Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Sasa mbona mnamficha wakati Uingereza waziri mkuu ametangazwa kabisa, miafrika aliyeturoga kafia zake mbali, huyo mkimficha hivyo ataambukiza wauguzi maskini wanaomhudumia kisha na wao wakaambukize wengine huko makwao.
 
"Waziri wa... ambaye alikuwa safarini akitua nchini kutokea London (Uingereza 🇬🇧) ambapo safari yake ilianzia Italy 🇮🇹 kisha kurejea wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya ... akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA."

Kuna mambo mengine ya ajabu sana... Alisafiri for what? Wanaficha for what? Anagoma kupitia process for what?

Hili gonjwa halina masikni wala tajiri, wenye vyeo au wasiokua navyo...

Pascal Mayalla kwa hizi taarifa na huu uzi usishangae ukashughulikiwa na mamlaka zote... hata zile zisizohusika...



Cc: mahondaw
 
Pascal Mayalla nakushauri futa huu uzi. Kama ulipokonyoka ktk line ya akina Kabendera hapa utanasa. Ni ushauri tuu maana umetafutiwa target muda mrefu.

USIMTISHE!

Pascal Mayalla ni taasisi, kama sio mhimili.

Huwezi kumlinganisha na Kabendera. Kabendera siku anakamatwa a massive majority of us had never heard of him. Kumfuatilia tukakuta ameandika kwenye gazeti la Ecomist kwamba January Makamba anatishia kuchukua nchi kwa vile amefanikisha zoezi la marufuku ya mifuko ya plastiki. Tukajua huyu Kabendera is small potatoes.

Pascal Mayalla ni namba nyingine, Mike Pompeo anamjua na John Pombe anamjua. Huwezi kumkamata Mayalla kiepesi epesi kama Kabendera!
 
Ni waziri ama naibu waziri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Salama Aboud Talib (Waziri wa Nishati - SMZ) ashukiwa kuugua CORONA.
************************************************************************
Waziri wa Nishati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambae alikuwa safarini kutokea London (Uingereza 🇬🇧) na kupitia Italy 🇮🇹 kisha kurejea Zanzibar wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA...

Dr. Mkuu wa Hospitali ya mnazi mmoja baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya Mnazi mmoja akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Kidimni...

Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika... Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA 🦠...

Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda Kidimni, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya London kisha kupitia Italy na kurejea Zanzibar akiwa na homa kali!...

Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake...

Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine...

Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Wazanzibar wote!... Ameitaka SMZ kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari!...
 
Back
Top Bottom