limetumbuka,
Mfano, nipo juu ya gari then nikaruka juu basi gari litaniacha na mimi nitadondoka chini, iweje ndege imeruka ipo juu uniambie ipo duniani bado?
halafu na satelite (man made sio sayari) si zipo juu ya dunia why hatuzigongi?
Mie sio mtalaamu wa jiografia... ckupata bahati ya kuisoma angalau to A-Level lakini ngoja tutumie akili ya kawaida! Let's assume kwamba gari unayoizungumza ni kubwa sana, kwa mapana na marefu...
let's say ni kama kutoka Dar hadi Mwanza kwa upana na urefu... assumption is based on the fact kwamba hata dunia nayo ni kuwa sana!!
Sasa ndo upo juu ya gari, assuming haupo kwenye ncha kabisa ya gari husika huku nikijaribu kuamini kwamba hata humu duniani tunamoishi si kwamba tupo nchani! Sasa ukiwa juu ya hilo gari (kubwa), unaamua kuruka! Je, gari hiyo kubwa itakuwa na kasi gani kiasi kwamba, hadi unadondoka inakuwa tayari imeshakuacha?
Maana yangu ni kwamba, kama utakuwa umesimama, let's umbali wa 1km kutoka kwenye ncha moja ya gari, basi gari liwe limeenda kwa umbali wa zaidi ya 1km kabla hujaondoka ndipo utaweza kudondokea nje ya eneo la gari!!!
Tukichukua mfano huo kisha tukaupeleka kwenye principles za wana-jiografia, ni kwamba hata utakaporuka na ndege, kutokana na ukubwa wa dunia bado utakuwa around and within the earth circumference hata kama utakuwa above it... which means, utakapoamua ama kwa voluntary or involuntarily ku-descend bado utafikia duniani coz' bado ulikuwa around the dunia circumference!
Is like lile gari letu lenye urefu kutoka Dar hadi Mwanza... assume umeruka ukiwa Dodoma wakati sehemu ya gari bado ipo Dar es salaam (almost 500 km) na sehemu nyingine ipo Mwanza lakini gari hiyo inaelekea Kampala!
Sasa wewe ukisharuka, ina maana hata kama utaweza ku-float hewani kwa saa 3, bado ile sehemu ya gari iliyokuwa Dar itakuwa haijakupita... sana sana badala ya kuwa Dar es salaam, itakuwa mbele kidogo ya Morogoro na ili ikupite basi uendelee kuelea kwa saa nyingi zaidi ili hadi kile kipande ambach kipo Morogo kiweze kuvuka Dodoma na hapo ukidondoka, gari ndo itakuwa imekupita!!!