Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Sijijui mbona unataka kubisha tuu? Hebu niambieni, unajua kuwa Tanzania imetangazwa kuingia kwenye uchumi wa kati? Unafikiri ni vigezo gani vilitumika kutuweka hapo?
Kijezo kikuu kilichotumika ni GNI,Sasa wastani wetu ni USD 1080 per year.Mwaka 2015 GNI ilikuwa USD 980.00, only 20 USD away from uchumi wa kati,now tupo ndani ya uchumi wa kati tena kabla ya muda maana GNI yetu Sasa ni USD 1080,yaani mchapa kazi kaongeza USD 100 in five good years
 
Mafanikio makubwa yanagharama zake. Mwaka huu mshahara umeongezwa.
Kuhusu ajira ni lazima ujue haiwezekani kila mtu akaajiriqa na serikali. Serikali inatengeneza mazingira mazuri kupitia PPP na huko ajira rasmi na zisizo rasmi hutokea.
Ajira za walimu zimetangazwa. Najua bado eneo hilo lina changamoto ila tutafika pazuri zaidi
Kikwete aliwezaje?Miradi mikubwa ilikuwa inafanyika lakini maisha yalikuwa nafuu na biashara zilikuwa zinaenda kwa maana ya mzunguko wa fedha!Mfano ndege,kuna tija kweli kununua ndege zote hizo?

Kwanini hakuna uwazi na CAG kapigwa pini kukagua ATCL?Je,kujengs uwanja wa kimataifa CHATO kuna tija?

Mnaposifia tu kila jambo bila tafakari ya kina mnafanya JPM na seriksli yake kufanya makosa zaidi!
 
Upuuzi mtupu. Aliyefanya kazi kubwa kutupeleka kwenye uwigo wa chini wa uchumi wa kati (hatujafika uchumi wa kati) ni Mkapa na Kikwete. Hawa kwa vipindi vyao vya uongozi walipandisha per capita ya mtanzania kwa zaidi ya dola 400. Magufuli miaka 5 amepandisha per capita kwa dola 100. Magufuli administration has been the worst of all.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna anayekataa kazi nzuri iliyofanywa na watangulizi wake ila Kama yeye angeboronga tungefikaje kwenye huo uchumi wa kati?
 
Kijezo kikuu kilichotumika ni GNI,Sasa wastani wetu ni USD 1080 per year.Mwaka 2015 GNI ilikuwa USD 980.00, only 20 USD away from uchumi wa kati,now tupo ndani ya uchumi wa kati tena kabla ya muda maana GNI yetu Sasa ni USD 1080,yaani mchapa kazi kaongeza USD 100 in five good years
Ila kutufikisha hapo. Hata Mussa alifanya kazi ya kuwatoa wanawaisraeli Misri lakini ni Haruni aliyewafikisha kanani
 
Kikwete aliwezaje?Miradi mikubwa ilikuwa inafanyika lakini maisha yalikuwa nafuu na biashara zilikuwa zinaenda kwa maana ya mzunguko wa fedha!Mfano ndege,kuna tija kweli kununua ndege zote hizo?Kwanini hakuna uwazi na CAG kapigwa pini kukagua ATCL?Je,kujengs uwanja wa kimataifa CHATO kuna tija?
Mnaposifia tu kila jambo bila tafakari ya kina mnafanya JPM na seriksli yake kufanya makosa zaidi!
Kikwete alifanya alipoweza kwa staili yake, Magufuli naye anafanya kwa staili yake.
Kubwa ni kuwa pesa rahisi haipo. Fanya kazi upate ujira. Rushwa imedhibitiwa na Kodi inakusanywa.
 
Ila kutufikisha hapo. Hata Mussa alifanya kazi ya kuwatoa wanawaisraeli Misri lakini ni Haruni aliyewafikisha kanani
Ndo maana namsifia kwa kuongeza shilingi laki mbili kwenye wastani wa kipato Cha mnyonge kwa miaka mitano yaani 40,000 kwa mwaka pamoja na kupiga kazi sana
 
Kikwete alifanya alipoweza kwa staili yake, Magufuli naye anafanya kwa staili yake.
Kubwa ni kuwa pesa rahisi haipo. Fanya kazi upate ujira. Rushwa imedhibitiwa na Kodi inakusanywa.
Huyu Magu inaonekana kazi nyingi anafanya for nothing,yaani hatumii maarifa hivyo outcome yake inakuwa zero.
 
