Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Kwani nimekosea nikisema ni moja kati ya mapanbo ya hapo jangwani Dodoma.
Bora mji unaopambwa na vitu icon vinavyopatikana katika majiji yote makubwa yanayoheshimika duniani kuliko jiji linalotegemea pambo la sanamu ya sato round about.
 
Unawa-umiza wenzio roho vitu vizuri kama hivi wavitoe wapi kama hawatoishia kukupostia fremu za maduka na majengo ambayo hayajaisha eti apartment.
JIBUNI ni hapa bas
IMG-20221105-WA0004.jpg
IMG-20221106-WA0016.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo tuachane nayo, we unafikiri nchi inaokota pesa? Yaani project kubwa kama uwanja wa ndege ifanywe chini ya kiwango bila kuhusisha utaalamu kwa mabilioni ya shilingi kisha kabla hata mkopo wenyewe haujaanza kurejeshwa, turudi tena kubomoa nakuanza upya?

Nchi masikini kama Tanzania bajeti yake iko taiti sana mtu anapo abuse power nakutumia fedha vibaya anai-cost nchi pakubwa, just imagine ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Mwanza kimefukia pesa kiasi gani ambazo zingetumika kuimarisha miundombinu ya afya?
Nini kifanyike acha ujinga wakuongea bila kuleta suluhisho.
 
Hyo terminal haujajengwa Kwa pesa za mikopo acha uongo wako ...pesa zimejengwa Kwa force account...za halmashauri ya manispaa ya ilemela na mwanza CC ...kwanza magufuli alisema Ile ni temporary block ...

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora umejibu wewe, na kama limekosewa je serikali ina mpango gani nalo?
 
Siyo vibaya kujiliwaza wakati ambao unaona kabisa uliyemdhania siye ndiye anakupumulia kisogoni, tumeshayaficha completely majiji matatu kwa kila kitu na wenyewe walikuwa wakijiliwaza kama ninyi kuwa Dom itapoa but unfortunately next ni wewe tupishe tu na ulichobakiza kwa sasa ni idadi ya watu tu si vinginevyo.
Dodoma inachoizidi mwanza ni bunge, ukame, vumbi la trachoma na hiyo outer ring road
 
Hata kama ingekuwa ni account ya escrow kiufupi ni matumizi mabaya ya pesa za umma, na waliofanya hivyo ni wana Mwanza tena halmashauri ya jiji lenyewe hivyo msitafute sababu kwa kutia tia huruma hili kukwamisha miradi mingine ya maana kama msalato kwa kuhalalisha neno upendeleo kwenye ujinga wenu wenyewe.
Na hiyo msalato ina umuhimu gani kwa sasa kama sio kujenga bila taaluma na kutokuangalia hali halisi ya mambo, hiyo airport itakuwa ni hasara kubwa kwa taifa, na litakuwa linachukua wasafiri wa kutoka nchi gani waje washukie hapo, uwanja wa ndege wa mwanza mnaufanyia figisu alafu tusiseme.
 
Nchi ina utaratibu wake na namna ya utekelezaji wa miradi lazima ufuate mtiririko uliowekwa na siyo kila kitu kinatekelezwa kwa hisia za kikundi cha watu au papara, hayo ni matokeo ya maamuzi mabovu yaliyofanyika katika awamu iliyopita yakiusisha halmashauri inayoitikia ndiyo mkuu hata kama majukumu siyo yao walipaswa kuyakataa na badala yake wali-abuse power ili wasifiwe na matokeo yake ndiyo haya.
Miradi ya dodoma n dar huwa inafuata misingi gani? Huwa sisikii mbungeni lakini nakuta imeanza kutekelezwa huu ujinga nao unaitwaje?
 
Bora mji unaopambwa na vitu icon vinavyopatikana katika majiji yote makubwa yanayoheshimika duniani kuliko jiji linalotegemea pambo la sanamu ya sato round about.
Hiyo picha ya round about ya huyo sato anayetema maji, niliiona nilipokuwa Frankfurt, Germain.... Hilo sanamu ni maarufu kuliko jengo la bunge.
 
Hiyo picha ya round about ya huyo sato anayetema maji, niliiona nilipokuwa Frankfurt, Germain.... Hilo sanamu ni maarufu kuliko jengo la bunge.
Kwahiyo unajinasibisha kwa copy & paste[emoji23]
 
Miradi ya dodoma n dar huwa inafuata misingi gani? Huwa sisikii mbungeni lakini nakuta imeanza kutekelezwa huu ujinga nao unaitwaje?
Miradi ya Dodoma ni miradi ya kimkakati na bajeti yake utengwa na kuidhinishwa kila awamu na bunge, hivyo usianze kuleta mbishe za kiswahili
 
Na hiyo msalato ina umuhimu gani kwa sasa kama sio kujenga bila taaluma na kutokuangalia hali halisi ya mambo, hiyo airport itakuwa ni hasara kubwa kwa taifa, na litakuwa linachukua wasafiri wa kutoka nchi gani waje washukie hapo, uwanja wa ndege wa mwanza mnaufanyia figisu alafu tusiseme.
Kwanini unafikiri kiwanja cha ndege msalato ni project hewa?

Kwanini unafikiri Mwanza ndiyo inastahili kuwa na miundombinu bora ya usafiri wa anga na si Dodoma?
 
Kwanini unafikiri kiwanja cha ndege msalato ni project hewa?

Kwanini unafikiri Mwanza ndiyo inastahili kuwa na miundombinu bora ya usafiri wa anga na si Dodoma?
Dodoma ipo karibu na Dar, na tayari Dar kuna uwanja mkubwa wa kimataifa, je hao wageni wataacha kutumia JNIA na washukie msalato? Je msalato itapokea wageni wa aina gani? Jibu hayo nakuja kukupa facts kuwa hiyo msalato ni upotevu wa fedha kwenye nchi maskini kama hii
 
Dodoma inachoizidi mwanza ni bunge, ukame, vumbi la trachoma na hiyo outer ring road
Ungeendelea kutaja tunavyowazidi kuwa si bunge tu bali ikulu, jiji la kisasa la kiserikali, estates,majengo ya taasisi mbalimbali, vyuo vikuu, planned city, makazi bora, kilomita ndefu za mtandao wa barabara za lami mjini, bustani za kupumzikia,n.k

Bora unusu jangwa wenye trachoma kuliko kunywa maji yenye mchanganyiko wa vinyesi na mwisho wa siku ni kufa kwa kansa.
 
Hapo kwenye estate na makazi bora elezea vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom