Serikali lazima itengeneze Sera nzuri za kutengeneza ajira... tulishuhudia awamu ya Tano ikiiona sekta binafsi kama threat kwake, ikaimaliza - hili lilikuwa ni kosa kubwa mno.
Nafikiri Mama Kaliona hilo na walau sasa hivi kuna ka mzunguko ka hela mtaani, mama ntilie anapika, fundi ujenzi wana kazi, fundi chelehani anashona, maduka ya ujenzi wanauza bidhaa, Bar walau zinauza uza na wahudumu wao nao afadhali kidogo, makampuni binafsi nayo pamoja na NGO zimetema ajira.
Mnyonge mnyongeni jmn, kuna ka kupumua kidogo - maana ilifikia hali kubwa mbaya mbaya.