Ni waziri ama naibu waziri?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Salama Aboud Talib (Waziri wa Nishati - SMZ) ashukiwa kuugua CORONA.
************************************************************************
Waziri wa Nishati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambae alikuwa safarini kutokea London (Uingereza 🇬🇧) na kupitia Italy 🇮🇹 kisha kurejea Zanzibar wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA...
Dr. Mkuu wa Hospitali ya mnazi mmoja baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya Mnazi mmoja akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Kidimni...
Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika... Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA 🦠...
Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda Kidimni, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya London kisha kupitia Italy na kurejea Zanzibar akiwa na homa kali!...
Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake...
Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine...
Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Wazanzibar wote!... Ameitaka SMZ kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari!...