Je, ni kweli kazi ya Serikali si kutengeneza ajira?

😆😆😆
 
Kazi ya serikali ni kutengeneza mazungira wezeshi ya watu wake kuajirika na kujiajiri. Sio lazima wala wajibu wa serikali kukuajiri.

Serikali au nchi yeyote ikiwa na nguvu kazi isiyotumika "untapped workforce" kama ilivyo sasa katika nchi nyingi ni hasara maana kunakuwa hakuna uzalishaji, lakini sio hasara inayoudhi au inayoleta sharti wala kukera. Ni juu ya serikali husika kujali hilo au kutojali.

Jitahidini vijana mtafute au mjitengezee ajira la sivyo mtazeeka na kufa huku mnailaumu serikali.
 
Ndio kazi ya serikali ni kutengeneza ajira (mazingira) , ila kutoa ajira sio kazi yake.
 
Hawa watu ni wajinga sana kila alisemalo rais hata kama ni pumba wao huja kupaka mafuta ili ionekane ni halali.

..Na kama Ssh ndiye mwenye fedha zote za miradi na matumizi ya kawaida ya serikali nini kinamzuia kutengeneza ajira?

..suala la serikali kutengeneza au kutokutengeneza ajira ni UAMUZI au SERA ya serikali au chama kilichoko madarakani.
 
Kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuzalishwa kwa ajira bora.
 
Ndio ni kazi ya Serikali kutengeneza AJIRA.

Kama HUWEZI kutengeneza AJIRA achia MAMLAKA wanaoweza wafanye KAZI.
 
Samia anajikwepesha tu Jukumu la msingi hapa.

Mazingira na ajira vyote ni kazi ya msingi ya serikali. Asikwepe na kila siku lazima alale akijua hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…