Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!


Mahmoud Thabit Kombo amekuwa waziri na ataendelea waziri si kwa sababu ana sifa za uongozi na diplomasia bali ni kwa sababu ya baba yake ni Mzee Thabit Kombo mmoja wa walokuwa mbele pamoja na Karume wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi, kwa ufupi hakuna atakaethubutu kumvua uwaziri hata iwe vipi, amevaa joho la baba yake.
 
Mahmoud Thabit Kombo amekuwa waziri na ataendelea waziri si kwa sababu ana sifa za uongozi na diplomasia bali ni kwa sababu ya baba yake ni Mzee Thabit Kombo mmoja wa walokuwa mbele pamoja na Karume wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi, kwa ufupi hakuna atakaethubutu kumvua uwaziri hata iwe vipi, amevaa joho la baba yake.

Kaondoka baba yake itakuwa yeye
 
ukweli kama unao ungeusema ili uwaokoe watanzania wengi, kwa kuficha ficha kwako hakuna tofauti na hao unaowashutumu kuhusu kusema ukweli..

JAMII TUNAIFUNZA NINI KWA ViTUKO VYA BAADHI YA WENYE DHAMANA YA UONGOZI SMZ
Ni matukio ya kuhuzunisha na kustaajabisha ya tabia za baadhi ya viongozi wetu hasa baadhi ya Mawaziri
wa SMZ kujifanya wao wapo juu ya sheria.
Namuonea huruma sana Mhe Dr Ali Mohamed Shein Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa upole wake na hulka yake na vituko vinavyofanywa na wasaidizi wake.
Mawaziri ni wasaidizi wa karibu wa Mhe Rais. Ikiwa Mawaziri ndio wanaoongoza kuvunja sheria za nchi na kuhatarisha uhai wa wananchi wetu sisi raia wa kawaida tufanyeje???
Nafikiri wanamlazimisha Mhe Rais achukue maamuzi magumu juu yao ili iwe fundisho kwa wengine.
Hivi karibuni kuna kigogo mmoja wa SMZ alikuwa ziarani barani Ulaya. Nasikia ilikuwa ziara binafsi baada ta kuchukua likizo. Likizo wakati nchi ilikuwa katika timbwili la mtafaruku wa ZAN ID na Daftari na huku Mjumbe wa Baraza la MapinduI anachukua likizo. Mbona Mhe Rais hajaenda likizo au sio binaadamu. Mnamuonea Rais wetu Shein kwasababu ni mpole. Muungwana na hapendi misuguano na misigano hasa na wasaidizi wake na hapo ndipo mnapochukulia pouwa tuu.
Kigogo huyu alikwenda Italy na Uengereza na kurejea nyumbani mnamo March 22 wakati wa asubuhi na Ndege ya QR.
Alipofika alitumia ukumbi wa watu mashuhuri VIP Uwanja wa Ndege wa Karume Zanzibar akiwa ba dalili tosha za mafua na baridi ya ulaya.
Kwa madaha na kujiamini alikataa ushauri wa mabwana afya waliopo uwanjani wa kuwa isolated kwa siku 14 na badala yake akaamua kwenda nyumbani kujipumzikia.
Wakati yuko nyumbani anaugua ndani ya nyumba ikawa ingia toka hamkani watu ndugu ma majirani kwenda kumjuilia hali kigogo huyo. Wakiwamo wafanyakazi wa UWT na baadhi ya watendaji wa CCM Kisiwandui.
Siku ya Alkhamis 26 March 2020 Kigogo akaanza kujisikia kuumwa zaidi na kuamua kukimbilia hospitalini. Hapo ndio mkasa ulianzia
1. Kigogo baada ya kufika kapokelewa na madaktari wa zamu na kuhudumiwa pamoja na kutolewa vipimo na kupelekwa maabara kwa uchunguzi.
2. Kosa kubwa lililofanyika Kigogo alilazwa wodi ya zamani ya wazazi Hospital ya Mnazi Mmoja tena amelazwa pamoja na watoto njiti na mama zao kwa siku tatu kuanzia hiyo Alkhamis 26 March 2020 hadi Jumamosi saa saba mchana 28 March 2020 alipochukuliwa kwa nguvu kupelekwa kwenye kambi.
3. Muda wote yuko hapo wodini na hao watoto njiti wagonjwa Kigogo huyo alikuwa mkaidi kuvaa mask ya kujikinga na pia kutulia kitandani alipowekwa. Alikuwa hatulii mara huku mara kule.
