Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

Udhaifu wake ni upi mkuu?
Mbona unasema uongo kwa hii comment yako hapa chini na zingine zilizotangulia:

Mafanikio makubwa yanagharama zake. Mwaka huu mshahara umeongezwa.
Kuhusu ajira ni lazima ujue haiwezekani kila mtu akaajiriqa na serikali. Serikali inatengeneza mazingira mazuri kupitia PPP na huko ajira rasmi na zisizo rasmi hutokea.
Ajira za walimu zimetangazwa. Najua bado eneo hilo lina changamoto ila tutafika pazuri zaidi
 
Mbona unasema uongo kwa hii comment yako hapa chini na zingine zilizotangulia:

Mafanikio makubwa yanagharama zake. Mwaka huu mshahara umeongezwa.
Kuhusu ajira ni lazima ujue haiwezekani kila mtu akaajiriqa na serikali. Serikali inatengeneza mazingira mazuri kupitia PPP na huko ajira rasmi na zisizo rasmi hutokea.
Ajira za walimu zimetangazwa. Najua bado eneo hilo lina changamoto ila tutafika pazuri zaidi
Onesha uongo ulipo
 
Watu waliozoea kishu ujima wa kuishi kwenye mapango utawajua tu.
Mtatoka lini huko?
Mkuu mjima ni yule anayewanyima watoto wake chakula eti anajenga nyumba.Huna sababu ya kuwabana wanao,tafuta tu kuongeza kipato,kipato kikiongeza utajenga tu tena ukiwa unaenjoy maisha
 
Mkuu mjima ni yule anayewanyima watoto wake chakula eti anajenga nyumba.Huna sababu ya kuwabana wanao,tafuta tu kuongeza kipato,kipato kikiongeza utajenga tu tena ukiwa unaenjoy maisha
Ukiishi bure, kusali kila siku bahati ikudondokee ili uishi vizuri na ulishe watoto wako, utakufa masikini na heri usingezaa mzigo huo wa watoto.
Jitahidi uishi na wakati na usiwe mtumwa wa matatizo yako.
Hakuna mtu atakayetokea kutatua matatizo yako binafsi, ila wewe mwenyewe.
 
Salamu kwenu,

Kumekuwa na kelele nyingi kuwa ndege zetu hazina maana yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Watu wanaenda mbali zaidi kuhoji ikiwa flyovers za Dar es Salaam zina umuhimu wowote kwa watanzania waishio vijijini, mikoani huko.

Ukiangalia hizi hoja, unapata picha mbili. Ya kwanza ni kuwa ni kweli hawajui umuhimu wake na picha ya pili ni kuwa wanajua ila wameamua kupotosha. Picha zote mbili zinao wahusika, yaani wapo wasiojua na wapo wanaojua ila wameamua kupotosha. Kwa faida ya wote tuchambue kama ifuatavyo:

Utangulizi
Kujenga uchumi imara sio kazi rahisi. Ni kazi inayohitaji weledi na uwekezaji janja (smart investment) pamoja na mazingira wezeshi kiuchumi. Kufikia uchumi mzuri sio kazi ya muda mfupi ingawa matokeo chanya yanaweza kuonekana ndani ya muda mfupi Kama miaka mitano hivi. Haya yanakuwa ni viashiria kuwa tupo kwenye mstari sahihi (right track).

Kwanini watu huona kuwa flyovers na ndege haziwasaidii chochote?
Wanadamu tuna asili flani ya ubinafsi. Unataka uone wewe Kama wewe umefaidikaje. Aidha ukiacha ubinafsi, Ni kweli kuwa kwa macho ya kawaida, mfanyakazi atataka kuona mshahara mnono, mkulima atataka pembejeo, barabara ya uhakika ya kusafirisha mazao yake na soko la uhakika. Mwanafunzi atataka elimu Bora, vifaa vya kujifunzia na mazingira bora ya kujisomea. Watu wanataka huduma bora za afya kwa kuwa na vituo vya afya karibu yao, hospitali nzuri zenye vifaa na wataalamu wa kutosha. Hivyo matarajio yao Ni hivyo vitu kutimizea, na kwa hakika hivyo ndivyo serikali inapaswa kufanya.

Kwanini flyovers na ndege ni muhimu kwa watanzania wote hata kwa wale waishio nje ya Dar es Salaam na vijijini?

