Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?


View: https://www.instagram.com/p/C4yCQ2yLUwn/?igsh=MXZ1ZzQwYzZ1YmJzdA==
1456376542.jpg
737237812.jpg
-43745534.jpg
1638038778.jpg
 
Mkuu ni suala la muda maana Dodoma inakuja kwa kasi ya 5G huku Mwanza inachechemea
Mwanza haipati support ya serikali ndiyo maana ya kusuasua. kitu kimoja kingefanyika Mwanza ingebadilika sana nayo ni upanuzi wa uwanja wa ndege kuwa wa kimataifa na njia nne barabara za Kenyatta na Nyerere.
 
Mwanza haipati support ya serikali ndiyo maana ya kusuasua. kitu kimoja kingefanyika Mwanza ingebadilika sana nayo ni upanuzi wa uwanja wa ndege kuwa wa kimataifa na njia nne barabara za Kenyatta na Nyerere.
Viongozi kusema uongo ni siasa ila mwananchi akiidanganya serikali ni kizaazaa viongozi wetu kwakweli kwenye hili la uwanja wa ndege wa kimataifa mmeshadanganya sana ifike mahali muone aibu!
 
Nasikia Aloyce Nyanda atakuwa na kongamano Mwanza la tathmini ya miaka 3 tarehe 30.3.2024 mimi nasema kama uko serious kweli suala la uwanja wa ndege wa Mwanza iwe ni ajenda kuu ikifuatiwa na Barabara za Nyerere na Kenyata kuwa njia nne katika tathmini yenu, lisiwe kongamano la uchawa na kampeni msaidieni Rais kwa kusema ukweli kanda ya ziwa imetelekezwa ukiacha miradi michache ya kimkakati. Kongamano liwe la ukweli.
 
Kitombile Jengo jipya liko wapi mbona ni umaliziaji wa lile like godown lenu? 😆😆😆😆👇👇👇

View: https://youtu.be/LditTksgQ68?si=rRe699A2g_2f9CDq

Wanamalizia jengo la zamani ndio ao TAA pamoja na serikali tukiwemo sisi wadau wa Mwanza tulilidhiaki ilo jengo kwa maneno mengi ikiwemo kuliita godown au supermarket, hivi karibuni alisikika mkuu wa wilaya ya Nyamagana, ndugu Amina Makilagi akisema ilo jengo watalifanya supernarket na watajengo jengo jipya la hadhi ya kimataifa cha ajabu hao hao wanafiki wanamalizia jengo walilosema halina kiwango chochote na wala halina kigezo cha kimataifa..

Hapa kuna mambo mengi ya mkanganyiko, hapa kwa sisi wa jicho la tatu tunaona bado kuna figisu juu ya huu uwanja, huu ukarabati hauwezi kutufanya tuwe wakimataifa hata siku kwa bilion 29, hapa wanaweza kuuita international airport lakini sijaona bado kigezo cha kimataifa.

Tukija kwenye thamani ya mradi tukilinganisha na pesa ilitajwa na serikali kuwa itatumika naona kama vile sijui serikali inatuchukuliaje sisi watu wa Mwanza, jengo ilo la abiria lilikuwa limeisha bado vitu vidogo ikiwemo parking hata hiyo parking ya magari wanayosema watajenga tayari blocks kwaajili ya pavement za parking tyr zilikuwa zimejengwa tena nyingi sana kutosha eneo lote la mradu, tukisema mashine za ndani tayari mchina alikuwa ameleta machine mbili za kufunga, hizo bilion 29 zinatumika wapi???? kama barabara ya kuingia kupaki gari haziwezi kuzidi mita 100, kama finishing na nini na madoido mengine bilion 5 ilikuwa inatosha.

Swali kwanini wameendeleza jengo lisilokuwa na viwango vya kimataifa?
Zile bilion 30 za mwanzo walizosema hawali na wakati wa kusaini wakasema 29 bilion je hiyo bilion moja ipo wapi?
Je wakikamilisha ilo jengo je kweli uwanja wetu wa Mwanza utakidhi vigezo vya kimataifa?
Je thamani ya mradi na hizo pesa zilizowekwa na serikali je vinaendana?

N.B Nalikumbusha shirika la NSSF wakumbuke ahadi yao ya kujenga hotel ya nyota nne hapo uwanja wa ndege hii kidogo itainua hadhi ya uwanja huo na sio hizi ngonjera za kitoto za hii serikali(TAA)
 

hawa waandishi wa serikali wengine naona viatu haviwatoshi,hakuna kitu kinaitwa Kituo Cha mahiri Bali ni Kituo mahiri,sijui kiswahili alipata ngapi shuleni? kwenye matumizi ya lugha ukishaweka kiunganishi "Cha" unabadili kabisa maana ya neno, yaani inakuwa mahiri ndiye mmiliki wa hicho kituo
 
Back
Top Bottom