Je, ni kweli kazi ya Serikali si kutengeneza ajira?

Vijana wapewe elimu, ujuzi na maarifa ya kazi za mikono. Wazazi tuwape mitaji watoto wetu waanze kujishughulisha na uwekezaji mdogo mdogo
Kweli na ndio maana Serikali ya Rais Samia Suluhu inatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana ili waweze kujiajiri
 
Kweli kabisa kwa upande wa ajira Serikali ya Rais Samia Suluhu imejitahidi sana kutokomeza tatizo la ajira Tanzania kupitia miradi inayotekelezwa nchini wanaonufaika ni watanzania pia inatoa mikopo yenye mashart nafuu vilevile inawekeza katika kilimo na kuwapa vijana kipaumbele kupewa eneo mambo ni mengi sana aisee Rais Samia Suluhu tumpe hongera zake
 
Ni kweli? Kazi yake ni kutengeneza
Hapana sio kweli Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira ya kumuwezesha mwananchi kujiajiri maana haiwezekani Tanzania nzima tukaajiriwa na Serikali sio kweli kabisa
 
..wakati wa kampeni huwa wanasema serikali ya Ccm itatengeneza ajira.

..pia ikitokea kukawa na ajira nyingi husema Raisi au Mwenyekiti wa Ccm ametengeneza ajira.
Issue ni kwamba kuna asilimia kubwa ya watanzania ambao hawajaariwa serikalini na sio kila mtu ataajiriwa kwaiyo ili kuondoa tatizo la ajira Serikali inatengeneza mazingira wezeshi ya kujiajiri kwa wale wasiokuwa na ajira serikalini ndio maana unaona mikopo yenye masharti nafuu
 
Amekwepa jukumu!

Lini wameleta mtaala wa kujiajiri Ili vijana wawe na ujuzi wa kujiajiri!?

Vijana wanaandaliwa kuajiriwa halafu wanageuziwa kibao eti wajiajiri KWELI!???
Na ndio maana Serikali ya Rais Samia Suluhu imekuja na mpango wa kujenga vyuo vya veta nchi nzima lengo ni vijana tupate elimu ya ufundi na tuweze kujiajiri au kuajiriwa na kama unafatilia Rais Samia Suluhu alisema mtaala wa elimu ubadilishwe uwe ule unaomtengeneza muhitimu katika mazingira yote ya kuajiriwa na kujiajiri
 
Na ndio maana serikali ya Rais Samia Suluhu imeweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri na hakuna serikali kokote duniani inayoweza kuwaajiri wananchi wake wote watu inatakiwa waelewe hili suala
 
Wengine tulifanikiwa tukiwa hakuna hata mzazi mmoja kwenye system. Kwa hiyo sio kesi
Exactly haya mambo ni bahati tu ya kuajiriwa na wala sio system na kitu kingine serikali haiwezi kuajiri nchi nzima
 
Pote duniani moja ya kipengele kinachotumika kuangalia hali ya uchumi ni ongezeko au upunguaji wa ajira katika nchi. Ila sisi tuna vigezo vyetu tofauti ingawa hata darasani wachumi wetu wamefundishwa hivyo.
 
HAKIKA HIYO SIYO KAZI YA SERIKALI.

Serikali kazi yake ni kutoa huduma na kuhakikisha kuna miundombinu wezeshi kwa ajili ya kufanyika uwekezaji utakao zalisha ajira

Copy that.
Mbona hata Hilo bado selikal yetu ime shindwa?

Hakuna kitu ambacho taifa letu Lina kifanya kwa ufanisi kama ufisad na upigaji basi ndio tunaweza
 
Tatizo la Vijana wengi ni Uchawa ndio unaowasumbua; hii ni mbaya sana kwa ustawi wa taifa letu.
Yani vijana wanakubali kuwa mavuvuzela ya wanasiasa eti swala la ajira sio jukumu la serikali!
 
Sad reality.Serikali is just an imaginary thing
 

..hicho ambacho serikali inafanya au haifanyi matokeo yake ni tatizo kubwa la UKOSEFU WA AJIRA tunalolishuhudia hapa nchini.
 
Hii hoja ni controversial kulingana na unavyoweza kutafsiri but ukiangalia kwa jicho la Uchumi Ni sahihi , Serikali haitengenezi ajira Bali Ni facilitors wa kutengeneza ajira.
Kijamii inagoma. Serikali Ina wajibu... Mbaya zaidi inalaumu wahanga kwamba wanapenda mteremko, wanashinda vijiweni, KUBETI na kukataa kazi zingine. Hili ni tatizo la jamii, maelezo ya siasa yanatoa kwenye jamii na kulipeleka ngazi ya mtu mmojammoja. Hiv unajua kama daktari akipata kazi lakini ya umeneja wa bar bado tatizo lipo?
 
Ndio, inashirikiana na watu binafsi. Kwa upande wa serikali, kodi inayokusanya ndio malipo kwa wafanya kazi.
 
Bibi Kavurugwa,ni wajibu wa serikali kuhakikisha watu wake wanakuwa na kazi zenye staha.Kazi kuu za serikali Duniani ni KUWALINDA na KUWAENDELEZA watu wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…