Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Salamu kwenu,

Kumekuwa na kelele nyingi kuwa ndege zetu hazina maana yoyote kwa mwananchi was kawaida. Watu wanaenda mbali zaidi kuhoji ikiwa flyovers za Dar es Salaam zina umuhimu wowote kwa watanzania waishio vijijini, mikoani huko.

Ukiangalia hizi hoja, unapata picha mbili. Ya kwanza ni kuwa ni kweli hawajui umuhimu wake na picha ya pili ni kuwa wanajua ila wameamua kupotosha. Picha zote mbili zinao wahusika, yaani wapo wasiojua na wapo wanaojua ila wameamua kupotosha. Kwa faida ya wote tuchambue kama ifuatavyo:

Utangulizi
Kujenga uchumi imara sio kazi rahisi. Ni kazi inayohitaji weledi na uwekezaji janja (smart investment) pamoja na mazingira wezeshi kiuchumi. Kufikia uchumi mzuri sio kazi ya muda mfupi ingawa matokeo chanya yanaweza kuonekana ndani ya muda mfupi Kama miaka mitano hivi. Haya yanakuwa ni viashiria kuwa tupo kwenye mstari sahihi (right track).

Kwanini watu huona kuwa flyovers na ndege haziwasaidii chochote?
Wanadamu tuna asili flani ya ubinafsi. Unataka uone wewe Kama wewe umefaidikaje. Aidha ukiacha ubinafsi, Ni kweli kuwa kwa macho ya kawaida, mfanyakazi atataka kuona mshahara mnono, mkulima atataka pembejeo, barabara ya uhakika ya kusafirisha mazao yake na soko la uhakika. Mwanafunzi atataka elimu Bora, vifaa vya kujifunzia na mazingira bora ya kujisomea. Watu wanataka huduma bora za afya kwa kuwa na vituo vya afya karibu yao, hospitali nzuri zenye vifaa na wataalamu wa kutosha. Hivyo matarajio yao Ni hivyo vitu kutimizea, na kwa hakika hivyo ndivyo serikali inapaswa kufanya.

Kwanini flyovers na ndege ni muhimu kwa watanzania wote hata kwa wale waishio nje ya Dar es Salaam na vijijini?

1. Flyovers
Dar es Salaam ni mji wa kibiashara na ndio mji wenye watu wengi zaidi Tanzania. Dar es Salaam ndio mji iliko hospitali ya taifa. Kila siku maelfu ya magari huongia Dar es Salaam kuleta wafanyabiashara wa ndani na nje, wagonjwa walioshindikana huko mikoani, watalii hasa wa ndani na bidhaa za mashambani.

Unapokuwa na msongamano mkubwa barabarani ni kuwa unapoteza muda mrefu kupeleka bidhaa sokoni, mgonjwa hospitalini na kuwahi kazini kwaajili ya kuwahudumia watanzania. Unapoondoa kero hiyo unakuwa hujamsaidia tuu mtu aishiye Dar Bali umemsaidia mkulima aliyeleta mazao yake manzese au kariakoo aharikishe biashara yake, mgonjwa aliyetoka mkoani kuwahi hospitali na mfanyakazi kuwahi kazini. Hapa utaokoa gharama za mafuta, muda na maisha ya mgonjwa. Pia utaongeza vivutio vya utalii na kupendezesha mji.

Ndege
Ndege zinarahisha usafiri wa ndani ya nchi. Unafika popote nchini ndani ya muda mfupi. Bibi akiumwa na kuzidiwa kule ikungi, mnachangishana anaenda sehemu ndege inapotua, huyoo anawahishwa hospitalini.

Uwepo wa usafiri wa ndani was uhakika unawafahya watalii waongezeke na hivyo Kukuza pato la taifa. Kuwa na ndege yenu (national carrier) inayofanya safari za nje inachangia sana kuongeza pato la taifa kwani watalii watalipa nauli jwa fedha za kigeni ambazo zitaingia Tanzania na watalipa fedha za kigeni wanapoingia hapa kufanya utalii. Hiyo itakuza ajira nchini kwa waongoza watalii, madereva, wenye hoteli, migahawa na orodha inaendelea.

Mazingira hayo yanatengeneza kipato cha uhakika ambacho kitakuwezesha kulipa watumishi mishahara mizuri zaidi, kujenga shule nyingi zaidi zenye ubora, hospitali zenye ubora zaidi, kutoa ruzuku kwa wakulima na orodha inaendelea.

Hongera Rais Magufuli kwa kufanya uwekezaji janja, hongera CCM, hongera Tanzania. Msioelewa sasa muelewe Rais anaposema tuko kwenye right track anamaanisha Nini.

