Je, ni kweli kuwa Utumishi watapangia walimu vituo kwa kuchagua wenye GPA kubwa?

Je, ni kweli kuwa Utumishi watapangia walimu vituo kwa kuchagua wenye GPA kubwa?

Mto wa mbu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2021
Posts
2,228
Reaction score
3,045
Hello wakuu,

Kuna tetesi nimezipata kuwa Utumishi ,hawatawafanyisha usahili walimu, badala yake wame wamechagua selection criteria, nazo ni mwenye GPA kubwa atapata ajira.

Na tetesi zinasema kuwa below 3.0, unaweza husi chaguliwe.

Je, yanaukweli hayo? Na ni kweli mwenye GPA ya 4.0 anaweza kuwa mwalimu mzuri kuliko mwenyewe GPA ya 2.0?

Karibu
 
Si lazima. GPA ni mojawapo tu ya vipimo vingi vinavyoweza kuonyesha ufanisi na mafanikio ya mwanafunzi. Mwalimu mwenye GPA kubwa anaweza kuwa na maarifa mazuri na ujuzi mkubwa, lakini sio lazima awe bora kuliko mwalimu mwenye GPA ndogo. Mambo mengine kama vile uzoefu wa kufundisha, uwezo wa kuwasiliana vizuri na wanafunzi, na jitihada zinazoonyeshwa pia ni muhimu katika kufanya mwalimu kuwa bora.
 
Si lazima. GPA ni mojawapo tu ya vipimo vingi vinavyoweza kuonyesha ufanisi na mafanikio ya mwanafunzi. Mwalimu mwenye GPA kubwa anaweza kuwa na maarifa mazuri na ujuzi mkubwa, lakini sio lazima awe bora kuliko mwalimu mwenye GPA ndogo. Mambo mengine kama vile uzoefu wa kufundisha, uwezo wa kuwasiliana vizuri na wanafunzi, na jitihada zinazoonyeshwa pia ni muhimu katika kufanya mwalimu kuwa bora. Hivyo, ni muhimu kutazama mambo mengi zaidi ya GPA pekee wakati wa kuchagua mwalimu bora.
Hayo mambo mengine watayatizama vipi? Angalau kungekuwa na interviews.
 
Hayo mambo mengine watayatizama vipi? Angalau kungekuwa na interviews.
Hoja yangu ipo kwenye G.P.A, ukisema bora interview je ni lini wameajiriwa kwa interview na je, walimu walio ajiriwa miaka yote sio bora?

Vigezo walivyotumia miaka yote kuajiri watumishi wa kada ya elimu waendelee navyo kama wameamua kutoitisha interviews.
 
Kwani hayo umeyatoa wapo, haujasema source of information au tujadili tetesi?
 
Iko hivi GPA haiokotwi ni inatafutwa kwa jitihada kubwa, kwa maono ya nje na ya kawaida maamuzi ya waajiri yanaweza kuwa mazuri, lakini critically hatuwezi kuamini kuwa GPA inabeba uhalisia wa utendaji kazi wa asilimia zote za muajiriwa, ila wakipata wamepata kwa sababu no good comes easier!!!
 
Ila hata vyuomi Ili uwe Tutorial lecturer lazima uwe na GPA ya 3.8+
 
Hoja yangu ipo kwenye G.P.A, ukisema bora interview je ni lini wameajiriwa kwa interview na je, walimu walio ajiriwa miaka yote sio bora?

Vigezo walivyotumia miaka yote kuajiri watumishi wa kada ya elimu waendelee navyo kama wameamua kutoitisha interviews.
Kila jambo lina mwanzo, ndio waanze sasa na GPA ikiwemo.
 
Back
Top Bottom