Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Unahisi tukiachana na CBD tukahesabu jengo moja moja la ghorofa mpaka lingine kwa mji mzima mwanza inatoboa kwa Dom?

Vipi ushaitembelea chinangali, CBE, Majengo,mazengo,nyerere square, sabasaba, developed cities area n.k huko kote majengo marefu yanazidi inuka tu ndugu yangu kitu pekee mwanza inaizidi Dom kwa sasa ni ile density/kusongamana kwa maghorofa katika eneo finyu la CBD yao ukilinganisha na Dom.

Dodoma CBD imetanuka nje ya kariakoo yao ndogo inayoitenganisha na CBD nakuleta mwonekano wa kisasa na majengo mazuri yaliyoachiana uwazi wa kupumua ukilinganisha na Zoo na siku nyumba za bati au kawaida zikishaondoka zote kupisha ghorofa CBD ya Zoo ikatafute ligi yake kwenye suala la CBD.
Kilaza kweli wewe hii Dodoma yenye ghorofa mbili iizidi City center ya Mwanza [emoji32]

Hapa kuna ghorofa moja tu jipya nalo ni hotel iliyopo karibu na white house nimeisahau jina owner nadhani ni serikali design mbaya ya kizamani kabisa.

Kwingine hakuna ni vijumba uchafu, ndio maana hata Vunjabei ya Dodoma ni robo ya ukubwa wa ile iliyopo Iringa.

Biashara za oneway na 7/7 zotee zinafungwa kuanzia saa 1 yani saa mbili ni mji unaanza kulala.
Usafiri wa kutoka city center ya wagogo saa tatu ni unabahatisha daladala bajaj ndio wana double bei.

Purchasing power ni ya hovyo wengi ya wanunuzi wa bidhaa za hawa wakoma ni wanafunzi na wafanyakazi wengine ni mandezi tu
 
Shughuli gani za kiuchumi zipo hapo Dodoma ambazo unaweza ukazilinganisha na Mwanza. Mwanza ndo kitovu cha biashara kanda ya ziwa na pia inaunganisha mpaka na nchi jirani. Hela nyingi za dhahabu uko Kahama, Geita zinakuja Mwanza. Ukiachana na dhahabu, fishing industry ipo juu sana.
 
Najua ni mara chache sana watu kuizungumzia Dodoma kwa sababu wanai-underrate nakudhani kuwa Dodoma imelala ukweli mchungu ni kuwa kwa kasi ya ukuaji wa mji huu kuna majiji mengi nchini yajiandae kukabidhi crown very soon akiwemo mbabe Mwanza ambaye so far bado anahold title la jiji kubwa after DSM wakati DOM yeye akishikilia title la jiji la Kisasa zaidi after DSM hayo ndo maoni yangu utaki leta evidence kuwa MWANZA CBD nizaidi ya DODOMA CBD

Hivyo kwa heshima ya Dodoma mpya na ya kisasa ambayo kwa mtizamo wangu binafsi inaichapa Mwanza 3-0 kwenye ukubwa wa City Center (CBD)
Kuanzia majengo mengi ya ghorofa, ukisasa, mpangilio, bustani na round about nzuri, purchasing power (vitu bei ni juu na watu wana-afford) ndiyo maana mabasi makali na ghali mengi uanzia safari zake hapa kuelekea Dar nasiyo vinginevyo.

Kingine Dodoma CBD bado inakuwa kila sekunde mijengo inazidi chepushwa tena project za maana, ila Mwanza CBD haina jipya sana zaidi ya soko linalojengwa pale hamna kingine chakutarajia kwa sasa, kinachoiangusha Dodoma CBD ni ubaya wa soko lake kuu la majengo(ombi langu kwa mamlaka husika walifanyie mpango wa maboresho linafubaza jiji) ila kwingine huko kote ni fire.

CBD ya Dodoma inaichapa mwanza upande wa barabara za lami, private cars na magari ya kifahari,mandhari ya kimjini mjini kama ni mgeni ukiwa mazengo ukajichanganya majengo huko kwa kina vunja bei bila kusahau uhindini n.k wawezadhani uko kariakoo ndogo,
Dodoma CBD ina city vibes ukilinganisha na mwanza CBD.

MADHAIFU:

I. Ukarimu na kauli za kibiashara(customer care) ni "F"

II. Usafi ni "F'' mifereji inanuka vinyesi plus taka zinatupwa tu ovyo na hakuna hatua yeyote inachukuliwa mara mia na halmashauri ya manispaa ya Singida.

III. Upande wa Mahoteli na viwanja nawapa "D" demand bado nikubwa kuliko kilichopo, ukiiondoa Morena ambayo nayo ni yakawaida sana bado hakuna hotel za maana.

IV. Hali ya hewa ya vumbi la kuwasha macho, ukame na unusu jangwa, hata kama umetupia nguo mpya na Kali vipi zinaappear zimefubaa nakupaukiana achilia mbali baridi kali usiku. (Tushirikiane wote kuakikisha Sera ya Dodoma ya kijani inatekelezwa kwa vitendo)

V. Shida ya MAJI hapa usishangae chumba kimoja kikilipiwa 15k na kingine kinachofanana nacho kwa kila kigezo kikilipiwa 30k kumbe kigezo ni kimoja kina maji na kingine hakina. Jamani SERIKALI timizeni majukumu yenu mruhusu jiji hili lifunguke zaidi na likuwe maana kikwazo kikuu ni hiki kabla ya vingine.

But all in all ukiondoa mapungufu hayo machache, mwanza CBD inakalishwa benchi kipindi cha kwanza cha mchezo hata kabla ya kipyenga cha mwamuzi kuamuru game lianze.

TAKE HOME
Ninachoipendea Dodoma; UZALENDO kwani karibia asilimia 95 ya majengo yote, mabango na mapambo CBD lazima neno DODOMA litaappear unlike mwanza na sehemu zingine za Tanzania hii.
Hizo ni kodi za Watanzania zilizokusanywa mikoani ndizo zinazojenga hapo acha ushamba eti magorofa majengo ya serikali hayo we unaona fahari.
 
Hali ya hewa Dodoma inakwaza sana...miti ipandwe kwa wingi tena kwa lazima...
 
We mgogo acha mabalaaa

Ivi pale Dodoma Wana garden nzuri kweli ?

Na hili la kisema Basi nzuri Zina anzia Dodoma kwenda Dsm ...hapa umepaishaaaa
 
Acha uongo wakulinganisha manispaa na jiji na mwishowe unajidumaza kwa kukosa exposure tafuta nauli ufike Dom kwanza afu uje ufute comment yako
jiji imetamkwa tu lakini dodoma hakuna quality za kuitwa jiji mji umejaa omba omba kila mahali ile airport pale ukishuka unaenda kupanda bodaboda alafu hata bunge sijui kwanini wali allocate likae pale barabarani yani bunge linapakana ukuta na chuo jamani mi nilitegemea liwe sehem flani nje ya mji waswahili hawafiki kirahisi sasa bunge nalo liko katikati ya mji hivi gari la matangazo likipita pale sauti haifiki ndani mule
 
Back
Top Bottom