4. Baada ya kugundulila kigogo ameathirika bado alikuwa hataki kuondoka hapo Mnazi Mmoja na kurnda kambi ya waathirika hadi amri kutoka juu zilipoanza kumiminika ndio akaamua kwenda kwa nguvu.
5. Taarifa zilizopo ndani ya wodi hiyo kigogo huyo aliamua kulala na shioga yake hapo hapo kwa siku hizo na Uongozi wa hospital ya Mnazi Mmoja kukubali hali hiyo.
Sasa ikiwa Kiongozi mwenye dhamana kubwa katika nchi anafanya kama haya sisi wanyonge tufanyeje??? kiburi hiki kakitoa wapi???
Kuna maswali mengi ambayo Serikali na Uongozi wa Hospital ya Mnazi Mmoja watusaidie
1. Kwanini Kigogo huyu hakuwa monitored huko nyumbani kwake wakati amewekwa karantini ya siku 14 ili kujua mienendo ya matendo yake huko?
2. Kwanini Serikali au Hospital ya Mnazi Mmoja imempokea na kumuweka mtu mwenye risk kubwa ya Korona kwa kumchanganya wodi moja na watoto wadogo Mnazi Mmoja Hospital???
3. SMZ inatuambia nini kuhusu wale abiria aliokuja nao kigogo March 22 kutoka Doha na wote wameteremka Zanzibar jee wamewapata na kuwapima kama wapo salama??
4. Jee Wafanyakazi wa VIP Airport Zanzibar wamechunguzwa afya zao???
5. Dereva wa Kigogo na familia yake wameangaliwa??
6. Wafanyakazi wa CCM Kisiwandui na UWT walioenda kumkagua mgonjwa jee wapo salama??
7. Madaktari na manesi waliompokea siku ya Alkhamis Mnazi Mmoja hospital na kumhudumia kama mgonjwa wa mafua tuu kabla ya kubainika ana Korona jee wameshapimwa wao na familia zao???
8. Jee wale watoto njiti na Mama zao wapo salama na watu wanaokwrnda kuwatizama wagonjwa kuanzia Alkhamis hii hadi hii leo hee wapo salama na wanajulikana???
9. Jee Serikali imechukua hatua gani kama kufanya upigaji wa dawa kwa hospital ya Mnazi Mmoja hasa wodi na sehemu alizotembelea kigogo huyo badala ya kusubiri manusura ya Allah????
10. Mwisho kabisa jee Wahusika mnaona alivyofanya huyu kigogo ni sawa??? kuhatarisha afya za madaktari wetu tena wengine madaktari wa kigeni ambao wameshikwa na wahka kutokana na walivyokuwa karibu na mgonjwa pamoja na madaktari wenzao katika kutoa msaada kwa mgonjwa huyo.
Wizara ya Afya Waziri anajitahidi sana kutoa elimu na maelezo ya kutosha kwetu sisi wananchi.
Linaloshangaza kiongozi anajijua katoka safari katika nchi hatarishi na corona na bado anachukulia mchezo mchezo kama vile asife peke yake afe na wengi, hili si sawa kabisa.
Sisi wananchi hatukufundishi Dr Shein Rais wetu lakini hawa watu walikuwa wajiuzulu wenyewe wanaopindisha sheria za nchi yetu kwa ubinafsi wao. Lakini wanaonekana wamejawa na kibri na hawajijui kama hata wamekosea. Allah yuko radhi kwa kigogo kama huyu kumtumbia ili iwe fundisho kwa wengine. Ndio maana tunasikia mengi ya Mawaziri kupindisha sheria maana wengine wanapitisha ndugu na marafiki zao wanaotoka UK kupitia VIP kinyemela kukwepa kukaa siku 14 karantini. Hii si sahihi. Corona ni hatari lazima tuambizane ukweli.
Hivi kwa mfano huyu Kigogo aliewekwa katika wodi ya watoto na ana korona kwa uchache keshaambukiza wangapi???? au wangapi wapo katika hatari ya maambukizi???? Allah atunusuru lakini faida na hasara ya ukaidi wake tutaanza kuiona ndani au baada ya siku 10 zojazo kuanzia leo.
Hatari lakini salama Allah atuhifadhi ja shari hii.
Wenu
Kubwa Lijalo
Ziwatuwe
Zanzibar
 
*MAWAZIRI WETU SMZ BAADHI YENU KWANINI MNAKUA HIVI.*

Inasikitisha sana baada kuisikia na kuipata taarifa hii.
Jana tulisikia jinsi waziri alotoka safari na kuingia hapa kupitia VIP na kukaa Nyumbani akiwa anaumwa na kupelekwa Hosptl ya mnazi mmoja na mwishoe kuishia Kidimni.

