Kama hujuma, udhalimu na ufedhuli mkubwa ulifanyika katika vitega uchumi vyake, katika akaunti zake binafsi, kwa wafuasi, wanachama na viongozi wa chama chake, nini ambacho kilishindikana katika kufanya maandalizi ya kesi ile ya mchongo?
Moderators, tunaomba nyuzi zote zenye kumuhusu hayati huyu ziunganishwe katika uzi mmoja tu, pengine ambao upewe kichwa kinachosemeka kama;
"Mazuri na mabaya yaliyofanyika katika utawala wa awamu ya tano"
Ili kama mtu atajisikia kuupitia, aende humo kwa wakati wake, na siyo kama ilivyokuwa hivi sasa nyuzi nyingi zinakuja kwa vichwa vya habari tofauti lakini "the bottomline" ni kwamba kuna mazuri na mabaya yaliyoambatana na utawala wake.
Hayati kafa na matendo yake mengi ya jinai yaliyoambatana na utawala wake, lakini pia anawiwa na madeni kupitia madai mengi dhidi yake. Ukweli ni lazima usemwe, na kama ambavyo yeye mwenyewe alipenda kusisitiza, msema kweli ni mpenzi wa Mungu, hii kwa kuwa ukweli utatuacha huru, utawala wake ulikuwa ni wa kibabe, kidikteta, na ulitamalaki kila aina ya uovu.