Je, ni kweli Hayati Magufuli alihusika katika kuandaa kesi ya ugaidi ya Mbowe? Ilikuwa kwa lengo lipi?

Je, ni kweli Hayati Magufuli alihusika katika kuandaa kesi ya ugaidi ya Mbowe? Ilikuwa kwa lengo lipi?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari JF, binafsi huwa nakuwa na shaka sana na upinzani wa Mwenyekiti wangu Mbowe.

Kuna muda huwa napata mawazo ni mtu aliyewekwa kimkakati kuhakikisha CCM haitoki madarakani.

Nimekaa nimejiuliza sana, je, Kesi ya Mbowe ilianza kusikilizwa kwa benefits au faida kwa Awamu ya Tano au Sita au Wananchi?

Ilifunguliwa kwe lengo gani? Maana kwa Awamu ya Tano Mbowe alinyamazishwa na akanyamaza tofauti na Tundu Lissu.

Ushahidi ulikuwepo hata kabla uchaguzi 2020, ni Kesi yenye shutuma nzito vile, kwanini haikufunguliwa mapema ikichukuliwa ingeidhoofisha CHADEMA uchaguzi 2020?

Kwa haya mazingira ni kweli serikali ya awamu ya Tano ilihusika na ilikuwa kwa lengo lipi? Au ndio ulikuwa mwanzo wa kinachoitwa sasa ni Maridhiano?
 
Baada ya uchaguzi wa 2020, Mwendazake alidhamiria kuiangamiza CDM kabisa. Baada ya mbinu ya kununua wapinzani kuto kuleta matunda yaliyotarajiwa na ugumu alioupata kwenye campaign za 2020 na kwa jinsi Lissu alivyo mkalia kooni na kumpelekesha kwenye campaign dhamira yake ilikuwa kumaliza game kwa kuua yeyote ambaye alionekana hatari au kuwafungilia kesi za ugaidi ili waozee gerezani.

Utakumbuka pia Mwendazake alitaka kubadili katiba ili agombee tena 2025...hivyo alikuwa hataki kabisa kelele wakati wa mchakato wa mabadiliko ya katiba.
 
Never your contention is not correct! Mbowe was not silenced, he was only not vocal like Lisu and even today Mbowe is not vocal, he is a slower mover contrary to Lisu!
Sio kweli
 
Nyie kila mipango yenu ikifeli,mnamsingizia Magufuli.

Ila Magufuli huyo huyo ndiye aliyeifanya ccm ianze walau kukubalika kwa wananchi.nakumbuka wakati wa kikwete ilifikia point mtu ukionekana umevaa linguo la kijani mtaani watu wanakuzomea,huyu mwamba wa lake zone ndiye akaja kurekebisha mambo.

Na sasa tunakoelekea ni kule kule kwa enzi za kikwete.
 
Habari JF ,binafsi huwa nakuwa na Shaka sana na upinzani wa Mwenyekiti wangu mbowe

Kuna muda huwa napata mawazo ni mtu aliyewekwa kimkakati kuhakikisha CCM haitoki madarakani...
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani anawezaje kufunguliwa kesi ya uhaini kipindi cha uchaguzi mbele ya jumuia ya kimataifa?

Uliona Lisu alivyokolewa na wazungu mara baada ya uchaguzi?

Kushirikiana na CCM kwa Mbowe ni kuvunjiwa biasharan na account zake zote, kufungwa jela na kufunguliwa kesi ya uhaini.

Spare us
 
Nyie kila mipango yenu ikifeli,mnamsingizia Magufuli...
Hakika ilikuwa vile. Sijui sasa kwa Mama itakwenda kuwa vipi !! Tunamsubiri Queen of philosopher atuvushe !! Tunataka maridhiano pande zote.
 
Sijui wale police walioshirikiana na jamaa kumtesa Mbowe wanajisikiaje SAsa hivi Mbowe alivyo juu.

Unamtesa mtu ambae hata ustaafu pensheni YAKO hata ukiuuzwa na wewe ufikii hata robo ya mapato yake.

Acheni ujinga hii Dunia ikanyage polepole.

Leo wanaona aibu.

Pana siku Kova kova baada ya kustaafu alimkimbia Gwajima supermarket akikumbuka alipokuwa akimsotesha kabla ajastaafu.
 
Tulisema wote waliotamani upinzani ufe watakufaa wao upinzani ungali imara. Bashiru, ndugu, bashite, heri james, kingai, mroto, hata sijui walipotelea wapi. Mambosasa hakuwa na shida sema hakuwa na jinsi kama mateka.

Huwezi ukashindana na nature ukashindana.
 
