Je, ni kweli kazi ya Serikali si kutengeneza ajira?

Je, ni kweli kazi ya Serikali si kutengeneza ajira?

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu kaika maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika katika Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 10 Januari, 2023

Amezungumzia mambo mengi lakini pia amegusia suala la ajira kwa vijana na kusema

"Nataka kuwaambia, kazi ya serikali si kutengeneza ajira, kazi yake ni kuweka mazingira mazuri ili vijana muyatumie kutengeneza ajira na hiyo kazi tunaifanya vya kutosha, naomba mkatengeneze ajira kwa mazingira yaliyokuwepo,"- Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa maoni yangu naona ni sahihi kwasababu kazi kubwa ya serikali ni kututengenezea mazira mazuri ya kufanya biashara au kuajiriwa na serikali imefanya juhudi hizo kupitia kufungua vyuo vya ufundi (VETA) nchi nzima kwaiyo kupitia elimu ya ufundi vijana wanaweza kujiari.
 
HAKIKA HIYO SIYO KAZI YA SERIKALI.

Serikali kazi yake ni kutoa huduma na kuhakikisha kuna miundombinu wezeshi kwa ajili ya kufanyika uwekezaji utakao zalisha ajira

Copy that.
Exactly sasa vijana wa Tanzania wanataka kupewa ajira mkononi yani amelala tu ndani apigiwe simu njoo ufannye kazi kitu ambacho sio kweli
 
Binafsi mpaka leo sijawahi pata maana halisi ya serikali, siku zote naona serikali zote ulimwenguni zipo kwa ajili ya kutia ugumu ktk maisha ya mwanadamu. Na dunia nzima mfumo wa serikali ni mmoja. Na hakuna kitu kinachoitwa serikali bali ni Mamlaka.

Kwamba huyu mwenye mamlaka yeye ndio ataandaa sheria ambazo hazitamhusu yeye, ( hichi fanya, hichi usifanye-huku yeye akifanya, atajitengenezea ukuta wa kujilinda yeye( wao wenye hiyo mamlaka ) na agenda zake/zao.

*Ardhi ni mali ya serikali
*Wewe mwenyewe ni mali ya serikali
*Utatakiwa ulipe kodi zote stahiki kwa serikali ( waita chombo ) japo ni watu. Yaani unaambiwa pesa inaenda serikalini ( unknown place ) sababu serikali haipo. Serikali ni kitu ambacho ki ukweli hakipo na badala yake kuna Mamlaka.

Sasa hii serikali isiyokuwepo huku ikiwepo ktk kivuli cha Mamlaka hapa ndipo panaponichanganya.

*Serikali ili ikamilike inatakiwa iwe na vitu vingapi?
*Serikali kamili ina watu wangapi?
*serikalini ni wapi?
*Serikali inaongozwa na misingi ipi?
*Msimamizi wa Serikali ni serikali yenyewe?

Kodi zetu lakini Mali ni za Serikali, na Mwisho Serikali haiwezi kukutaftia ajira sababu ni hiyo kwamba Serikali ki uhalisia haipo.

Njaa tu hii pengine nikishiba ntarudi ku edit
 
Hata pale ambapo Serikali inaajiri Lengo Ni Hilo hilo kuwezesha mazingira mazuri kwa watu kufanya shughuli zao na Kutoa Huduma tuu..

Kwenye ilani husema tutawesesha kutengeneza ajira rasmi kadhaa na zisizo rasmi kadhaa Ila yenyewe haiwezi tengeneza ajira maana injini ya Uchumi Ni private sector.
 
Binafsi mpaka leo sijawahi pata maana halisi ya serikali, siku zote naona serikali zote ulimwenguni zipo kwa ajili ya kutia ugumu ktk maisha ya mwanadamu. Na dunia nzima mfumo wa serikali ni mmoja. Na hakuna kitu kinachoitwa serikali bali ni Mamlaka.
Serikali Ni referee watu wasivuke mipaka na pia kazi kubwa ya serikali Ni Kuhakikisha ulinzi na usalama na Kutoa Huduma kwa kutumia Kodi zetu wenyewe
 
Serikali lazima itengeneze Sera nzuri za kutengeneza ajira... tulishuhudia awamu ya Tano ikiiona sekta binafsi kama threat kwake, ikaimaliza - hili lilikuwa ni kosa kubwa mno.

Nafikiri Mama Kaliona hilo na walau sasa hivi kuna ka mzunguko ka hela mtaani, mama ntilie anapika, fundi ujenzi wana kazi, fundi chelehani anashona, maduka ya ujenzi wanauza bidhaa, Bar walau zinauza uza na wahudumu wao nao afadhali kidogo, makampuni binafsi nayo pamoja na NGO zimetema ajira.

Mnyonge mnyongeni jmn, kuna ka kupumua kidogo - maana ilifikia hali kubwa mbaya mbaya.
 
Binafsi mpaka leo sijawahi pata maana halisi ya serikali, siku zote naona serikali zote ulimwenguni zipo kwa ajili ya kutia ugumu ktk maisha ya mwanadamu. Na dunia nzima mfumo wa serikali ni mmoja. Na hakuna kitu kinachoitwa serikali bali ni Mamlaka.

Img 3.jpg
 
Hata pale ambapo Serikali inaajiri Lengo Ni Hilo hilo kuwezesha mazingira mazuri kwa watu kufanya shughuli zao na Kutoa Huduma tuu..

Kwenye ilani husema tutawesesha kutengeneza ajira rasmi kadhaa na zisizo rasmi kadhaa Ila yenyewe haiwezi tengeneza ajira maana injini ya Uchumi Ni private sector.
Serikali itafanyaje kazi bila kuwa na watendaji kwenye ofisi zake?
 
Back
Top Bottom