1. Flyovers
Dar es Salaam ni mji wa kibiashara na ndio mji wenye watu wengi zaidi Tanzania. Dar es Salaam ndio mji iliko hospitali ya taifa. Kila siku maelfu ya magari huongia Dar es Salaam kuleta wafanyabiashara wa ndani na nje, wagonjwa walioshindikana huko mikoani, watalii hasa wa ndani na bidhaa za mashambani.

Unapokuwa na msongamano mkubwa barabarani ni kuwa unapoteza muda mrefu kupeleka bidhaa sokoni, mgonjwa hospitalini na kuwahi kazini kwaajili ya kuwahudumia watanzania. Unapoondoa kero hiyo unakuwa hujamsaidia tuu mtu aishiye Dar Bali umemsaidia mkulima aliyeleta mazao yake manzese au kariakoo aharikishe biashara yake, mgonjwa aliyetoka mkoani kuwahi hospitali na mfanyakazi kuwahi kazini. Hapa utaokoa gharama za mafuta, muda na maisha ya mgonjwa. Pia utaongeza vivutio vya utalii na kupendezesha mji.

Ndege
Ndege zinarahisha usafiri wa ndani ya nchi. Unafika popote nchini ndani ya muda mfupi. Bibi akiumwa na kuzidiwa kule ikungi, mnachangishana anaenda sehemu ndege inapotua, huyoo anawahishwa hospitalini.

Uwepo wa usafiri wa ndani was uhakika unawafahya watalii waongezeke na hivyo Kukuza pato la taifa. Kuwa na ndege yenu (national carrier) inayofanya safari za nje inachangia sana kuongeza pato la taifa kwani watalii watalipa nauli jwa fedha za kigeni ambazo zitaingia Tanzania na watalipa fedha za kigeni wanapoingia hapa kufanya utalii. Hiyo itakuza ajira nchini kwa waongoza watalii, madereva, wenye hoteli, migahawa na orodha inaendelea.

Mazingira hayo yanatengeneza kipato cha uhakika ambacho kitakuwezesha kulipa watumishi mishahara mizuri zaidi, kujenga shule nyingi zaidi zenye ubora, hospitali zenye ubora zaidi, kutoa ruzuku kwa wakulima na orodha inaendelea.

Hongera Rais Magufuli kwa kufanya uwekezaji janja, hongera CCM, hongera Tanzania. Msioelewa sasa muelewe Rais anaposema tuko kwenye right track anamaanisha Nini.

Unaweza kuona nimetaja punje tuu ya mambo yaliyofanyika yenye lengo la kutufikisha mbali kiuchumi.

Fuatilia
Ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere
Ujenzi wa barabara
Uwekezaji kwenye madini
Ununuzi wa meli na vivuko

#2020 kura yangu kwa John
Hizo ndege zimenunukiwa kwa kufuata open tender process kama inavyotakiwa kwenye manunuzi ya kiserikali?

Gharama zilizotumika kuzinunua ni zipi?

Gharama hizo zitarudiahwa lini?

Ndege zinajiendesha kwa faida au hasara?

Kulikuwa na ulazima gani wa serikali kujiingiza katika biashara ya ndege wakati sekta binafsi ilikuwa inatoa huduma hii kwa ufanisi?

Toka serikali ijiingize kwenye biashara ya ndege, nauli za safari za ndege zimepanda au zimeshuka?
 
Ukiishi bure, kusali kila siku bahati ikudondokee ili uishi vizuri na ulishe watoto wako, utakufa masikini na heri usingezaa mzigo huo wa watoto.
Jitahidi uishi na wakati na usiwe mtumwa wa matatizo yako.
Hakuna mtu atakayetokea kutatua matatizo yako binafsi, ila wewe mwenyewe.
Kwa hiyo kwa akili yako unadhani kazi ya kina Magu ni kukusanya Kodi zetu,Kisha kujilipa marupurupu na mishahara minono basi,kwamba madaraka yao hayana connection na umasikini wetu siyo mkuu?
 
Nimegundua mleta mada unapenda mwonekano wa vitu vya juu bila kujua athari ya wanayopitia watu wa chini.

Hayo yote yangekua na maana kama yangeenda sambamba na vipato vya wananchi.

Mfumo wa kodi zetu sasa umekua kandamizi kiasi cha kwamba watu wanaofikiria kuanza biashara kujifikiria mara mbilimbili
 
Hizo ndege zimenunukiwa kwa kufuata open tender process kama inavyotakiwa kwenye manunuzi ya kiserikali?

Gharama zilizotumika kuzinunua ni zipi?

Gharama hizo zitarudiahwa lini?

Ndege zinajiendesha kwa faida au hasara?

Kulikuwa na ulazima gani wa serikali kujiingiza katika biashara ya ndege wakati sekta binafsi ilikuwa inatoa huduma hii kwa ufanisi?

Toka serikali ijiingize kwenye biashara ya ndege, nauli za safari za ndege zimepanda au zimeshuka?
Kama hupandi ndege huoni umuhimu wake.
Kitu lingine, ambao hamsafiri mnaona hata barabara zinazojengwa ni bure
 
mkuu umeandika vizuri tu mfano ujenzi wa bwawa mwl nyerere sawa , hata miradi mingine ulio itaja ni sawa ila elewa kama nchi maskin ipo miradi kati ya miradi ulioitaja haikutakiwa kwenda kwa kasi na kufanya watu kuishi kama watumwa kwa kusosa mzunguko wa fedha katika jamii , kupanga ni kuchagua, lazima ilitupasa kufanya miradi ambayo ikiendelea pasiwepo wananchi kufunga mikanda ,na hii ndo hoja kuu ya watanzania na sio kila kitu lazima kimalizike kwa miaka mitano, taifa hili lipo na lilikuepo na litaendelea kuwepo, so watu wanazungumzia sana ndege sio kwamaba sio muhim lakini wanalinganisha tu kwamba mfano tangu ndege zimenunuliwa na chango wake katika uchumi linganisha may be na utalii kipi kimeongeza sana katika pato la taifa?
Na je kweli kama nikuinua shirika letu la ndege ambalo ni jambo zuri why hatukuanaza nunua ha ndege hata tatu kwanza huku tukiendelea jipanga ?
kuhusu bwawa sina shida kabisa
kuhusu barabara sina shida sana hapo maana kila awamu imekua ikijitahidi but jk aliyajenga sana tunashukuru sana kwa hili maana pia zachangia sana kwenye uchumi wa serikali.
mwisho
mada yako nzuri but yaitaji mjadala mpana sana mkuu


Kipimo Cha maendeleo Ni kipato/ Cha mtu mojamoja,,matumizi ya rasmiamali( uvuvi,utalii,madini), miundo mbinu, Ajira/mitaji nguvu au pesa na techonojia, Pato la taifa.....

1, hakuna ajira sio Mwl. Dr, hakuna mitaji... Hapo ajira Ni labda itakavyua.
2.khs kipato.... Vyuma vimekaza...
3. Hizo asilimali wanakula wachache...
4... Ktk miundo mbinu tuwe na Subira...
5. Ktk techonojia hapo hamna kitu... Kama Ile formula ya Madagascar ya covd59 ili feli unategemea nn...

Uchumi
Sio tu kubana pesa pia unatumiaje.. inflation, pricing, utilazation of labour, inter trade, natural resources Ni vitu vya kuzingatia sio kujenga Jenga tu....
 
Yani unajua mimi mwenyewe nashangaa sana hivi huduma muhimu ambazo ni za lazima kama Afya, barabara n.k unazifanyaje kuwa za kisiasa?

Malaysia ni kosa mwanasiasa kufanya hizi siasa sijui nitajenga barabara au kituo cha afya

Kwani hizo pesa Ni mapato ya Tra, ushuru na fani/tozo.... Kwahiyo walitaka hayo makusanyo yafanyiwe nn au yapo kwaajiri ya nn....
 
Fursakibao

Barabara zimejengwa tokea enzi ya mkoloni... Labda ukaulize Familia ya Sokoine enzi hizo ilikuaje...
Hayo Ni matusi kuita watu mafirauni na wakati wanalipa Kodi halali...
 
Kwa hiyo kwa akili yako unadhani kazi ya kina Magu ni kukusanya Kodi zetu,Kisha kujilipa marupurupu na mishahara minono basi,kwamba madaraka yao hayana connection na umasikini wetu siyo mkuu?
Magufuli hatakubadilisha kama wewe mwenyewe hutabadilika.
Hakuna mtu anabadilishwa na watu, anajibadilisha mwenyewe.
Kuna watu wanapata pesa ya kutosha, wanazilewea na kula starehe za kufa mtu.
Anakumbuka kujenga ana mitoto mitano ambayo hata kusomesha ni shida, hajajenga na sana sana ana Brevis kali.
Watu kama hao wapo na wanalaumu toka Mwinyi, Mkapa,Kikwetu hadi sasa Magufuli.
Na hata akipata urais mtu wa upinzani wataendelea kuwa masikini wa fikra na kimaisha.
 
Back
Top Bottom