Never, your contention is not correct! Mbowe was not silenced, he was only not vocal like Lisu and even today Mbowe is not vocal, he is a slow mover contrary to Lisu!
In other words. Mbowe ana busara na si mropokaji.

Sijawahi msikia Mbowe akimtusi mpinzani wake yeyote hata akiwa amepiga Faru John. Tofauti na yule Mbelgiji - yule wanaendana na Mdude.
 
Habari JF ,binafsi huwa nakuwa na Shaka sana na upinzani wa Mwenyekiti wangu mbowe

Kuna muda huwa napata mawazo ni mtu aliyewekwa kimkakati kuhakikisha CCM haitoki madarakani...
Kama hujuma, udhalimu na ufedhuli mkubwa ulifanyika katika vitega uchumi vyake, katika akaunti zake binafsi, kwa wafuasi, wanachama na viongozi wa chama chake, nini ambacho kilishindikana katika kufanya maandalizi ya kesi ile ya mchongo?

Moderators, tunaomba nyuzi zote zenye kumuhusu hayati huyu ziunganishwe katika uzi mmoja tu, pengine ambao upewe kichwa kinachosemeka kama;

"Mazuri na mabaya yaliyofanyika katika utawala wa awamu ya tano"

Ili kama mtu atajisikia kuupitia, aende humo kwa wakati wake, na siyo kama ilivyokuwa hivi sasa nyuzi nyingi zinakuja kwa vichwa vya habari tofauti lakini "the bottomline" ni kwamba kuna mazuri na mabaya yaliyoambatana na utawala wake.

Hayati kafa na matendo yake mengi ya jinai yaliyoambatana na utawala wake, lakini pia anawiwa na madeni kupitia madai mengi dhidi yake. Ukweli ni lazima usemwe, na kama ambavyo yeye mwenyewe alipenda kusisitiza, msema kweli ni mpenzi wa Mungu, hii kwa kuwa ukweli utatuacha huru, utawala wake ulikuwa ni wa kibabe, kidikteta, na ulitamalaki kila aina ya uovu.
 
Habari JF ,binafsi huwa nakuwa na Shaka sana na upinzani wa Mwenyekiti wangu mbowe

Kuna muda huwa napata mawazo ni mtu aliyewekwa kimkakati kuhakikisha CCM haitoki madarakani....
Wewe unamzungumzia Mbowe huyo anayelewa na kusingizia kapigwa na watu wasiojulikana,Kamanda Nnayemkubali kwenye Upinzani wa kweli wa Taifa hili alimuwaga Augustine Lyatonga Mrema (RIP) Na Pro.

Ibrahim Lipumba aliyepigwa na kuvunjika Mkono, hawa wengine ata wakitiwa tairi shingoni au Fungwa jiwe tumbukizwa baharini hakuna shida.
 
Habari JF ,binafsi huwa nakuwa na Shaka sana na upinzani wa Mwenyekiti wangu mbowe

Kuna muda huwa napata mawazo ni mtu aliyewekwa kimkakati kuhakikisha CCM haitoki madarakani...
Modus operand za serikali za kidikiteta,huwa zinafanana,
Zuia mawazo binafsi,bana vyombo vya habari,ua wapinzani,funga wapinzani,wazungu wanaita attach on descent.

Ilitokea Kenya, kipindi Cha Kenyata na Jaramongi Odinga,inatokea Uganda, kati ya museven na kiiza besigye,sio jambo geni, kwa wapinzani kuuliwa,kufungwa,kutengenezewa kesicza kisiasa, Ili wasiongee na kuleta.

Awakening kwa raia inavyoweza kuzaa mass protest.

Rejea kilichotokea nchi za kiarab, Arab spring, mpaka madikiteta kadhaa wakaangushwa.

CCM ya Maghu ilimuogopa Mbowe na upinzani, ilitaka ifsnye wizi bila kusemwa, ikabidi Mbowe apewe kesi, afungwe, Ili kuzima vuguvugu la ukombozi wa raia.

Hii Haina tofsuti na kinachotokea Uganda,Mseveni na kiiza besigye
 
Wewe unamzungumzia mbowe huyo anayelewa na kusingizia kapigwa na watu wasiojulikana,Kamanda Nnayemkubali kwenye Upinzani wa kweli wa Taifa hili alimuwaga Augustine Lyatonga Mrema (RIP) Na Pro.Ibrahim Lipumba aliyepigwa na kuvunjika Mkono.....hawa wengine ata wakitiwa tairi shingoni au Fungwa jiwe tumbukizwa baharini hakuna shida.
Wakati Mrema anapigwa mabomu hadi Nyerere akakataza hukuwepo?
Maumivu yakizidi wahi Chato, nafasi za makaburi bado zipo,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom