Je, ni kweli kwamba China imesababisha mgogoro wa chakula duniani?

Je, ni kweli kwamba China imesababisha mgogoro wa chakula duniani?

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG211314104576.jpg


Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limetoa “Ripoti ya Mgogoro wa 2022 wa Chakula Duniani”, ikisema dunia itakabiliwa na uhaba wa chakula ndani ya wiki 10 zijazo. Hili ni suala kubwa linalohusisha usalama wa chakula wa mabilioni ya watu duniani, hivyo linafuatiliwa sana. Kwa mara nyingine tena,vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vimeipaka matope China kwa kutoa ripoti mfululizo hivi karibuni, vikiishutumu China kwa kununua na kuhifadhi zaidi ya nusu ya mahindi na ngano duniani, na kudai China inapaswa kuwajibika na upandaji wa bei ya vyakula na mgogoro wa chakula duniani. Lakini huu si ukweli!

Takwimu zinaonesha kuwa, maagizo ya ngano ya China kutoka soko la kimataifa kuanzia Januari hadi Aprili mwaka 2022 yalikuwa tani milioni 3.75, na kupungua kwa asilimia 1.8 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Kwa mwaka mzima uliopita, China ilinunua tani milioni 9.77 za ngano, na mauzo ya jumla ya ngano duniani mwaka jana yalikuwa ni tani milioni 206. China, yenye karibu asilimia 20 ya watu duniani, ilichukua chini ya asilimia 5 tu ya biashara ya ngano ya kimataifa. Sasa inawezekanaje kuwa China imedhibiti soko la kimataifa?

Katika biashara ya mahindi duniani, kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu, China iliagiza jumla ya tani milioni 9.81 za mahindi kutoka nje ya nchi. ikilinganishwa na maagizo ya nafaka hiyo ya China ya mwaka jana, hiki ni kiwango cha kawaida, na China haijaongeza maagizo ya mahindi kwenye soko la kimataifa.

Kuhusu akiba ya nafaka, ikiwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani, ili kuhakikisha usalama wa chakula, China imedumisha akiba ya chakula kwa takriban tani milioni 300 kwa miaka mingi. Lakini nafaka nyingi hizi huzalishwa ndani ya nchi. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2021, kiwango cha kujitosheleza kwa nafaka kuu tatu za China, ambao ni mchele, ngano na mahindi, kilifikia asilimia 98. Maana yake ni kwamba hata China isiponunua kabisa chakula kwenye soko la kimataifa, inaweza kujitosheleza kabisa. China inalisha asilimia 20 ya watu wote duniani, kwa kutumia chini ya asilimia 9 ya mashamba ya kilimo duniani, na ni mchango mkubwa zaidi wa China kwa usalama wa chakula duniani.

Mbali na kukidhi mahitaji ya ndani, China pia imekuwa ikitoa mchango muhimu katika kutatua matatizo ya chakula duniani. Katika miaka 40 iliyopita, mchele chotara wa China umekuwa maarufu katika nchi mbalimbali za Afrika, Asia na Amerika, na maeneo ya upandaji wa mchele huo kwa mwaka yamezidi hekta milioni 8. Huko Madagascar, mchele chotara umechapishwa hata kwenye pesa ya nchi hiyo. Aidha, mara kwa mara China hutoa msaada kwa nchi zinazokabiliwa na njaa. Kwa mfano, tangu mwanzo wa mwaka huu, China imetoa misaada ya chakula kwa nchi kadhaa za Pembe ya Afrika ambazo zinakumbwa na ukame mbaya.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limesema katika ripoti yake kwamba, mgogoro wa chakula uliopo hivi sasa duniani unatokana na sababu tatu, ambazo ni vita, ongezeko la bei ya mafuta na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, huku mzozo kati ya Russia na Ukraine ambao umesababisha sababu mbili kati ya hizo tatu. Zaidi ya hayo, wakati dunia inakabiliwa na njaa, zaidi ya nchi 20 zilizoendelea ikiwemo Marekani zinageuza tani milioni 300 za chakula kuwa nishati, ili kukabiliana na upunguvu wa nishati na gesi. Aidha, mashirika makubwa zaidi ya kimataifa ya biashara ya chakula ADM, Bunge, Cargill, na Louis Dreyfus yanadhibiti zaidi ya asilimia 80 ya biashara ya nafaka duniani. Miongoni ya mashirika hayo, matatu yanatoka Marekani na moja linatoka Ufaransa, na yanapata faida kubwa kutokana na ongezeko la bei ya chakula duniani.

Ni wazi kwamba, anayesababisha mgogoro wa chakula duniani, anachochea mgogoro huo, na anayenufaika na mgogoro huo anafahamika. Na kupaka matope China katika swala hilo ni hila nyingine iliyofanywa na nchi za Magharibi.
 
Back
Top Bottom