Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

πŸ˜‚Mkuu huku ndio usiguse kabisa ....wenzako tukiwaletea projects kama hizo huwa wanajificha kwenye kichaka cha "eti Dom inajengwa na Serikali, Mwanza inajengwa na private sector"πŸ˜€πŸ˜€πŸ‘‡πŸ‘‡
-NHC Medeli Projects
-NHC Chamwino Project
-NHC Iyumbu Satellite City
-Kitelela/Msalato Satellite City
-Watumishi Housing (Phase 1,Phase 2 ,Phase 3)
-TBA Project
-Njedengwa Projects
-Kisasa Hilltop Projects
-Mradi wa nyumba 3500 za Watumishi Nzuguni
-PSPF Project

.....and the list continues kilasiku
 
Mkuu

Unalinganisha mji uliojengwa kwa mipango ya Serikali dhidi ya mji uliojipigania wenyewe kwa juhudi za wakulima, wavuvi na wafugaji?

Unalinganisha mji wenye mamlaka rasmi ya uendelezaji (CDA Dodoma), dhidi ya mji usiokuwa na mipango mahsusi wa maendeleo kitaifa, mji unaoota kama uyoga porini?

Huu ni uonevu usiopimika.
 
Tatizo la hizo Nyumba ni copy &Paste Nyumba moja including hata mara 20 na ina accommodate Vitu vile vile
 
Pamoja na hayo yote Mji bado unasuasua wewe kuuza kiwanja tu tena potential area mpaka waweke drone akati huku vinagombaniwa
 
Exactly you nailed it...shida ya humu wanabishana kwa ushabiki badala ya "facts"
 
Kenya, Uganda, Rwanda, DRC na Sudan Kusini zimeamua kuweka nguvu ya pamoja kufanikisha ujenzi wa reli ya mwendo kasi SGR inayopita Afrika Mashariki.
Mawaziri wa uchukuzi kutoka mataifa hayo wamekubaliana kwa pamoja kutafuta wafadhili na wajenzi wa reli hiyo, kurekebisha mkataba wa maelewano na kuhusisha mataifa ya DRC na Sudan Kusini na vile vile jinsi ya kugawana majukumu ya kulinda reli hiyo ya SGR.
Waziri wa uchukuzi nchini Uganda Fred Byamukama amesema wamechukua mkondo huu kupunguza gharama ya kufanya biashara kuimarisha uchukuzi na kuunganisha mataifa hayo na pia kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Uganda imefikia hatua za mwisho za mkataba kati ya wafadhili kufanya ujenzi wa SGR kutoka Mpakani Malaba hadi mji mkuu Kampala.
Naye waziri wa Uchukuzi wa Kenya Kipchumba Murkomen amebainisha kwamba Kenya itarejea katika ujenzi wareli ya SGR kutoka Naivasha kwenda mpakani Malaba mwaka huu kwa kima cha dola bilioni 5.3 ambazo inakusudia kupata kutoka sekta ya kibinafsi.
Ujenzi wa SGR Afrika Mashariki umegawanywa kwa vipande, kutoka Naivasha mpaka Malaba kisha Uganda itaunganisha Malaba na Kampala, sehemu ya tatu ni kati ya Kampala , Bihanga Kasese - Mpondwe mpaka DR Congo sehemu ya nne ikiwa kati ya Bihanga mpaka Milima ya Mirama na kisha mji mkuu Kigali Rwanda, sehemu ya tano ni kati ya Tororo – Gulu, mpaka Sudan Kusini Pakwach na Vurra.
Rwanda inapojiunga na msukumo huu waziri wa uchukuzi Jimmy Gasore amesisitiza umuhimu wa ushirikiano ambao utaharakisha na kupunguza mzigo wa kujenga reli ya SGR na hivyo kuwa ya faida kwa mataifa hayo .
Katika mkutano huo pia waziri Murkomen na mwenzake wa Uganda Katumba Wamala waliidhinisha mkataba wa maelewano kati ya Kenya na Uganda kufadhili ujenzi wa SGR kati ya Naivasha Kisumu Malaba na pia Malaba hadi Kampala baada ya makubaliano mwaka 2023.
Mwaka 2014 mataifa ya Kenya Rwanda na Uganda yaliweka makubaliano kujenga reli ya SGR kutoka Mombasa , Kampala mpaka Kigali Rwanda lakini ujenzi huo alisimamishwa ghafla mfadhili mkuu China ilipokukataa kuendelea kuufadhili baada ya kukosa maelewano na Uganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…