ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kolo ni.kolo aisee 😀😀Wewe hujui kuwa alizeti haihitaji mvua, ni zao linalolimwa sehemu zenye ukame. Hivi wewe mwananjombe shule ipo kweli?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kolo ni.kolo aisee 😀😀Wewe hujui kuwa alizeti haihitaji mvua, ni zao linalolimwa sehemu zenye ukame. Hivi wewe mwananjombe shule ipo kweli?
Umekwama sana kolo wa njombe.Kolo ni.kolo aisee 😀😀
Mwanza kuna flyover?Ngoja na mimi nichangie kidogo hapa;
Mm nipo Dodoma toka 2017, Dom ilikuwa na watu wengi sana wanaojihusisha na masuala ya ujenzi mda huo nyumba nyingi sana zimejengwa, Ilazo, Swaswa, Nzuguni, Meriwa, Kisasa, Iyumbu, Mkonze pia Michese (hii ni mitaa mipya kabisa tulioijenga sisi, ikumbukwe mm n mkandarasi)
Kabla ya hapo mitaa iliyokuwa na watu ilikuwa ni Nkuhungu, Maili 1 & 2, Majengo, Changombe(kwa warangi), kuna mtaa umenitoka ila ni karibu na CBE zilipo ofisi za mapasi naona siku hiz uongozi wa mji wamevunja wanampango wa kuweka bustani, pia kulikuwa na vijumba kidogo juu ya station ya TRC kama unaenda Ntyuka mitaa ya Pestana
Ipo hivi Dodoma imejenga sana kuliko Mwanza kwa kipindi hiki hakuna ubishi, maana mitaa niliyotaja hapo mwanzo yote ni mipya, changamoto ni moja tu hiyo mitaa mpya haina watu, utakuta nyumba moja wanaishi watu wanne tu, yaani familia ya baba mama mtoto na beki tatu
Na ndio maana hata upande wa usafiri Dom ni changamoto sana, Dom hakuna daladala za kutosha nadhani hii ni sababu ya uchache wa watu thats why daladala zote za Dom zinaishia sehemu moja na zinatosha (sabasaba) na zingine kidogo Majengo, My friend Mwanza hakuna eneo unaweza kuweka daladala za mji mzima sehemu moja zikatosha
Pia hapo hapo kwenye usafiri Dom ina route chache sana za daladala naweza kuziweka hapa, Nane nane - 77, Mipango-77, Ntyuka-77, Kwa massta (Nzugun)-77, Nkuhungu-77, Chan'gombe-77, Swaswa-77, Msalato-77,
pia kuna kidogo zinaishia majengo ambazo ni Mnada mpya- Majengo, Mkonze-Majengo pia. zipo daladala kama mbili au tatu zinajaribu kwenda Michese, unaweza nikumbusha nimesahau route ipi ya daradara hapo mkuu, maana ake route za daladala Dom hazizidi 11
Wakati huo huo mtu anaetoka Nanenane kwenda Chang'ombe kwa mfano hawezi kupata route ya moja kwa moja ni lazima aingie sabasaba achukue daladala lingine aendelee na safari, kuna sehemu kama Kikuyu hakuna daladala kabisa ni mwendo wa bajaji , njoo Kisasa anzia hapo Kwa mnama njoo mpka La Liga zunguka hiyo ring road Kisasa sekondari, Amazon ingia ndani ndani kote hakuna usafiri
Kufikia hatua mnaiongelea Mwanza najua mtakuwa mmeshafika mnapajua vizuri mm sitaki kueleza maana ndio nyumbani mnaweza kusema ni sehem gan kwa Mwanza pamoja na kuwa jiografia yake ni milima ni sehemu gani unaweza unga dalala ukiitoa Nyashana?( kwa ambao mnaiponda tu Mwanza kwa kusikia mnakosea sana) Mm mji yote Tz naijua
Tafuteni mafundi ujenzi au watu waliopo kwenye sekta ya ujenzi muulize kuhusu kasi ya ujenzi ilivyo Dom sasa hivi mtajua kuwa Dom pia imeanza kwenda taratibu,, ni tofauti sana na ilivyokuwa before na sababu ni kuwa nyumba zimekuwa nyingi lkn hazina watu, (maana Dom nyumba wanajengewa wageni na tayari wameshapata, wenyeji wapo wapo tu)