Unaweza kuona nimetaja punje tuu ya mambo yaliyofanyika yenye lengo la kutufikisha mbali kiuchumi.

Fuatilia
Ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere
Ujenzi wa barabara
Uwekezaji kwenye madini
Ununuzi wa meli na vivuko

#2020 kura yangu kwa John
mkuu umeandika vizuri tu mfano ujenzi wa bwawa mwl nyerere sawa , hata miradi mingine ulio itaja ni sawa ila elewa kama nchi maskin ipo miradi kati ya miradi ulioitaja haikutakiwa kwenda kwa kasi na kufanya watu kuishi kama watumwa kwa kusosa mzunguko wa fedha katika jamii , kupanga ni kuchagua, lazima ilitupasa kufanya miradi ambayo ikiendelea pasiwepo wananchi kufunga mikanda ,na hii ndo hoja kuu ya watanzania na sio kila kitu lazima kimalizike kwa miaka mitano, taifa hili lipo na lilikuepo na litaendelea kuwepo, so watu wanazungumzia sana ndege sio kwamaba sio muhim lakini wanalinganisha tu kwamba mfano tangu ndege zimenunuliwa na chango wake katika uchumi linganisha may be na utalii kipi kimeongeza sana katika pato la taifa?
Na je kweli kama nikuinua shirika letu la ndege ambalo ni jambo zuri why hatukuanaza nunua ha ndege hata tatu kwanza huku tukiendelea jipanga ?
kuhusu bwawa sina shida kabisa
kuhusu barabara sina shida sana hapo maana kila awamu imekua ikijitahidi but jk aliyajenga sana tunashukuru sana kwa hili maana pia zachangia sana kwenye uchumi wa serikali.
mwisho
mada yako nzuri but yaitaji mjadala mpana sana mkuu
 
Mshara uliongezwa kwa 2000 ukaja kwa 17,000/= kwa TGS C2

Ila kikwete 2014 aliongeza kwa 80,000/= kwenye TGS C1.

Hivi kweli Magu ameongez mshahara?

#YNWA
Kaka huwezi kufanya yote kwa wakati mmoja. Ili tufikie mafanikio ni lazima tukubali kutoa sadaka.

Kikwete mwenyewe pamoja na kuongeza watu walikuwa wanamzingua. Nakumbuka Kuna kipindi alikuwa mkali kidogo kuhusu nyongeza ya mshahara
 
Barabara, Flyovers, Shule,Zahanati, Viwanja vya michezo Viko wapi hapa kwetu kijiji sijaona hata komoja

Sasa Ulitaka Uwanja Wa Mkapa,unaochukua watazamaji 60K waujenge hapo KIJIJINI KIBINDA ambako hamzidi wanakijiji 2000...

Na Ukija Dar KULETA Ng'ombe vingunguti,hayo malori YATAPAA angani eee?!!
 
mkuu umeandika vizuri tu mfano ujenzi wa bwawa mwl nyerere sawa , hata miradi mingine ulio itaja ni sawa ila elewa kama nchi maskin ipo miradi kati ya miradi ulioitaja haikutakiwa kwenda kwa kasi na kufanya watu kuishi kama watumwa kwa kusosa mzunguko wa fedha katika jamii , kupanga ni kuchagua, lazima ilitupasa kufanya miradi ambayo ikiendelea pasiwepo wananchi kufunga mikanda ,na hii ndo hoja kuu ya watanzania na sio kila kitu lazima kimalizike kwa miaka mitano, taifa hili lipo na lilikuepo na litaendelea kuwepo, so watu wanazungumzia sana ndege sio kwamaba sio muhim lakini wanalinganisha tu kwamba mfano tangu ndege zimenunuliwa na chango wake katika uchumi linganisha may be na utalii kipi kimeongeza sana katika pato la taifa?
Na je kweli kama nikuinua shirika letu la ndege ambalo ni jambo zuri why hatukuanaza nunua ha ndege hata tatu kwanza huku tukiendelea jipanga ?
kuhusu bwawa sina shida kabisa
kuhusu barabara sina shida sana hapo maana kila awamu imekua ikijitahidi but jk aliyajenga sana tunashukuru sana kwa hili maana pia zachangia sana kwenye uchumi wa serikali.
mwisho
mada yako nzuri but yaitaji mjadala mpana sana mkuu
Shukrani Sana. Ni kweli yahitaji mjadala mpana
 
Yaaani Vinachekeshaga sanaaa...

