Je, ni kweli kazi ya Serikali si kutengeneza ajira?

Je, ni kweli kazi ya Serikali si kutengeneza ajira?

Binafsi mpaka leo sijawahi pata maana halisi ya serikali, siku zote naona serikali zote ulimwenguni zipo kwa ajili ya kutia ugumu ktk maisha ya mwanadamu. Na dunia nzima mfumo wa serikali ni mmoja. Na hakuna kitu kinachoitwa serikali bali ni Mamlaka...
😆😆😆
 
Kazi ya serikali ni kutengeneza mazungira wezeshi ya watu wake kuajirika na kujiajiri. Sio lazima wala wajibu wa serikali kukuajiri.

Serikali au nchi yeyote ikiwa na nguvu kazi isiyotumika "untapped workforce" kama ilivyo sasa katika nchi nyingi ni hasara maana kunakuwa hakuna uzalishaji, lakini sio hasara inayoudhi au inayoleta sharti wala kukera. Ni juu ya serikali husika kujali hilo au kutojali.

Jitahidini vijana mtafute au mjitengezee ajira la sivyo mtazeeka na kufa huku mnailaumu serikali.
 
Ndio kazi ya serikali ni kutengeneza ajira (mazingira) , ila kutoa ajira sio kazi yake.
 
Hawa watu ni wajinga sana kila alisemalo rais hata kama ni pumba wao huja kupaka mafuta ili ionekane ni halali.

..Na kama Ssh ndiye mwenye fedha zote za miradi na matumizi ya kawaida ya serikali nini kinamzuia kutengeneza ajira?

..suala la serikali kutengeneza au kutokutengeneza ajira ni UAMUZI au SERA ya serikali au chama kilichoko madarakani.
 
Bila shaka katikati ya hotuba yake alitupia hii kitu kulainisha koo.
FB_IMG_16719808230659874.jpg
 
Kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuzalishwa kwa ajira bora.
 
Rais Samia Suluhu kaika maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika katika Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 10 Januari, 2023

Amezungumzia mambo mengi lakini pia amegusia suala la ajira kwa vijana na kusema

"Nataka kuwaambia, kazi ya serikali si kutengeneza ajira, kazi yake ni kuweka mazingira mazuri ili vijana muyatumie kutengeneza ajira na hiyo kazi tunaifanya vya kutosha, naomba mkatengeneze ajira kwa mazingira yaliyokuwepo,"- Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa maoni yangu naona ni sahihi kwasababu kazi kubwa ya serikali ni kututengenezea mazira mazuri ya kufanya biashara au kuajiriwa na serikali imefanya juhudi hizo kupitia kufungua vyuo vya ufundi (VETA) nchi nzima kwaiyo kupitia elimu ya ufundi vijana wanaweza kujiari.
Ndio ni kazi ya Serikali kutengeneza AJIRA.

Kama HUWEZI kutengeneza AJIRA achia MAMLAKA wanaoweza wafanye KAZI.
 
Rais Samia Suluhu kaika maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika katika Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 10 Januari, 2023

Amezungumzia mambo mengi lakini pia amegusia suala la ajira kwa vijana na kusema

"Nataka kuwaambia, kazi ya serikali si kutengeneza ajira, kazi yake ni kuweka mazingira mazuri ili vijana muyatumie kutengeneza ajira na hiyo kazi tunaifanya vya kutosha, naomba mkatengeneze ajira kwa mazingira yaliyokuwepo,"- Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa maoni yangu naona ni sahihi kwasababu kazi kubwa ya serikali ni kututengenezea mazira mazuri ya kufanya biashara au kuajiriwa na serikali imefanya juhudi hizo kupitia kufungua vyuo vya ufundi (VETA) nchi nzima kwaiyo kupitia elimu ya ufundi vijana wanaweza kujiari.
Samia anajikwepesha tu Jukumu la msingi hapa.

Mazingira na ajira vyote ni kazi ya msingi ya serikali. Asikwepe na kila siku lazima alale akijua hilo.
 
Back
Top Bottom