Je, ni kweli Idd Amini alikuwa shujaa wa Afrika, Nyerere alitumiwa na wazungu kumchafua?

Waambie Waganda vizazi vya leo ambao wananyanyaswa na viwanda na maduka ya wahindi, uone kama hautatolewa nduki.....
Nyerere alikosea sana kumchokonoa Amin.
Amini hajawahi kua mtu wa maana tusidanganyane hapa! hakuna tofauti yake na M7
 
Hueleweki
 
Anaitwa ALHAJJ IDD AMIN DADAA,ALLAH AMWEKE MAHALA PEMA PEPONI,JEMEDARI WA VITA HUYO
 
Hakuna uchonganishi wowote hapo, idi amini alilewa madaraka akafanya aliyofanya ikiwemo kuvamia ardhi ya Tanzania , kumbukumbu zipo hivyo sio vizuri kupindisha historia
 
Nduli, joka kuu, kumbe nawe sawa na yeye. Ungejua watz wa wakati huo alivyowasababishia usumbufu usingesema hivyo. Inabidi upimwe damu ya uraia wako.
 
Wazungu wameendelea kutuchezea hado leo hii braza, na ni mbaya zaidi. Tangu enzi za harakati na kabla ya hapo, tumechezewa sana, na hadi leo ni yaleyale. Na mataifa mengine yanafuata nyayo zile zile. Sasa hivi Mwarabu nae keshachomoa mikucha yake .... kama zamani. Sasa sie na werevu wote hatujaweza chomoa ... kama kina WAHUNI walipotezea kupatikana kwa RAIS bora awamu ile, na mwenye vinasaba vya huko, kwani uzalendo wake ulikua na shaka? Hapana! Je kuibuka kwa mapandikizi yenye vinasaba na mataifa mengine ni MBINU za kimkakati ? Tusubirie na wa Kihindi au kabla ya hapo yule wa KICHINA. Kiafrika bana???
 
unaweza kumlaumu idd Amin lakini pia usimlaumu. Alichokosea Amin ni kujaa kwenye mtego wa obote. Amin alimtoa madarakani obote , obote akakimbilia tanganyika , huku tanganyika kukawa na mipango ya namna ya kumlejesha obote madarakani , amini alipoliona Hilo akachukua shortcut ambayo ikawa ni fursa kwa obote kwa upande wake , na hasara kwa tanganyika.

Ile Vita ilitakiwa iishie kagera tu , hakukuwa na sababu kuingia Hadi Uganda. hasara tuliyoipata ni kubwa mno , wageni wengi waliikimbia nchi , uchumi ukayumba , yaani tabu tunazopitia miaka hii ya kiuchumi asilimia 90 ni matokeo ya ile Vita ya Uganda.
 
Alipambanishwa
Nope!
Hivi ukigombana na mke wako na baadaye ukasikia jirani yako amempa room mkeo katika nyumba yake, hivi utafanyaje?
Sifahamu kama unajua ugomvi wa Milton Obote na Nduli Idi Amin Dada?
Hivi Obote alipopinduliwa na Idi Amin mwaka 1971 alikimbilia nchi gani?
 
Tz
 
Nduli, joka kuu, kumbe nawe sawa na yeye. Ungejua watz wa wakati huo alivyowasababishia usumbufu usingesema hivyo. Inabidi upimwe damu ya uraia wako.
Mpaka usiku, usiku wa manane, tutaandama usiku, usiku wa manane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…