Sasa Mtu Anapoitumia Huduma Ya Serikali Mfano Barabara,Flyovers,Shule,Zahanati,Viwanja vya michezo....

Kote huko inakuwa Ni KODI YAKE TU iliyotumika KUYAWEKA HAYO?!!!

Jamii Nikutegemeana Maana Ninavyopenda KULA UBWABWA wa Kutoka Mbeya Haina Maana nimekula PESA YANGU....yaani ile NOTI NYEKUNDU ya buku 10 iweze kuyeyushwa na kunyonywa na PARIETAL cells za UTUMBO WANGU MDOGO?!!!
Yani unajua mimi mwenyewe nashangaa sana hivi huduma muhimu ambazo ni za lazima kama Afya, barabara n.k unazifanyaje kuwa za kisiasa?

Malaysia ni kosa mwanasiasa kufanya hizi siasa sijui nitajenga barabara au kituo cha afya
 
Sasa Ulitaka Uwanja Wa Mkapa,unaochukua watazamaji 60K waujenge hapo KIJIJINI KIBINDA ambako hamzidi wanakijiji 2000...

Na Ukija Dar KULETA Ng'ombe vingunguti,hayo malori YATAPAA angani eee?!!
Dar ni myama gani Serengeti umeambiwa Tanzania ni Dar Watanzania wote tukaishi dar umesikia wapi kama akili zenu ndio hizo ccm kura yangu msinipangie inamuhu Lissu
 
Kwa hayo aliongea anaweza kupata ukuu wa wilaya
Sio rahisi kihivyo. Halafu uteuzi hautegemei mtu kuweka namba ya simu. Ni lazima upimwe na uonekane unafaa. Hapa ni uwanja wa sisi kujadiliana kuhusu nchi yetu na vile tunavyoviamini
 
Aisee ni rahisi Sana hasa kwa kuandika mambo ya kujifanya ww ni mzalendo zaid na unajua kujitolea
 
Dar ni myama gani Serengeti umeambiwa Tanzania ni Dar Watanzania wote tukaishi dar umesikia wapi kama akili zenu ndio hizo ccm kura yangu msinipangi inamuhu Lissu
Kura ni maamuzi yako ila kusaidiwa kuujua ukweli ili ufanye maamuzi sahihi ni wajibu wetu
 
Aisee ni rahisi Sana hasa kwa kuandika mambo ya kujifanya ww ni mzalendo zaid na unajua kujitolea
Sasa ni kosa kuandika unachokiamini? Kuandika mema ya nchi yako na kutetea viongozi wazalendo nao pia ni Uzalendo na sio kujifanya mzalendo. Kama ni kuandika wangapi wanaandika? Unaweza kumsoma mtu ni wa mtindo gani kwa maandishi yake
 
Dar ni myama gani Serengeti umeambiwa Tanzania ni Dar Watanzania wote tukaishi dar umesikia wapi kama akili zenu ndio hizo ccm kura yangu msinipangie inamuhu Lissu
Sawa.....ila Jua Ya Kwamba Dar es salaam pekee inachangia 80% ya Uchumi wote wa nchi.....
 
Kura ni maamuzi yako ila kusaidiwa kuujua ukweli ili ufanye maamuzi sahihi ni wajibu wetu
Hata ndege kupanda unasimuliwa tofauti ya madaraja na Flyovers hujui unataka unifundishe nani waku mpigia kura
 
Maendeleo ni watu si vitu,vitu ni matokeo ya maendeleo.Ushamba wa mtu wenu kupeleka taa za barabarani chattle akidhani chatlke ndo itaonekana ni mji haujawahi kumuisha
Watu waliozoea kishu ujima wa kuishi kwenye mapango utawajua tu.
Mtatoka lini huko?
 
Sasa ni kosa kuandika unachokiamini? Kuandika mema ya nchi yako na kutetea viongozi wazalendo nao pia ni Uzalendo na sio kujifanya mzalendo. Kama ni kuandika wangapi wanaandika? Unaweza kumsoma mtu ni wa mtindo gani kwa maandishi yake

Ndio maana nikasema Namba ya simu ni muhimu
 
Salamu kwenu,

Kumekuwa na kelele nyingi kuwa ndege zetu hazina maana yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Watu wanaenda mbali zaidi kuhoji ikiwa flyovers za Dar es Salaam zina umuhimu wowote kwa watanzania waishio vijijini, mikoani huko.

Ukiangalia hizi hoja, unapata picha mbili. Ya kwanza ni kuwa ni kweli hawajui umuhimu wake na picha ya pili ni kuwa wanajua ila wameamua kupotosha. Picha zote mbili zinao wahusika, yaani wapo wasiojua na wapo wanaojua ila wameamua kupotosha. Kwa faida ya wote tuchambue kama ifuatavyo:

Utangulizi
Kujenga uchumi imara sio kazi rahisi. Ni kazi inayohitaji weledi na uwekezaji janja (smart investment) pamoja na mazingira wezeshi kiuchumi. Kufikia uchumi mzuri sio kazi ya muda mfupi ingawa matokeo chanya yanaweza kuonekana ndani ya muda mfupi Kama miaka mitano hivi. Haya yanakuwa ni viashiria kuwa tupo kwenye mstari sahihi (right track).

Kwanini watu huona kuwa flyovers na ndege haziwasaidii chochote?
Wanadamu tuna asili flani ya ubinafsi. Unataka uone wewe Kama wewe umefaidikaje. Aidha ukiacha ubinafsi, Ni kweli kuwa kwa macho ya kawaida, mfanyakazi atataka kuona mshahara mnono, mkulima atataka pembejeo, barabara ya uhakika ya kusafirisha mazao yake na soko la uhakika. Mwanafunzi atataka elimu Bora, vifaa vya kujifunzia na mazingira bora ya kujisomea. Watu wanataka huduma bora za afya kwa kuwa na vituo vya afya karibu yao, hospitali nzuri zenye vifaa na wataalamu wa kutosha. Hivyo matarajio yao Ni hivyo vitu kutimizea, na kwa hakika hivyo ndivyo serikali inapaswa kufanya.

Kwanini flyovers na ndege ni muhimu kwa watanzania wote hata kwa wale waishio nje ya Dar es Salaam na vijijini?

1. Flyovers
Dar es Salaam ni mji wa kibiashara na ndio mji wenye watu wengi zaidi Tanzania. Dar es Salaam ndio mji iliko hospitali ya taifa. Kila siku maelfu ya magari huongia Dar es Salaam kuleta wafanyabiashara wa ndani na nje, wagonjwa walioshindikana huko mikoani, watalii hasa wa ndani na bidhaa za mashambani.

Unapokuwa na msongamano mkubwa barabarani ni kuwa unapoteza muda mrefu kupeleka bidhaa sokoni, mgonjwa hospitalini na kuwahi kazini kwaajili ya kuwahudumia watanzania. Unapoondoa kero hiyo unakuwa hujamsaidia tuu mtu aishiye Dar Bali umemsaidia mkulima aliyeleta mazao yake manzese au kariakoo aharikishe biashara yake, mgonjwa aliyetoka mkoani kuwahi hospitali na mfanyakazi kuwahi kazini. Hapa utaokoa gharama za mafuta, muda na maisha ya mgonjwa. Pia utaongeza vivutio vya utalii na kupendezesha mji.

Ndege
Ndege zinarahisha usafiri wa ndani ya nchi. Unafika popote nchini ndani ya muda mfupi. Bibi akiumwa na kuzidiwa kule ikungi, mnachangishana anaenda sehemu ndege inapotua, huyoo anawahishwa hospitalini.

Uwepo wa usafiri wa ndani was uhakika unawafahya watalii waongezeke na hivyo Kukuza pato la taifa. Kuwa na ndege yenu (national carrier) inayofanya safari za nje inachangia sana kuongeza pato la taifa kwani watalii watalipa nauli jwa fedha za kigeni ambazo zitaingia Tanzania na watalipa fedha za kigeni wanapoingia hapa kufanya utalii. Hiyo itakuza ajira nchini kwa waongoza watalii, madereva, wenye hoteli, migahawa na orodha inaendelea.

Mazingira hayo yanatengeneza kipato cha uhakika ambacho kitakuwezesha kulipa watumishi mishahara mizuri zaidi, kujenga shule nyingi zaidi zenye ubora, hospitali zenye ubora zaidi, kutoa ruzuku kwa wakulima na orodha inaendelea.

Hongera Rais Magufuli kwa kufanya uwekezaji janja, hongera CCM, hongera Tanzania. Msioelewa sasa muelewe Rais anaposema tuko kwenye right track anamaanisha Nini.

Unaweza kuona nimetaja punje tuu ya mambo yaliyofanyika yenye lengo la kutufikisha mbali kiuchumi.

Fuatilia
Ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere
Ujenzi wa barabara
Uwekezaji kwenye madini
Ununuzi wa meli na vivuko

#2020 kura yangu kwa John
Thread nyingine ya udaku unaandika lini ?
 
Back
Top Bottom