Mzee wa fact upungufu husabibisha shida. Unaweza tumia maneno mengi kuzunguka pale pale.👉👉Nikusahihishe tu Dom hakuna "shida" ya maji ila kuna "upungufu" wa Maji kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kijamii especially baada ya Serikali kuhamia rasmi na kwa miradi inayoendelea.Mwanza yenyewe licha ya kuzungukwa na Ziwa Victoria bado wana changamoto ya Maji.
👉👉Hakuna mji wowote Tanzania ambao maji yanapatikana 24/7 mwakamzima.
Na kwa miradi ya maji inayoendelea kujengwa Dom kwamfano mradi wa Bwawa la Farkwa,mradi wa kuongeza visima Mzakwe n.k ishu ya maji baada ya miaka michache Dom itakua historia.
👉👉Ukija kwenye suala la usafi Dom ni mojawapo ya miji misafi apa Tanzania huwezi kuikosa kwenye top 5 ...umekiri mwenyewe kuwa wana barabara nzuri na mtandao mpana wa barabara za lami. Ukienda soko la Majengo ulilolitaja hili limezungukwa na mfereji/mto ambao ni msafi mwakamzima ingekua miji mingine ule mfereji ungeshageuzwa dampo la takataka. Dom ni mji pekee Tanzania wenye dampo la kisasa na la ainayake lililopo Chidaya-Mvumi Road yale malori yanayobeba takataka za kwenye makontena yote yanaenda kumwaga hizo taka kwenye hilo dampo.