Nenda Kisasa, Swawa, Ilazo kote 30% ya nyumba hazina watu, na hapa nishauri tu uwekezaji wa real estate unaenda kudorora Dom, watu wamejenga lakini hakuna wapangaji Dom haina watu, mfano Dodoma soko la maana lenye watu lipo moja tu (sabasaba) na limebeba bidhaa zote japokuwa majengo kidogo inavyakula, ikitoka city center ya Dom center ndogo ndogo kama Buzuruga, Mecco, Nyakato, Kona ya Bwiru, Buhongwa, Nyegezi, Sabasaba(mbao), Nyasaka nk kwa Mwanza Dom huzikuti na hata ukizikuta ni ndogo sana kama Makuru, Meriwa, Kwa mnama
Maanake ni kwamba mjasiriamali mdogo wa genge la matunda na mboga mboga wa Mwanza kama yupo Buzuruga anachukulia bidhaa zake Mecco sokon kama yupo Buhongwa anachukulia hapo hapo Buhongwa ila Dom wote wanaenda Sabasaba mpaka mtu wa Chamwino anahemea sabasaba
Dodoma majengo marefu yaliyokamilika mpaka sasa ni matatu tu (Kambarage, PSSSF na Dom city hotel kwingine kote ni vijengo vya ghorofa tano kushuka chini
Ukubwa wa mji Dom inaanzia Nala upande wa magharibi, Mkonze na Ntyuka Kusini magharibi, Ng'ong'ona, UDOM, Iyumbu upande wa Kusini mashariki, Nane nane, Ilazo upande wa magharibi (hapa Ihumya naitoa maana hapo katikati Elishadai na St Peters kuna kipori, Chama Msalato na Mipango upande wa kasikazini hapo Dom ndio ilipo Mtumba ipo nje sana na katikati kuna eneo kubwa sana la wazi tunaitoa japo ipo nda ya halmashauri
Dom nimeifahamu yote ndan ya wiki moja na hakuna sehem unanidanganya,,,,, oyaaaaa eeeeeh? Njoo Mwanza sasa!!!
Kiukwel huwaga naumia sana kusikia mtu anaiongelea Mwanza na Dom, Mwanza ina manispaa mbili ndan ya mji (Ilemela na Nyamagana) Dom haina, Mwanza imekuwa jiji rasmi awamu ya tatu 2002 Dom ikawa 2017
Nyakato kuna viwanda vya kila aina Nondo, Soda(koka na peps zinatoka ndan ya mji) wakati Dom zinatoka Dar, Bia SBT na TBL wanafyatua ndani ya mji, idadi ya hotels route za safari za ndege ATCL na Precision Mwanza ina safari nyingi kuliko mji wowote ukiitoa Dar, Reli ya mwendokasi Dom hakuna fly over hakuna kote wameweka kifusi, Mwanza Fly Over ipo hakuna kifusi
Duh! Nyie endeleeen kuifananisha Mwanza na KiDodoma chenu, kuna jamaa amewahi kuniambia Dom kuna nyumba za kishua nikazitafuta Area D, Mlimwa C sikuziona kidogoooooo nikazikuta Michese zenye za ghorofa moja moja, nikamuuliza unaijua Kapripoint wewe, Bwiru kupata kiwanja tu mil 150 na kuendelea hapo bado hujavunja mawe maana unanunua mlima wenye mawe uvunje mwenyewe ndio kiwe kiwanja na kuvunja tu inagharimu mil 100 zingine ndio uanze kujenga hapo tayari mil 200 na kitu zimetumika huna hata msingi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Jiji la Kisasa ,very nice [emoji106]
Mwanza kuna flyover?
Dodoma inagongwa na Iringa pamoja na Moshi mshukruni mwenda zake aliipa status za Jiji. Vinginevyo dodoma ni manispaa tu.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unaleta picha za mwaka 2011 😂😂😂Mwanza bila uswazi haijakamilika 😁😁View attachment 2561006View attachment 2561007
Usifananishe Dom na mauswazi yenu ,kuwa na adabu kabisaDodoma inagongwa na Iringa pamoja na Moshi mshukruni mwenda zake aliipa status za Jiji. Vinginevyo dodoma ni manispaa tu.