Kikwete alifanya alipoweza kwa staili yake, Magufuli naye anafanya kwa staili yake.
Kubwa ni kuwa pesa rahisi haipo. Fanya kazi upate ujira. Rushwa imedhibitiwa na Kodi inakusanywa.
Rushwa imedhibitiwaje?Kura za maoni CCM haijakupa somo kuwa rushwa bado ni kubwa?Kwanini ununuzi wa ndege haujafuata utaratibu wa manunuzi wa serikali?kwanini ATCL haikaguliwi na CAG?Nini kinafichwa?Hujua athari kwenye mzunguko wa fedha kutumia matrilioni kununua ndege nyingi tena cash?

Mmefanya mazingira ya biashara kuwa magumu kwa kupunguza mzunguko halafu watu wakilalamika mnasingizia mianya ya rushwa imezibwa!!0Acheni ushabiki maandazi!
 
Mafanikio makubwa yanagharama zake. Mwaka huu mshahara umeongezwa.
Kuhusu ajira ni lazima ujue haiwezekani kila mtu akaajiriqa na serikali. Serikali inatengeneza mazingira mazuri kupitia PPP na huko ajira rasmi na zisizo rasmi hutokea.
Ajira za walimu zimetangazwa. Najua bado eneo hilo lina changamoto ila tutafika pazuri zaidi
Mbona una hoja dhaifu namna hiyo mkuu, au unaona humu watoto sana.
 
Hakuna mtu anayebisha umuhimu wa miundombinu kwenye kuleta maendeleo lakini huwezi ukataka kujenga miundombinu yote kwa pamoja kama vile nchi inaondoka uksahau kuwa na wananchi wana mahitaji ya muhimu.

Hata marekani hadi leo bado wanajenga miundo mbinu. Hata Baba katika familia hawezi kwa kipato chake cha kawaida na mikopo akataka kujenda nyumba kununua Gari kununua shamba kuanzisha kampuni ati kwa vile hivyo ni vya muhimu bila kujali kuwa kuna watoto wanatakiwa kwenda shule.

Ni vema kuwa na vipaumbele lakini kwa uwiano ulio mzuri siyo kuwaumiza watanzania kwa umasikini kwa kisingizio cha kujenga miundo mbinu. Hilo ndiyo tatizo linalozungumzwa hivi mwananchi ambaye ameshindwa kumpeleka Mtoto wake shule au chuo ukimwambia pesa umenunulia ndege atakuelewa kweli.
 
Hakuna mtu anayebisha umuhimu wa miundombinu kwenye kuleta maendeleo lakini huwezi ukataka kujenga miundombinu yote kwa pamoja kama vile nchi inaondoka uksahau kuwa na wananchi wana mahitaji ya muhimu...
Mkuu ndio maana unaona zahanati zimejengwa kila Kona, watoto wanapata elimu bila malipo na watoto was masikini hawashindwi kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa ada, hawa wanapatiwa mikopo. Je, hapo sio kubalansi?
 
Rushwa imedhibitiwaje?Kura za maoni CCM haijakupa somo kuwa rushwa bado ni kubwa?Kwanini ununuzi wa ndege haujafuata utaratibu wa manunuzi wa serikali?kwanini ATCL haikaguliwi na CAG?Nini kinafichwa?Hujua athari kwenye mzunguko wa fedha kutumia matrilioni kununua ndege nyingi tena cash?
Mmefanya mazingira ya biashara kuwa magumu kwa kupunguza mzunguko halafu watu wakilalamika mnasingizia mianya ya rushwa imezibwa!!0Acheni ushabiki maandazi!
ATCL haikaguliwi na CAG? Una hakika?

Rushwa imedhibitiwa japo haijaisha. Vitendo vya rushwa kwenye kura za maoni vinashughulikiwa. Pia tambua kuwa sio wanaCCM wote ni waaminifu, wapo wenue shida na hao hakika wanashughulikiwa
 
Angeweza kwenye mfumuko wa bei kama alivyo fanya Rais Mkapa, hata msingemlaumu.
 
Ila kweli nimeamini ule msemo wa kindali " you'll never please human beings"

Hata Kama kusingekuwa na faida zozote za kiuchumi, Dar es Salaam nayo ni sehemu ya Tanzania tena kwenye watu wengi kuliko sehemu yoyote nchini. Foleni ni kero kubwa Sana na hata upinzani walishaliongelea hili. Hivi inakuwaje nongwa serikali kuamua kutumia Kodi ya wananchi kuwasaidia wananchi hao?
 
Kwahiyo ndege ina manufaa kuliko nyongeza ya mshahara kwa mtumishi!?

Hiyo ndege ina manufaa ya moja kwa moja kwa mtoto wa mtumishi aliyekosa mlo wa jioni?
 
Tanzania hatujawahi kuwa na mabwawa ya kuzalisha umeme.

Tanzania ndio tunaanza kujenga barabara awamu hii.

Tanzania kwa mara ya kwanza ndio imezindua "National Carrier" ATC.
.......
.......
.......
 
Back
Top Bottom