Baada ya hili kutokea Purukuchu unapata taarifa za kuaminika Waziri mwengine wa SMZ kayafanya mengine yanayofanana na yale yale.

Kuna mgeni kaingia kutoka Uengereza mgeni wa kike kuna waziri wakiume kaenda uwanja wa ndege kumpokea mgeni uyo na kumpitisha VIP wakati hana hadhi ya kupitia VIP mtu huyo.

lakusikitisha VIP nao kwakua kapitishwa na waziri wakamruhusu na baadala ya kumuandika kaingia wakamuandika katoka baada ya apo akapelekwe kwa maofisa wa immigration Nao wakataka taarifa zake anapokwenda Akaandikwa anakwenda Bububu.

matokeo yake mtu huyo kapelekwa Chukwani Nyumbani kwao. Shida mwanamke baada ya kupitishwa kwamsaada wa waziri akaanza kuwataarifu wenzie walipo ulaya kama kishapita na yupo Nyumbani anafanya shuhuli zake.

Watu wa ulaya ndio walotoa taarifa znz ya hayo yote yalotokea huku hapo ndio taarifa zikaenea mpaka kufika maeneo husika na kufatiliwa uyo mtu na kupatikanwa Chukwani.

Tumuombe mungu awe hana maambukizi je kama atakua nayo nani hasa wakumlaumu kwenye hili?

Kwann tunaowapa dhamana na kuwaamini kwenye hili wanatuangusha haliyakua yote wameyapanga wao watu wakija wafikie wapi na Siku ngapi au Amri hii kwetu sisi tu wenye uluwa haiwahusi.

Hivi kwann mtu hajiambii ikiwa Makamo wa pili wa Raisi wetu Ambae ni mtendaji Mkuu wa shuhuli za serekali na mkewake na watumishi wake wote alokua Nao safari wamezingatia hili na kutii Amri ya Serekali. inakuwaje mtu tu wakawaidi waziri anajitwisha kumpitisha tu Jaman mnalengo gani na sisi tunaoishi humu visiwani?

Inakuwaje mnajipangia mikakati mnashidwa kuitekeleza wenyewe serekali kupitia vikosi vya ulinzi na Salama havilali kwa kulinda mipaka ili watu wasipitishe Kumbe nyie mnawapitishia kwa VIP kuna haja gani ya kuwafanya wasialale majumbani kwao kwa kulinda Taifa.

kwakweli inasikitisha sana Tunaowaamini na kuwaheshim ndio wanaotuhatarishia Maisha yetu haya mkuu ila kwasasa mgeni alopokea kisha chukuliwa yupo KAMILA tuombe mungu awe mzima ili ndugu zetu waokoke Ukanda wa chukwani.
Huyu mama kwa kweli amefanya kitu cha kizembe kweli. Hapo nasikia kashamuambukiza mwanawe, na kuna watu kama 70 ivi ambao amekutana nao wapo kwenye hatari ya kuwa na ivo virusi. Halafu anasema hana hadhi ya kwenda kidimni? Ana hadhi ya kwenda wapi?

Huyu akipona, apokonywe vyeo vyote kwa kuonesha dharau. Hospitali zimejengwa na Serikali yake mwenyewe halafu anasema hana hadhi ya kwenda kule kisa yeye ni waziri? Kwao kwa wanyonge wanawaekea spitali shaghala baghala kwa viongozi wakatibiwe nje?

Huu ugonjwa si bure, ni adhabu. Sasa ata aumwe rais, atatibiwa hapa hapa nchini mana hakuna nchi itakayopokea mgonjwa wa corona kutoka taifa jengine. Sasa ndio wataona umuhimu wa kuboresha sekta za afya na kuhakikisha hospital zinavifaa vya kutosha!
 
Back
Top Bottom