Kuna habari kuwa Gen Z wa Kenya wana mpango wa kukinukisha tena. Katika kusikiliza habari baada ya kutekwa kwa mchoraji vibonzo vinavyompinga Ruto aitwaye Kibet Bull, wamesema kuna watekaji toka nchi jirani. Kumbuka. Wakati wa maandamano ya Gen Z kulizuka shutuma kuwa askari polisi wa Tanzania walikuwa Kenya kuteka wakenya na serikali yetu haikukanusha tena kwa ukali kiasi cha kufanya iwepo imani kuwa kuna namna inashiriki hasa ikizingatiwa kuwa utekaji nchini Tanzania ni jambo la kawaida hasa baada ya rais kusema hivyo.