Ghorofa 33 is it true au porojo tuMliopo Dodoma tafuteni mafundi ujenzi au yeyote anaejihusisha na masuala ya ujenzi muulize kuhusu kasi ya ujenzi Dom, mm nina mafundi niliwatoa Dar, Mwanza na Arusha sasa hivi 60% wamesharudi makwao kazi hakuna watu hawajengi tena kwa kasi ile ya 2017, baadhi ya wasiojua wanamweka Dr Samia hapa eti wafanyakazi wamerudi Dar
Mnaweza kutuambia ni nani karudi Dar? Maana hata Mtumba JPM kaondoka kuna ghorofa mbili tu ya TARURA na TAMISEMI, zile ghorofa zote zimeanza kujengwa na mama hebu jaribu kufikiria katikati ya mji Dom bado ina viwanja kutoka Morena ukiwa unatembea kuelekea CBE hapo kati kuna kipori, Makole yote ile ipo wazi, Kiwanja cha kula bata maarufu ni kimoja tu kilichopo pale Emausi karibu na jengo la GSM Capital city mall nimesahau jina lake
Tunavyoongea mda huu nipo Mwanza naona tofauti kabisa hapa Mwanza mda huu majengo ndio yanaamuka na sio serikali ni watu binafsi, hivi mnajua kama Makoroboi kuna mzigo wa ghorofa 33 kwenda juu unajengwa
Uwekezaji wa Mwanza ni wa sekta binafsi kwa kiasi kikubwa na sababu ni uwepo wa fursa nyingi za biashara mfano uvuvi, madini, kilimo nk, mnaweza kutuambia Dom zaidi ya uwekezaji wa real estate kwa ajiri ya wafanuakazi wa serikali ambao nao tayari wameshajitosheleza ni nn kinhine mwekezaji anaweza kufanya Dom?
Hebu angalia huu uwekezaji kwa Mwanza,,
Afya Mwanza ina mahospitali mengi zaidi ya private kuliko Dodoma Uhuru hospital, Agha Khan, Bugando, kuna moja ipo kona ya bwiru na sasa hivi wanajenga jengo kubwa la ghorofa 9 lipo mtaa wa Ghana jirani na Olympic
Benki ngoja nitaje tu zilizopo Mwanza ambazo Dom hazipo Standard Chaterd, KCB,, Stanbic
Viwanda, Pepsi Kolakola, TBL, SBT hapa nitaje hivyo tu lkn najua mnaijua vizuri Nyakato Industry Area maana kufikia mnaiongelea Mwanza mmeshafika
Usafiri Dom ina kampuni za mabasi kama nne au tano tu kubwa Kimbinyiko, Shabib, Satco, na wengine wengine wadogo kina Brightline wenye vigari viwili viwili,, unataka nitaje kampuni za Mwanza???? ,[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
Hivi mnaijua Rwagasore nyie kuhusu maduka makubwa ,,, kuna siku nilipata tenda ya kufanya finishing Dom mitaa ya Chadulu jirani na Pestana Pup kawaida yangu natumia rangi za master nilishaangaa Dom yote muuzaji ni mmoja tu Abuu Marangi na ndo mfanyabiashara mkubwa akifuatiwa na Ngozi
Hivi mnapataga ujasiri wapi wa kuifananisha Dom na jiji la Miamba?
Idadi ya watu kwa mjibu wa Sensa ya watu na makazi Dom yote kama mkoa inazidiwa watu na Tabora
Mwanza bila uswazi haijakamilika 😁😁View attachment 2561006View attachment 2561007
Ndio excuses mliyobakiwa nayo Kwa Sasa Ili kujifariji 😁 😁Unaleta picha za mwaka 2011 😂😂😂
Ghorofa 33 is it true au porojo tu
Uwanja wa ndege dodoma ni white elephant project.Usifananishe Dom na mauswazi yenu ,kuwa na adabu kabisa View attachment 2561009View attachment 2561010
🤣🤣🤣
Wewe unaleta picha ya Google map una akili au matope halafu utegemee ikuonyeshe majengo vile unataka wewe. Kuwa na shule basi japo kidogo.🤣🤣🤣 View attachment 2561014Unabana ,leta picha nzima kama hii.
Tulia dozi ikuingie weweUwanja wa ndege dodoma ni white elephant project.
View attachment 2561022
Dodoma mnayotupigia kelele