.........
ushahidi wa macho
wakati wa summer northern hemisphere jua tunaliona likienda west-west-south mpaka mchana then west-west north hadi usiku kama picha inavyoonesha.
Sijaelewa vizuri mchoro huu. We umeuelewa kabisa? Hata hivyo ningependa kujua huu "ushahidi wa macho" aliufanya nani.. ili nisitumie nguvu sana kufikiri kumbe ni watu wamefabricate. Ningependa kujua aliyetoa huo ushahidi au ni hao jamaa wenyewe?
...kwenye theory ya heliocentric tunaambiwa dunia inajizungusha kwenye mhimili wake huku inazunguka jua, na kinachosababisha majira ya mwaka ni kwamba dunia
inajitilt nyuzi 23.44. upande unaokuwa karibu na jua kunakuwa ndio summer na upande ambao upo mbali na jua inakuwa ndio winter kama picha inavyoonyesha tena.
kama dunia
inajitilt kuelekea kwenye jua inamaana ile northern hemisphere yetu pia nayo itaathirika na jua litacover eneo kubwa
Dunia inajitilt??? Unamaanisha kuna wakati inakuwa angle nyuzi 0 halafu wakati wa summer inajitilt kwa 23.44??? Hapana dunia haijitilt bali iko tayari katika angle hiyo na angle hiyo haibadiliki..iko hivyo hivyo forever... angalia picha hii

Dunia (ya bluu) haibadili angle ya mhimili wake bali northern hemisphere inakuwa more exposed kwa jua wakati hicho kitufe cha bluee kinapokuwa upande wa kulia na kinapokuwa upande wa kushoto (hapo ni nusu mwaka tayari) southern hemisphere inakuwa more exposed na na northern less exposed interms of direct sunlight (hence intensity and heat).
tujikumbushe kitu hapa dunia inaenda ant-clockwise sio? inatoka west kwenda east hivyo ndio maana tunaona jua linatoka east kwenda west (bado tupo heliocentric)
Sawa hakuna ubishi hapo.
kutokana na mchoro hapo juu unatonesha kuwa dunia ikijitilt basi direction ya jua itabadilika na kuwa west-west-north mpaka mchana then west-west-south mpaka usiku kama picha inavyoonesha
Kama nilivyosema dunia haijitilt periodically. Iko tayari tilted na agle inakuwa maintained kama animation inavyoonesha hapo juu.
Kwanza hiyo animation niliyoweka umeielewa?
tunatoka sasa heliocentric tunakuja kimacho sasa
hakujawahi kuthibitika jua likienda upande wa kaskazini hata mara moja kwenye northern hemisphere, hivyo inamaana dunia haijitilt na kama haijitilt heliocentric imefeli kuelezea majira ya mwaka na kama majira ya mwaka yameshindwa kuelezeka ina maana theory haipo sahihi.
Una maana gani hakujawahi kuthibitika. Aisee mbona jambo dogo sana hili yaani mwezi wa saba mwaka huu chombo cha Marekani kitafika Pluto halafu hii ishu ya kuthibitika jua kwenda kaskazi iwe ni utata?? Taratibu bana!! Jua linafika vizuri tu japo si kiwango cha kuwa la utosi hasa kama unazungumzia arctic. Hujui nchi kama Norway ama Sweden kuna wakati saa
sita usiku si giza totoro kama huku Bongo?
Unajua hilo?
hio ilikuwa ni observation ya kwanza jamaa wana njia nyengine kama hio ya upepo niliolezea juu pamoja na hizi.
1.hovering and falling
2.stellar parallax
3.scientific experiments
wasome zaidi hapa
Heliocentric theory is wrong (pt1) - The Wild Heretic
Sijasoma kila kitu walichoandika hapo hadi nitakapopata muda maana wameandika meeengi na presentation za kitoto kama kauli za "ubishi umeisha!! Heliocentric blahblah tumeiprove wrong!!"
Utoto!! Nikipata muda ntawasoma.
Kwa harakahara hiyo ya Hovering and falling naona kama imeshajibiwa na wadau kwa mifano ya abiria aliye ndani ya gari. Kama hujaelewa niko tayari kufafanua kwa lugha rahisi kabisa.
Nikupe tu hint: Hivi konda akiwa ndani ya daladala iliyo katika kasi na huyo konda anatoka nyuma alikokwenda kuchukua nauli na sasa anarudi kwa dereva halafu kabla hajafika kwa dereva, huyo konda akasimama ili amrudishie abiria wa siti ya kati chenji yake..
huyo konda anakuwa kweli kasimama au bado anakwenda kwa mwendo wa kasi ya gari? Ukielewa vizuri hii concept hoja ya hovering (helkopta kuganda hewani kwanini haiachwi) and falling (konda akidondosha coin inaangukia wapi) inajibika vizuri plus hoja za Sheikh fulani katika post za nyuma kuwa dunia haizunguki.
NB. Ni vizuri ujijengee tabia ya kufuatilia facts za kisayansi juu ya mwili wa binadamu, chura, mende, panzi, kunguni, maji, hewa, ubongo, jua, nyota, Samsung, Bill Gates, Justin Bieber, Nokia Lumi (anga zako), hisabati plus everything else etc hutababaishwa na hoja nyepesi za watu kama hao wala hutajihangaisha kuthibitisha
maajabu na usahihi wa Biblia ama Korani kwa kuifananisha na sayansi na wala
hutaogopa kujadili dini eti utakufuru.. ila unatakiwa ujue kweli mambo..sayansi na falsafa (dini ikiwa ndani yake).