Ile kitu Dodoma anamfanyia Mwanza kwenye uzi huu si poa kabisa; Yaani katoto ka juzijuzi tu hapa kamemtandika mkubwa mpaka ametubu;
Maeneo aliyoongoza Mwanza mpaka sasa dhidi ya mpinzani wake;
1. Ukubwa wa jiji
2. Maisha nafuu/duni
3. Idadi kubwa ya watu
4. Viwanda
5. Slums
6. Maji
7. Bandari na meli
8. Hali ya hewa
9. Poor infrastructure I.e barabara, taa, stendi n.k
10. Umasikini
Maeneo aliyoongoza Dodoma dhidi ya mpinzani wake;
1.Jiji la kisasa.
2. Kasi ya ukuaji na utanukaji wa jiji.
3. Mpangilio (hapa inaeleweka mwanza ni jiji la zero planning)
4. Shopping malls& super markets (mwanza hakuna hata mini zaidi ya rockcity mall)
5. Barabara za lami (Zoo hapa imepigwa miles ndefu)
6. Estates (mwanza hakuna)
7. Idadi ya jumla ya majengo yote ya ghorofa juu ya ardhi kwa jiji zima (ukiunganisha majengo ya CBD na UDOM pekee Mwanza chali kifo cha mende bila kuigusa Mtumba,kisasa,maeneo ya Estates,CBE, makole, majengo ya idara mbalimbali za umma na binafsi yaliyopo njia ya Kikuyu avenue n.k)
8. Majengo ya ghorofa ndefu za kufikia ghorofa kumi (imedhihirika mwanza ni ndoto kuna ghorofa moja tu la flow 16 basi)
9. Mzunguko wa pesa dom nimkubwa pamoja na purchasing power.
10. Wakazi wengi wanakipato cha kati na cha juu.
11. Facilities za mikutano, kumbi kubwa kwa ajili ya dhifa na vikao vya ndani na vya kimataifa.
12. Makao makuu ya serikali na wizara zote. I.e ofisi za wizara, jeshi,bunge na ikulu.
13. Kuna high demand ya huduma, starehe na accommodation kutokana na kipato kizuri hivyo spending nikubwa na wafanyabiashara wananufaika zaidi kuliko mwanza.
14. Idadi ya Round about na maeneo bora ya bustani za kupumzikia mjini
15. Makao makuu ya madhehebu kadhaa kama anglikana na nyumbani kwa misikiti mikubwa zaidi Tanzania.
16. Nyumbani kwa chuo kikuu kikubwa zaidi Afrika ya mashariki-UDOM na Taasisi ya moyo- Benjamini Mkapa.
17. Stendi na Soko la kisasa.
Matarajio ya Mwanza katika hatua za ujenzi au utekelezaji wa miradi iliyo kwenye mpango wa matekelezo:
1. SGR
2. Meli
3. Daraja la busisi
4. Airport
5. Stendi za magari
6. Soko kuu
Matarajio ya Dodoma katika hatua za ujenzi au utekelezaji wa miradi iliyo katika mpango wa matekelezo:
1. SGR
2. Bandari kavu
3. Ujenzi wa mji wa serikali au magufuli city
4. Ujenzi wa barabara za dual carriages way za njia nne katika barabara kuu nne za kuunganisha jiji la Dodoma pamoja na mikoa inayoizunguka dodoma.
5. Ukamilishaji wa nyumba za kuishi 1000 katika mradi wa iyumbu na maeneo mengine kama kisasa n.k
6. Ujenzi wa international Airport
7. Ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira cha kisasa
8. Ujenzi wa Arena
9. Ujenzi wa viwanda
10. Ujenzi wa BRT na commuter train
11. Ukamilishaji na ujenzi wa majengo mbalimbali ya maghorofa ambazo ni idara, taasisi, kumbi za mikutano na vitega uchumi kama vile mahoteli na malls pamoja na makazi ya watumishi mbalimbali wa mashirika ya umma na binafsi.
12. Ukamilishaji ujenzi wa ikulu
13. Ukamilishaji ujenzi wa kambi kuu ya JWTZ
14. Kuunganishwa na dar es salaam kwa njia 4
15. Mradi mkubwa wa Maji toka Ziwa Victoria.
Hivi jamani mpaka hapo bado kuna haja ya ku-battle, yaani unaanzaje kulilinganisha li-giant and super modern city na vijiji vikubwa kama Mwanza visivyo na CV yeyote wala future kubwa.