Naomba rudi tena wiki hii ukapatembelee utuletee mrejesho, Manispaa ya Shinyanga ni mojawapo ya manispaa nzuri na kubwa, Shinyanga kwa ukubwa wake wenzake ni Musoma, Bukoba, Morogoro, Iringa,Tabora na siyo mji wa kulinganishwa na Kahama, Geita,njombe, kasulu,korogwe n.k
Kiuchumi hapa ndo nyumbani kwa matajiri wengi wa kanda ya ziwa, Shinyanga ina viwanda vingi ukilinganisha na manispaa nyingi hapa nchini. Miundombinu ya barabara nzuri na taa zake usiku kunavutia mno kama vile Singida jirani yake.
Uwezi pata shida kujua eneo la Shinyanga lililotengwa kwa ajili ya viwanda na makazi, utunzaji wa mazingira kwa kuruka pasipo kujenga maeneo yenye miti ya asili.
Kunafanya mji uwe wa kupendeza kimandhari ukitokea mwanza ukishavuka kiwanda cha jambo product na International school ya Savanna mandhari ya pale ni nzuri sana mpaka unafika CBD yao siyo haba wanamijengo ikiwemo ghorofa siyo haba kiasi cha kubezwa.
Shinyanga ina Old Shinyanga town na New Shinyanga town na hizo towns zote mbili zimejengeka kuunda mji mmoja, daima wapita njia ya Mwanza-Shy tumekuwa tukipita pale Mkoani kwenye ofisi za Manispaa na mbele kidogo utaona magodauni na mashine za kukoboa mpunga nakujikuta tunapajua sana Shy kiasi cha kupadharau kumbe hata town hatufiki na ukichukulia wasukuma nchi hii mlishawachukulia poa poa mnadhani kila wanapoishi hapajaendelea.