Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Na hii ndo imeua biashara nyingi, purchasing power ya watu imepungua hivyo kupunguza kasi ya mzunguko wa pesa huku Kodi zikiwa za kukomoana.Ila malengo yake ya kuwafanya watu waishi Kama mashetani yametimia
Mleta mada anafumbia macho haya,anadeal na angle anayoona ni nafuu kwake kupotosha watu!
 
Hivyo ulivyovitaka ni vitu muhimu lakini ni vidogo sana kwa Taifa. Havihitajiki kuwa wimbo wa kila siku.

Kuna wakati niliishi Bamako, Mali - nchi ambayo robo 3 ni jangwa. Ndani ya mwaka mmoja flyovers zinajengwa hata 3, husikii hata kwenye TV wakitangaza. Unapita barabarani, unashangaa "ala, kumbe na hapa wanajenga flyover!". Tena zilikuwa ni flyovers kamili siyo kama lile daraja la TAZARA.

Tunapiga kelele sana za mafanikio kwa vitu vidogo sana kwa Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu hiyo kyabakari kama una manisha ile iliyopo Butiama-Musoma inaitwa Kiabakari
 
Kwa hiyo hayo mengi aliyofanya ndo yamepelekea kuongeza only USD 100 kwenye GNI na kuvuga kabisa market systems za mazao ya korosho,kahawa,mbaazi na tumbaku huku ukuaji wa uchumi ukiongezeka kutoka 7% hadi 4% si ndiyo mkuu?
Mengi aliyoyatenda ndio yametupeleka kwenye uchumi wa kati
 
Mafanikio makubwa yanagharama zake. Mwaka huu mshahara umeongezwa. Kuhusu ajira ni lazima ujue haiwezekani kila mtu akaajiriqa na serikali. Serikali inatengeneza mazingira mazuri kupitia PPP na huko ajira rasmi na zisizo rasmi hutokea...
Kwani aliyeua sector binafsi nchi hii ni nani mkuu?
 
Mafanikio makubwa yanagharama zake. Mwaka huu mshahara umeongezwa.
Kuhusu ajira ni lazima ujue haiwezekani kila mtu akaajiriqa na serikali. Serikali inatengeneza mazingira mazuri kupitia PPP na huko ajira rasmi na zisizo rasmi hutokea.
Ajira za walimu zimetangazwa. Najua bado eneo hilo lina changamoto ila tutafika pazuri zaidi
Kwenye uchumi kwa ujumla Rais Magufuli amepepesuka sana. Ni sawa na mtu anayeanzisha kiwanda cha magunia ya kuwekea nafaka halafu kila siku anatuma watu kwenda kufyeka mashamba yote yanayozalisha nafaka. Hayo magunia utaweka nini?

Kinachotengeneza ajira, kwa kiasi kikubwa ni sekta binafsi. Sera zake mbaya zimeiua na kuididimiza sekta binafsi. Kama unaiua sekta binafsi, ajira zitatoka wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mengi aliyoyatenda ndio yametupeleka kwenye uchumi wa kati
Aliyefanya kazi kubwa kutupeleka kwenye uwigo wa chini wa uchumi wa kati (hatujafika uchumi wa kati) ni Mkapa na Kikwete. Hawa kwa vipindi vyao vya uongozi walipandisha per capita ya mtanzania kwa zaidi ya dola 400. Magufuli miaka 5 amepandisha per capita kwa dola 100. Magufuli administration has been the worst of all.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo yameongeza USD 100.00 in five years? Kweli jamaa ni jembe
Sijijui mbona unataka kubisha tuu? Hebu niambieni, unajua kuwa Tanzania imetangazwa kuingia kwenye uchumi wa kati? Unafikiri ni vigezo gani vilitumika kutuweka hapo?
 
Kaka yani mafanikio yanayoongelewa na wenzetu sijui wenyewe wanangalia kwa kutumia darubini-yani ukitembea mikoa hali za watu zipo chini sana.
Nakubaliana na wewe. Kwa vipimo vyote, uchumi kwa ujumla wa nchi ukuaji wake umeanguka. Maendeleo ya watu yameanguka zaidi. Ukichanganya na ongezeko la watu, hali imekuwa mvaya zaidi.

Kwa ujumla utawala huu, tofauti na unavyojigamba, umewamaliza kabisa hata hao wanaoitwa wanyonge. Sijui waliofaidika ni watu gani. Labda wateule wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Hayo yanawahusu watu wote na fedha zimepelekwa huko badala ya kuzirejesha majimboni kwanini tunawahukumu wabunge na madiwani kuwa miradi hawakuiombea fedha? Kwanini Wasiendelee maana elimu bure inamgusa kila mtu jimbon?
 
Kwamba Bibi yangu akiumwa huko Mpwapwike Ndugu wachangishane Ili tumpakie Bibi kwenye Ndege..... Serious?
Sio lazima iwe hivyo Ila pata picha Bibi yako anaumwa huko unaposema halafu anatakiwa asafirishwe haraka kupelekwa Muhimbili na hakuna usafiri mwingine wowote zaidi ya gari, hata Kama mna hela hela hiyo inaweza isisaidie sana. Hatahivyo, simaanishi kuwa Ni lazima wagonjwa wote wasafirishwe kwa ndege ila nimeonesha umuhimu wake.

Ukitaka ujue umuhimu wake muulize Tundu Lissu, au ulitaka asafirishwe kwa basi kwenda Nairobi?

Ukitaka ujue umuhimu wa ndege Waulize CHADEMA, wao kampeni zao hutumia helikopta na watakupa sababu nzuri ni kwanini wanatumia
 
Sijijui mbona unataka kubisha tuu? Hebu niambieni, unajua kuwa Tanzania imetangazwa kuingia kwenye uchumi wa kati? Unafikiri ni vigezo gani vilitumika kutuweka hapo?
Kwanza ni uwongo kueleza kuwa tumetangazwa kuingia kwenye uchumi wa kati. Sisi tumefikia lower boundary ya uchumi wa kati. Lakini kwa kiasi kikubwa waliotufikisha hapo ni Mkapa na Kikwete, siyo Magufuli. Kikwete na Mkapa, kila mmoja alitupandisha kwa wastani wa zaidi ya dola 400. Magufuli miaka yake yote mitano katupandisha kwa dola 100 tu.

Ni sawa na gari ikusafirishe toka Tunduma mpaka Kimara, halafu kimara ukapanda daladala mpaka Posta, halafu dereva wa dala dala akaanza kutamba kuwa yeye ndiye aliyekutoa Tunduma kukufikisha Dar. Ni kutafuta sifa kwa njia za kuwahadaa watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom