande ambach kipo Morogo kiweze kuvuka Dodoma na hapo ukidondoka, gari ndo itakuwa imekupita!!!

Dunia hu move na kila kitu kilicho kwenye dunia hadi anga la dunia kwaiyo iyo ndege ipo kwenye anga la dunia ambalo nalo hu move pamoja na dunia. Kufill kama dunia ina move labda dunia ipige brek lakini ndege haimove free bali ipo attached na movement ya dunia hii ni sawa sawa na kuwa kwenye sit ya daladala dereva ataendesha speed 180 lakini wewe utabaki umekaa kwenye siti bila bugdha yoyote kakuwa upo attached na speed ya daladala(daladala ni dunia inayoelea kwenye vacum) ila sisi tunaona kuwa daladala linamove kwa kuwa daladala ni dogo (assume abiria wanaukubwa wa bacteria kwenye dalala) believe me you will not notice any thing but daladala ikipiga brek ghafra atanotice kwa sababu now your body will move free
 
Back
Top Bottom